Muda mfupi baada ya mwigizaji
Wema Sepetu kuonyesha nyumba yake mpya ya milioni 400 kwenye kipindi cha
Take One Clouds Tv baadhi ya wabongo walianza kutoa maoni kwamba hiyo
nyumba sio ya Wema, haiwezekani akamiliki nyumba ya namna hiyo.
Haikuishia hapo tu, hata baadhi
ya magazeti yalifichua siri kwamba mmiliki wa hiyo nyumba sio Wema ni
mama mmoja ambae ni mmiliki wa hospitali moja Dar es salaam.
Lawama za wachache pia zilitolewa kwa Zamaradi Mketema kwamba ameitoa hiyo stori huku akijua sio kweli inamilikiwa na Wema.
Zamaradi ameamplfy na
millardayo kwa kusema “mimi ni Mwandishi, unapokwenda kufanya
interview na mtu ninachotakiwa kusikiliza ni kile ninachoambiwa na mtoa
habari lakini sio ninachokijua au kusikia kwa watu, nilimuuliza hii
nyumba ni yako? akajibu kweli yeye ndio mmiliki sasa siwezi kubisha,
magazeti yanakosea kusema mimi naipotosha jamii ya watanzania…
sijaipotosha na kama kweli ile sio nyumba yake mimi sitakiwi kulaumiwa”
Kwenye sentensi nyingine
Zamaradi amesema “kwenye show ya Take One ndani ya wiki mbili zijazo
Wema amekubali kwamba atautoa uthibitisho kuonyesha kwamba ni mmiliki
halali wa hiyo nyumba japo siwezi kuutaja ni uthibitisho gani”Chanzo cha habari millardayo.com
No comments:
Post a Comment