Stori: Musa Mateja/Risasi
HATIMAYE ukweli wa kutekwa, kuteswa kwa kudhalilishwa kwa aliyekuwa mume wa mwimba taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’, umejulikana, Risasi Jumamosi limechimba.
Mfanyabiashara, Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa amefungwa kamba na watesi wake.
Januari 28, mwaka huu, picha za Tevez akiwa ametoka kuteswa kwa
kudhalilishwa zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku
wengine wakidai kisa ni kukutwa na mke wa mtu, wengine wakisema ni
dhuluma.RISASI LAINGIA MTAANI KUCHIMBA
Risasi Jumamosi halikufanya haraka kuichapisha habari hiyo mpaka kuichimba kwanza ili kujua kisa na mkasa kamili ndipo iwapelekee wasomaji wake. Na ndivyo ilivyofanyika!
ENEO LA TUKIO
Risasi Jumamosi lilichimba na kubaini kuwa, tukio la Tevez kufanyiwa ukatili huo lilitokea kwenye mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kibiashara.
“Tukio si la Dar kama wanavyosema wengine, limetokea mjini Durban, Afrika Kusini. Si unajua jamaa (Tevez) ni mtu wa tripu za kibiashara!” alisema mtoa habari mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Jeraha likiwa mgongoni mwa Jumanne Hassan ‘Tevez’ baada ya kuteswa.
WALIOFANYA UKATILIKwa mujibu wa chanzo hicho, watu waliomtenda Tevez ni jamaa zake anaofanya nao biashara ambayo Risasi Jumamosi halijaijua vizuri (ingawa kwenye mitandao ya kijamii wanadai ni madawa ya kulevya).
YATAJWA DHULUMA
Chanzo kikaanza kuanika historia nzima tangu Tevez hajafanyiwa utekaji na udhalilishwaji huo.
“Siku za nyuma Tevez alipewa mzigo nchini Tanzania ili awapelekee hao jamaa wa Afrika Kusini. Aliondoka jijini Dar kwenda Nairobi, Kenya kwa basi akiwa na begi.
“Alipofika Nairobi, ilidaiwa begi hilo alilisahau kwenye basi lakini wengine wanasema aliuuza Nairobi na kwenda Afrika Kusini akiwa na begi feki.”
TEVEZ AWASILI AFRIKA KUSINI, AKUMBANA NA MSALA
Habari zaidi zikachimbuka na kudai kwamba, Tevez aliwasili mjini Durban na kukutana na jamaa zake ambapo aliwaambia mzigo aliusahau kwenye basi.
“Kumbe inasemekana jamaa aliyemuuzia mzigo Nairobi anafahamiana na jamaa wa Sauz na aliwapigia simu kuwaambia kwamba, ameuziwa mzigo na Tevez.
“Kwa hiyo mpaka Tevez anawasili kule, jamaa walikuwa wanajua hana mzigo kwa kuwa aliuuza Nairobi,” kilisema chanzo.
‘Tevez’ akiwa na moja ya wadau wenzake katika biashara anazofanya huko Durban.
ATEKWA, ADHALILISHWAIkaendelea kudaiwa kuwa, madai ya Tevez yaliwakera jamaa kwa vile walijua kila kitu, hivyo walimteka na kuanza kumtesa kwa kumvua nguo zote, wakamfunga kamba za manila za rangi ya bluu na kuanza kumtesa kwa adhabu mbalimbali ili kumkomesha.
Inadaiwa katika adhabu hiyo, jamaa hao walimpiga na kitu chenye ncha kali hali iliyosababisha Tevez atokwe na damu na ngozi kuchubuka eneo la mgongoni.
MADAI WAKATI WA UDHALILISHWAJI
Inadaiwa wakati udhalilishaji huo ukiendelea, jamaa hao walikuwa wakisema wanachotaka ni mzigo wao na si kitu kingine.
MARAFIKI, JAMAA WA DAR
Kufuatia kusambaa kwa picha hizo mtandaoni, marafiki na jamaa wa Tevez waliopo Bongo walilazimika kufanya mpango kwa kuwasiliana na watu wa karibu waliopo Durban kumnusuru Tevez kwa kumpeleka hospitali ambako anapata matibabu hadi juzi, Alhamisi.
Risasi Jumamosi: “Kuna habari alikatwa sehemu za siri ni kweli?”
Chanzo: “Si kweli.”
Risasi Jumamosi: “Inasemekana alifanyiwa kitu mbaya cha mambo ya Sodama, ni kweli?”
“Si kweli. Watu wanasema tu. Ila walimtesa sana kwa kweli.”
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa na moja ya jamaa zake sauzi.
RISASI LATINGA DUKANI KWA MKEWE WA SASAIli kuzidi kupata habari zaidi, Januari 28, mwaka huu, usiku Risasi Jumamosi lilikwenda Kinondoni Kwamanyanya, Dar kwenye duka la mke wa sasa wa Tevez ili kumsikia anasema nini kuhusu tukio hilo.
Paparazi wetu hakumkuta mke huyo lakini alibahatika kuongea na msichana aliyekuwa nje ya duka hilo na kumuuliza aliko Tevez.
Msichana: “Tevez yupo safarini Morogoro.”
Risasi Jumamosi: “Mbona hapatikani hewani? Nipe namba zake nyingine.”
Msichana: “Nilizonazo ndiyo hizohizo ulizonazo wewe, ni…(akazitaja).”
Kweli namba hizo ndiyo alizokuwa nazo paparazi wetu.
MAMA MKWE WA TEVEZ
Kesho yake, Risasi Jumamosi lilimsaka kwa simu mama mkwe wa zamani wa Tevez (mama wa Isha) lengo ni lilelile, kutaka kujua kama naye ana taarifa hizo na anasemaje.
“Ni kweli nimesikia na nimeona picha zake yaani nimesikitika sana kiasi kwamba nikawa siamini kama ni kweli yeye anaweza kufanyiwa ukatili wa aina hiyo.
“Kikubwa namshukuru Mungu kusikia yupo hai na kwa maana hiyo namuombea zaidi ili arudi katika afya yake,” alisema mama mkwe huyo aitwaye Rukia Juma.
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’akiwa na mkewe.
MTU WA KARIBU NA TEVEZRisasi Jumamosi liliendelea kutafuta undani zaidi wa tukio la Tevez kwa kuongea na watu wake wa karibu waliopo Durban, ndipo likapenyezewa ishu mpya kuwa, baadhi ya ndugu na wafanyabiashara wenzake na Tevez wamechanga na kurudisha mali zilizokuwa zikidaiwa na jamaa hao.
“Nilikuwa Durban muda si mrefu na hapa ndiyo narejea nyumbani (Bongo). Kiukweli tukio la Tevez ndiyo habari ya mjini Sauz, maana jamaa wamemfanyia mbaya kinoma lakini kusema kweli hajakatwa nyeti kama mitandao ya kijamii inavyoandika, wamempiga sana.”
“Kingine ambacho ninajua tayari ameshatolewa kwenye jengo alilokuwa ametekewa na sasa yupo hospitali maalum ambayo siwezi kukutajia, ila huenda hali yake ikawa nzuri kama kweli atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari,” alisema jamaa huyo.
No comments:
Post a Comment