MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness
Malinzi ‘Diva’ amesema alichokuwa anahitaji katika sakata lake la kudai
ameibiwa ‘idea’ ya Kigoma All Star East Africa Tour na Mhe. Zitto Kabwe
ni kupewa heshima yake (appreciation) tu.
Loveness
Malinzi ‘Diva’ | Mhe. Zitto Kabwe.
Katika maelezo yake, Diva amefunguka kuwa walijadili na Zitto kuhusu
idea hiyo lakini badala yake akashangaa mheshimiwa anampotezea katika
utekelezaji kitu ambacho anadai siyo ‘feya’
“Angalau basi angenitaja
kama kunishukuru kwa kutoa mchango wangu katika Kigoma All Star Tour
lakini hakufanya hivyo na hata nilipomsisitiza aliniletea siasa,”
alisema Diva.
Jitihada za kumpata Zitto hazikuzaa matunda ila tunaendelea kumsaka.
Jitihada za kumpata Zitto hazikuzaa matunda ila tunaendelea kumsaka.
No comments:
Post a Comment