Jeshi la Kenya limesema hakuna
uwezekano wa kufanya mazungumzo na kundi la Al Shabaab ambalo limesema
litawaua mateka wanaoshikiliwa nalo kama Kenya haitawaachia wafungwa
waislamu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Cyrus Oguna amesema video ya mateka wanaoshikiliwa iliyooneshwa na kundi la Al Shabaab, si ya mateka wa kivita. Pia amesema Kenya haiwezi kuiambia Uganda iwaachie watu wanaoshikiliwa nchini Uganda kwa makosa ya ugaidi, kama kundi hilo linavyotaka, na wale wanaoshikiliwa nchini Kenya ni wale waliokamatwa kwa makosa mbalimbali.
Kundi la Al Shabaab limetoa taarifa ikiitaka serikali ya Kenya iwaachie waislamu wote wanaoshikiliwa kwa makosa ugaidi nchini Kenya, na ihakikishe kuwa waislamu waliopelekwa Uganda kutokana na makosa ya ugaidi wanaachiwa huru.

No comments:
Post a Comment