Monday, August 31, 2015
UKAWA YAMTANGAZA RASMI JULIUS MTATIRO KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA
SITTA AMJIBU SUMAYE KUHUSU MABEHEWA MABOVU
WATUMIAJI WA MITANDAO VIBAYA SHERIA KUWADHIBITI KUANZA LEO SAA 6:00 USIKU
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam leo.
DK AZIDI KUWACHANGANYA WAPINZANI KAMPENI ZA URAIS NJOMBE
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula akihutubia kwa kumnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli katika mkutano wa hadhara wa kampeni kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimtambulisha Naibu Waziri wa Ujenzi, ambaye anagombea ubunge Jimbo la Njombe Kaskazini, Gerson Lwenge katika mkutano wa hadhara wa kampeni wilayani Wanging'ombe, mkoani Njombe
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shilole akitumbuiza leo kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Dk Magufuli akitoa shukrani kwa viongozi wa CCM Mkoa wa Mbeya baada ya kumaliza ziara mkoani humo na kuanza kampeni katika Mkoa wa Njombe
Dk.Magufuli akijinadi kwa wananchi na kutoa ahadi katika nKijiji cha Igoma, Mbeya Vijijini aliposimama kwa muda akielekea Makete mkoani Njombe kuendelea na kampeni. Akichaguliwa ameahidi kujenga barabara ya lami ya Njombe hadi Mbeya kuptia Makete na kijijini hapo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Wananchi wakishangilia baada ya kuelezwa na Dk Magufuli kuhusu ijenzi wa barabara ya lami itakayopita kijijini hapo
Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli kijijini hapo
Dk Magufuli akijinadi katika Kijiji cha Ilungu Mbeya Vijijini mpakani na Mkoa wa Njombe
Wananchi wakishangilia huku wakiwa na vipeperushi vyenye picha za Dk Magufuli
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Makete, Binilith Mahenge akimpigia debe Dk Magufuli pamoja na Mgombea ubunge wa Jimbo la Makete, Norman Sigalla.
Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano uliofanyika Iwawa wilayani Makete
Dk Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Makete, Dk Norman Sigalla katika mkutano wa kampeni uliofanyika Iwawa Makete
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu nchini, Amon Mpanju akimpigia debe Dk Magufuli eneo la Iwawa wilayani Makete
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Dk Magufuli mjini Makete
Dk Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzania waliovihama vyama vyao na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Iwawa, Makete leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mmoja wa wafuasi wa Chadema akiwa amesamama karibu na pikipiki yenye bendera ya chama hicho huku akimsikiliza kwa makini Dk Magufuli akijinadi katika Kijiji cha Kenja, wilayani Makete leo.
Mfuasi wa Chadema (kulia) akishangilia baada ya kumsikia Dk Magufuli akitangaza kwamba akichaguliwa kuwa urais watoto watakuwa nasoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Kutano huo ulifanyika katika Kijiji cha Kenja wilayani Makete baada ya msafara kuzuiwa wananchi katika eneo hilo wakiwa na hamu ya kusikiliza sera zake.
Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Kenja wakimsikiliza Dk Magufuli huku wakiwa na mabango yenye picha za mgombea huyo wa urais wa CCM
Dk Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kenja wilayani Makete
Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, William Lukuvi akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula katika mkutano wa kampeni wilayani Wangi ng'ombe, Mkoa wa Njombe leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana akihutubia katika kutano wa kampeni wa kumnadi Dk Magufuli wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe leo
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula akisalimiana na Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli katika mkutano wa hadhara wa kampeni wilayani Wanging'ombe, mkoani Njombe
Wananchi wa Kijiji cha Igagala wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali walipokuwa wakimlaki Dk Magufuli, wilayani Wanging'ombe, Njombe
Dk Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Igagala, wilayani Wanging'ombe
Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Njombe
Msanii Cgegge akitumbuiza katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe leo
Saturday, August 29, 2015
Mkopo noma! Mfanyabiashara atupiwa vitu nje, Nyumba yauzwa!
Friday, August 28, 2015
LIONEL MESSI MCHEZAJI ULAYA
Mchezaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Lionel Messi.
MONACO, Ufaransa LIONEL Messi ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumpiku Cristiano Ronaldo katika tuzo zilizotolewa jana ambazo pia dunia ilishuhudia Manchester United ikirejea kwenye michuano hiyo hatua ya makundi. Messi, staa wa Barcelona, aliingia hatua ya fainali ya tuzo hizo pamoja na straika wa timu yake, Luis Suarez pamoja na Ronaldo wa Real Madrid, ambapo waandishi wa habari wa michezo ndiyo waliompigia kura.
Upande wa Man United ambao ni mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2008, wamepangwa katika kundi ambalo linaonekana kuwa jepesi kwao ambapo wapo Kundi B wakiwa pamoja na PSV Eindhoven ya Uholanzi, CSKA Moscow (Urusi) na Wolfsburg (Ujerumani).
