KILE kinyang’anyiro cha kumsaka Redd’s Miss IFM sasa kimefikia
patamu ambako warembo 10 bomba watapanda jukwaani katika kuwania taji
hilo Mei 25, kumsaka mrithi wa mrembo atakayevua taji hilo Fina
Revocatus.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika Hoteli ya JB Bellmonte
iliyopo Jengo la Golden Jubilee, maeneo ya Posta Mpya, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu
wa Redd’s Miss IFM, Daniel Sarungi alisema mshindi wa taji hilo
ataondoka na kitita cha sh mil.1.
“Warembo 10 ndio watakaoshiriki katika shindano hilo na mshindi
ataondoka na sh mil 1, huku washindi wengine watatu tukitarajia kuwapa
zawadi nyingine nzuri zaidi,” alisema Sarungi.
Meneja wa Redd’s Original ambao ni wadhamini wakuu wa Redd’s Miss
Tanzania, Victoria Kimaro alisema wanajivunia kuwa sehemu ya udhamini
wa shindano hilo na wanaamini warembo hao watafanya kweli zaidi na
kutwaa taji la Miss Tanzania.
“Hili shindano la Redds Miss IFM litakuwa moto, kwani tutalipa
sapoti kubwa zaidi na kuhakikisha anatoka mrembo atakayetwaa taji la
Redd’s Miss Tanzania,” alisema Victoria.
No comments:
Post a Comment