KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom imesema kukosekana kwa huduma
ya M-Pesa kwa saa takribani nane nzima Septemba 21 mwaka huu,
kunatokana na kuzidi kwa muda uliokuwa umetengwa kwa ajili ya maboresho
ya kawaida katika mfumo wa huduma hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Rene Meza, alisema jana kuwa
kazi ya uboreshwaji wa mfumo wa huduma hiyo ilipangwa kufanyika kwa saa
sita, lakini matatizo mengine ya kiufundi yalisababisha kufanyika
zaidi ya muda uliopangwa.
“Tunapenda kuwaomba radhi wapendwa wateja wetu, washirika wetu na
benki zote pamoja na wananchi wote kwa ujumla kwa kutoweza kutumia
huduma yetu ya M-Pesa kutokana na kazi ya kuboreshwa kwa mtandao wa
huduma hiyo.
“Kazi ya uboreshaji wa mtandao huo ilikwenda vizuri, lakini
mabadiliko hayo yalisababisha kutokea kwa matatizo kadhaa ya kiufundi
ambayo yalidumu kwa saa nane, hali iliyotulazimu kusitisha baadhi ya
huduma za mtandao wa M-Pesa,” alisema Meza.
Aidha, alisema baada ya kugundua chanzo cha tatizo hilo, wataalamu wa
kampuni hiyo waliendelea kufanya marekebisho hayo kwa umakini na
kuweza kugundua chanzo cha tatizo na kurudisha huduma hiyo katika hali
yake ya kawaida.
No comments:
Post a Comment