Lionel Messi (kushoto)akipokea tuzo ya mchezaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka kwa Michel Platini (kulia) na Cristiano Ronaldo akiwa kwa nyuma.
Vijana wa Kocha Arsene Wenger, Arsenal, wamepangwa Kundi F wakiwa pamoja na vigogo wenzao, Bayern Munich ya Ujerumani pamoja na Olympiacos (Ugiriki) na Dinamo Zagreb (Croatia). Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho atakutana na timu yake ya zamani ya FC Porto katika Kundi G, ambapo wapo pamoja na timu za Dynamo Kyiv na Maccabi Tel Aviv. Ratiba kamili na jinsi makundi yalivyopangwa soma ukurasa wa 24.
Thursday, August 27, 2015
MSHINDI WA TMT 2015 MPAKAKIELEWEKE APOKELEWA KWA NDEREMO MJINI MOSHI
Lulu amhenyesha Mboto ukumbini
Waandishi 2 wauawa wakiwa hewani Marekani
Siri 4 matusi ya Diamond kwa Diva
Siku hiyo majira ya saa 9:00 alasiri, Diamond alitia timu kwenye studio za redio hiyo zilizopo Mikocheni, Dar kwa lengo la kumtambulisha msanii wake mpya kutoka studio yake ya Wasafi Records iliyopo Sinza-Mapambano, Dar.Mwanyeji wa Diamond alikuwa mtangazaji Hamis Mandi ‘B12’. Lakini ndani ya studio hiyo alikuwepo Diva.
Kabla Diamond hajaanza kumtambulisha msanii wake, alianza na Diva kwa kumsema kwamba amekuwa akimchoresha mitandaoni kwa kumchafua.
Diva alijibu kuwa, kisa cha yeye kumchoresha, aliwahi kumuita Diamond kwenye Kipindi cha Ala za Roho lakini staa huyo hakutokea wakati meneja wake, Salam alimpa taarifa, akakubali na yeye Diva akaanza kutangaza mitandaoni kuwa, siku moja atakuwa na Diamond hewani jambo lilimfanya wasikilizaji wake kusema aliwaongopea na wengine kuanza kumtusi mitandaoni.
Baada ya maneno hayo ya Diva, ndipo Diamond apoonesha dalili ya kukasirika na kutoa lugha ya matusi ambayo haiandikiki gazetini lakini akimaanisha kuwa, kama Diva angewahi kuwa mpenzi wake, angemheshimu.
Diva naye alijimjia juu Diamond kwa kumwambia kuwa, hana hadhi ya yeye kuwa mpenzi wake, maneno ambayo yalimchefua baba Tiffah na kuanza kutupiana maneno bila utaratibu hali iliyomlazimisha B12 kuingiza matangazo ili kuwatoa hewani wawili hao.
Kwanza inadaiwa kuwa, meseji za Diva kwenye mitandao kumsema Diamond kwa kitendo chake cha kutotokea kwenye Kipindi cha Ala za Roho zilimfanya mzazi mwezake, Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumbana baba wa mtoto wake huyo akimtaka aseme ukweli kama kuna siri iliyofichika kati yao
“Kitendo cha Diva kutumia mitandao kumshambulia, Diamond alikiweka moyoni na kuahidi siku wakikutana laivu atampasulia ya moyoni mwake liwalo na liwe. Hata alipokwenda studio jana (Jumatatu), hakujua kama angekutana na Diva.”
“Diamond aliamini kuwa, Diva kumshambulia mitandaoni alilenga kumshushia heshima mbele ya jamii ili kumuua kisanii. Maana yeye mwenyewe alisema anaamini maneno ya Diva kwenye mitandao kuna zaidi ya kitendo chake cha kutotokea studio,” kilidai chanzo chetu.
Kwa upande wake, Diamond alipozungumza na Amani alianika siri ya nne akisema:
“Yule Diva dizaini f’lani kama ananitaka vile lakini mimi simpi nafasi ndiyo maana anatengeneza bifu na mimi.”
“Diva amekuwa akinisema mara kwa mara. Mimi nilikwenda pale kwa lengo lingine, yeye akaanza kuleta zake za kuleta. Kila nikiitafuta sababu siioni. Sijawahi kumkosea popote pale.”
Amani lilimtafuta Diva juzi kwa lengo la kumsikia anasemaje kuhusiana na sakata hilo ambapo alisema:
“Hii ishu iko kwa wanasheria wangu (tayari kwa kumpeleka Diamond mahakamani). Amenidhalilisha sana kama mwanamke nisiyefaa katika jamii. Ushahidi upo kila kona kwenye mitandao.”
“Akaenda mbali zaidi na kutaka kunipiga maana lugha ya matusi haikutosha. Amenitishia maisha jambo ambalo halitakiwi kisheria. Hakuna aliye juu ya sheria. Sitazungumza zaidi.”