USAJILI wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulifungwa usiku wa kuamkia leo
Jumanne, huku Simba na Yanga zikigongana uso kwa uso kwa wachezaji
wawili; Mrisho Ngassa na Moses Oloya.
Mpaka usiku saa sita usiku wakati usajili
ukifungwa, hakukuwa na muafaka kati ya Simba na


Moses Oloya (kushoto) na Abel Dhaira
Yanga, kwani zote
zimepeleka jina la Ngassa na zimeacha nafasi moja ya Oloya.
Simba imewasilisha majina 28 huku Yanga ikienda na majina 29 kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Simba na Yanga zimefanya mazungumzo na Oloya anayecheza klabu ya Saigon ya Vietnam ambaye mkataba wake unamalizika Oktoba lakini amewaambia atafanya uamuzi baada ya ligi ya nchi hiyo kumalizika Agosti 31.
Katika orodha ya timu hizo kila moja ina wachezaji wanne wa kigeni na wamebakiza nafasi moja ya Oloya.
Simba ina raia wa kigeni Joseph Owino na Abel Dhaira wa Uganda, Amis Tambwe na Kaze Gilbert wote wa Burundi.
Yanga ina Hamis Kiiza wa Uganda, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima wa Rwanda pamoja na Didier Kavumbagu wa Burundi.
Kikanuni kila klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji watano wa kigeni, lakini Simba na Yanga kila moja imeacha nafasi moja kwa ajili ya Oloya.
Usajili wa pili utaanza Agosti 15 kwa kipindi cha mwezi mmoja na utamalizika Septemba 15 ukihusisha wachezaji huru tu, upenyo ambao kati ya Simba na Yanga zitautumia kumalizana na Oloya.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala aliliambia Mwanaspoti jana Jumatatu jijini Dar es Salaam kuwa: “Tumewasilisha majina 28 ya wachezaji wetu TFF na jina la Ngassa (Mrisho) likiwemo.”
Mtawala alisema wamebakiza nafasi mbili kwenye usajili huo na nafasi moja ni ya Moses Oloya na nyingine wanaweza kuitumia kwenye usajili mwingine wa Agosti 15.
Simba inadai ina mkataba wa mwaka mmoja na Mrisho Ngassa ambaye amekanusha vikali kuhusu kauli hiyo. “Sina mkataba wowote na Simba. Nilikuwa nikicheza Simba kwa mkopo nikitokea Azam FC. Sijasaini mkataba na Simba, baada ya ule wa Azam kumalizika,” alisema Ngassa.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amewahi kusema siku za nyuma
kuwa: “Kama Simba wanasema wameleta mkataba wa Ngassa TFF na ukasajiliwa
waambie wawaonyeshe, kwa nini wanaficha. Kwa sasa hatuwezi kusema
lolote ingawa muda ukifika kila kitu kitawekwa hadharani.”
Usajili mpya wa Simba uliowasilishwa TFF ni Makipa: Abou Hashim, Andrew Ntalla na Abel Dhaira. Mabeki: Issa Rashid, Omary Salum, Rahim Juma, Hassan Khatib, Haruna Shamte, George Owino, Gilbert Kaze na Shomari Kapombe.
Viungo: Abdallah Seseme, William Lucian, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Said Ndemla, Abdulhalim Humoud, na Adeyoun Saleh.
Mawinga: Mrisho Ngassa, Ramadhan Singano, Ibrahim Hussein, Haroun Athuman, Marcel Kaheza na Edward Christopher. Mastraika: Amis Tambwe, Betram Mombeki na Sino Agustino
Usajili wa Yanga ni: makipa; Ally Mustapha, Deogratius Munishi na Yusuph Abdul.
Mabeki: Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub, Kelvin Yondan, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajabu Zahir, Ibrahim Job na Issa Ngao.
Viungo: Athuman Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Salum Telela, Hamis Thabit na Bakari Masoud.
Mawinga: Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Abdallah Mguhi na Reliant Lusajo. Mastraika: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerry Tegete, Hussein Javu, Shaban Kondo na Said Bahanuzi.
Kuna vita mbili kubwa zinakuja mbele kwa Simba na Yanga, nayo ni nani atampa Ngassa na nani atamkosa Oloya.
Credit: MWANASPORTS
No comments:
Post a Comment