Mkurugenzi
wa Kitengo cha Biashara cha kampuni ya Precision Air, Patrick
Ndekana(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba
na Vodacom Tanzania ambapo wateja wataweza kulipia tiketi za usafiri
kupitia huduma ya M-Pesa,kulia ni Mkuu wa kitengo cha huduma za fedha wa
Vodacom Tanzania Bw. Innocent Ephraim.
*******
Kampuni
ya usafiri wa anga ya Precision air hii leo imeingia kwenye mkataba na
Vodacom Tanzania ambapo wateja wataweza kulipia tiketi za usafiri
kupitia huduma ya M-Pesa.
Ili
kufanya malipo mteja atatakiwa kupiga namba *150*00# na kuchagua malipo
ya bili kupitia orodha ya M-pesa na kuingiza namba ya biashara ya
Precision Air ambayo ni 333777 ikifuatiwa na namba ya malipo na kiasi
cha fedha itakayolipwa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha
Biashara cha kampuni ya Precision Air, Patrick Ndekana, amesema kuwa
njia hiyo ni ya haraka, rahisi na itaokoa muda kwa wateja.
“Tunafurahi kuingia katika ushirikiano huu na Vodacom Tanzania,
Tunawahimiza wateja wetu kutumia huduma hii ili kuokoa muda na kufanya
malipo yao katika njia ambayo ni rahisi na ya haraka,” alisema Ndekana.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Kifedha cha Vodacom
Tanzania, Innocent Ephraim, alibainisha kuwa ushirikiano huo utatoa njia
badala katika malipo ya tiketi, na kusisitiza kuwa huduma ya M- pesa ni
salama, haraka na niya uhakika, kwa kuwa imeleta mapinduzi katika
huduma mbalimbali za kifedha tangu kuanzishwa kwake miaka mimne
iliyopita.
“Tunaamini
kuwa tutatoa huduma bora kwa wateja wetu. Tunajivunia ushirikiano huu
na tunatarajia utakuwa na mafanikio makubwa katika kukidhi mahitaji ya
huduma kwa wateja wetu,” alisema Ephraim.
Huduma
ya M-Pesa ya Vodacom Tanzania ina mawakala zaidi ya elfu 20,000 nchini
kote, na ni pekee ambayo inaongoza, kwa usalama na ubora katika kukidhi
mahitaji ya huduma za kifedha kwa Watatanzania walio wengi.
Kampuni ya Precision Air inatoa huduma zake katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, na kufika katika maeneo mengi ya nchi kwa siku.
Sasa
kampuni hiyo ina ndege tano zenye uwezo wa kubeba abiria sabini aina ya
ATR 72-500, na ATR 42 yenye uwezo wa kubeba abiria arobaini na nane na
ndege nyingine tatu aina ya Boeng 737. Na sasa iko katika mpango wa
kuongeza ndege nyingine aina ya E- jets na ATR.
Mkuu
wa kitengo cha huduma za fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Innocent
Ephraim,akionesha bango lenye maelekezo muhimu ya kufuatwa ambayo
yatawafanya wateja wapate huduma ya kulipia tiketi za usafiri kupitia
huduma ya M-Pesa kwa urahisi zaidi,kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha
Biashara cha Precision Air, Patrick Ndekana.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Precision Air wakifatilia kiumakini mkutano wa
waandishi wa habari kuhusiana na mkataba wa Vodacom Tanzania na kampuni
yao ambapo wateja wa Precision Air wataweza kulipia tiketi za usafiri
kupitia huduma ya M-Pesa.
Waandishi
wa habari wakiwa kazini wakati wa Precision Air na Vodacom Tanzania
walipokuwa wakitangaza mkataba kuhusiana na wateja wa Precision Air
kuweza kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa.
No comments:
Post a Comment