Regina Salago enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kinyama, limetokea hivi karibuni katika Kijiji cha
Maganzo, Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga.Akizungumza na
gazeti hili kuhusu tukio hilo, mama mzazi wa Regina aliyejitambulisha
kwa jina la Catherine Kondo (45) alisema siku mbili kabla ya kifo, binti
yake huyo alikuwa amerudi nyumbani kutoka kwa mumewe kwa nia ya
kuachana naye.‘’Siku aliyorudi mwanangu aliniambia amechoshwa na vitendo vya wivu wa kupita kiasi anavyofanyiwa na mume wake, ameona bora arudi nyumbani aanze upya maisha akiwa huru hata kama ni ya shida,’’ alisema mama huyo.
Aliongeza kuwa Regina alishinda siku mbili tu nyumbani hapo ndipo mume wake alimfuata na kumbembeleza kuwa waondoe tofauti zao na kwamba alikuwa amejirekebisha.
“Regina alikataa katakata kurudi kwa mwanaume huyo kutokana na vitendo vya kikatili na unyanyasaji alivyokuwa akifanyiwa kiasi cha kukosekana kwa amani kwa kusingiziwa alikuwa akitembea nje ya ndoa yao,” alisema Catherine.
Kufuatia hali hiyo mwanaume aliamua kubadili msimamo na kumpa shilingi 40,000 Regina kama kumuomba msamaha akashawika kuondoka naye kurudi kwao.Habari zinadai walipofika kwao alimshambulia kwa kumpiga na springi ya gari na kuivunja mikono na shingo kwa kutumia chuma hicho kizito.
Baada ya kumuua, Kishimba alimpigia simu mama mkwe wake mara kadhaa akimhimiza aende nyumbani haraka kwa kuwa mtoto wake Monica (mdogo wa Regina) alikuwa mgonjwa mahututi.Aliporudi nyumbani alianza kumtafuta Regina na alipokwenda kwa mumewe alimkuta akiwa amelala kifudifudi na damu ikiwa imetapakaa mwili mzima, akiwa amekata roho.
Mama huyo aliongeza kuwa, kufuatia tukio hilo alipiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani na baadaye polisi waliitwa eneo la tukio.Mama huyo alisema kuwa muuaji alifanikiwa kutoroka na kuwaacha watoto wake wawili, Frank (5) na Minza (3) aliozaa na marehemu.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, SACP Justus Kumugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. “Sasa hivi tunamtafuta muuaji ili aweze kufikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Kamugisha.
No comments:
Post a Comment