Kiungo
mshambuliaji wa timu ya Young Africans Mrisho Khlafani Ngassa leo
amelipa jumla ya mil 45, deni la mil 30 pamoja na faini ya mil 15 za
klabu ya Simba SC kwa Shirikisho la Soka nchini TFF ili aweze kuitumikia
timu yake kuanzia kesho.
Ngassa ambaye aliambatana na viongozi wa klabu ya Yanga mjumbe wa
sekretariat Partick Naggi, Afisa Habari Baraka Kizuguto na mhasibu Rose
Msamila alikabidhi hundi za malipo kwa idara ya fedha ya shirikisho
hilo.
Mara baada ya kukabidhi hundi hiyo Ngassa aliongea na
waandishi wa habari nje ya ofisi za TFF na kusema ameamua kulilipa deni
hilo ili aweze kuitumikia klabu yake, kwani kukosa michezo sita
kumemnyima fursa ya kuisaidia timu yake.
Naomba mnielewe hizi
fedha nimezitoa mimi mwenyewe kwenye akiba yangu iliyopo bank, hivyo
kama kuna mtu yoyote ataguswa na hili suala anaweza kuwasiliana na mimi
katika kujaribu kunichangia juu ya hili.
Aidha Ngasaa amesema kwa
sasa akili yake yote ipo kwenye michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom na lengo
lake ni kuhakikisha anaisadia timu yake kufanya vizuri n akupata ushindi
katika kila mchezo watakaocheza.
Kocha Ernie Brandts kwa sasa ana
fursa ya kumtumia mchezaji Mrisho Ngasa kwa kuanzia kwa mchezo wa kesho
kutokana na kuwa amekamilisha kila kitu.
Naye Afisa Habari wa
Yanga Baraka Kizuguto amewaomba wapenzi, washabiki na wanachama
kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Taifa kuja kuishangilia timu yao
itakapokua ikicheza na maafande wa Ruvu Shooting.
Young Africans itacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.
CHANZO NI BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment