Msanii kutoka Colombia Shakira mwenye miaka 
’37’ amebarikiwa kupata mtoto wa pili na mpenzi wake ambaye ni mwanasoka
 wa Barcelona ‘Gerard Pique’. Mtoto wao wa pili amepewa jina ‘Sasha’ . 
Sasha maana yake ni Alexander kwa tafsiri ya lugha ya Kirusi.
Shakira na Gerard walilipia floor nzima ya hospitali ya Quiron 
Teknono mjini Barcelona kwaajili ya kujifungua kwa Shakira na kukimbia 
mapaparazzi. Daktari aliyemzalisha Shakira mara ya kwanza ndio 
amemzalisha tema mara ya pili. 
 
Mtoto wao wa kwanza anaitwa Milan ana miaka miwili sasa.
 
 
 
 
 
 
 

 
No comments:
Post a Comment