VITA mpya imeibuka ikiwahusisha warembo wa Bongo Movies, Wema Isaac
Sepetu na Irene Pancras Uwoya kufuatia kuanzisha vipindi vya runinga kwa
mpigo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Clouds Media Group,
Ruge Mutahaba, katika harakati za vipindi hivyo, alianza Wema kwa
kuanzisha ‘aidia’ ya kipindi kipya kiitwacho In My Shoes ambacho
kitaanza kuoneshwa kuanzia Alhamisi hii, saa tatu na nusu usiku kupitia
Clouds TV.
Alisema baada ya Wema kutengeneza kipindi hicho na kupata maoni
mengi, Uwoya akajibu mapigo kwa kuanzisha cha kwake kinachoitwa Paradise
ambacho kitakwenda hewani Jumanne hii (kesho).
“Mashabiki wa Clouds
TV watapata kuona vita ya kibiashara, Uwoya atakuwa akionekana katika
kipindi hicho ambacho kitakuwa kinahusu upakaji rangi katika nyumba za
watu mbalimbali huku Wema naye akikimbiza katika In My Shoes,” alisema
Ruge.
No comments:
Post a Comment