EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, August 31, 2013

YAHAYA YA LADY JAY DEE YAMJAZA MAHELA LULU WAKATI WA UZINDUZI WA MY FOOLISH AGE.

UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE.

Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.

Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.

“Jamanieee kumbe mziki unalipa ile mbaya yaani  nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona hela kibao, kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba mziki”, alisikika Lulu akisenma huku akishangiliwa na mashabiki wake.

Uzinduzi wa fikamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe  kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City
 Lulu akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
 Wadau walifuatilia burudani...
 Jide akikamua jukwaani...

CHOMBEZO: KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA....SEHEMU YA 06.

Na Irene Mwamfupe Ndauka.
ILIPOISHIA...
 “Haa! Mume wangu huyo anapiga…
“Haloo…”
“Uko wapi wewe..?”
“Nani mimi..?”
“Unaniuiliza swali gani hilo..?”
“Niko nyumbani…”
“Na nani..?”
“Nani mimi..?”

“Mama Joy…”
“Abee…”
Baba Joy alikata simu. Alianza kuhisi kitu
kikubwa zaidi. Akampigia mfanyakazi wa ndani…
“Za safari bosi..?”
“Njema, upo nyumbani..?”
“Ndiyo bosi…”
“Mama je..?”
“Yupo bosi…”
“Yupo na nani..?”
 
“Nani mama..?”
“Hivi nyiye hapo nyumbani pana nini leo..?”
“Kwa nini bosi..?”
“Mbona hammalizi kujibu badala yake mnauliza
maswali… nimekuuliza mama je, yupo hapo nyumbani? Badala ya kunijibu unaniuliza
na wewe ‘nani mama?’” alifoka baba Joy…
“Samahani sana bosi, mama yupo na mgeni
wake…”
 
“Mgeni gani…?”
“Kijana mmoja hivi…”
“Huyo kijana we unamjua..?”
“Namjua bosi, anakujaga kuzoa taka...”
“Kumbe ni yule mzoa taka siyo?” aliuliza
baba Joy huku akisimama kwenda kuongelea pembeni maana aliona pale siri zake
zitakuwa nje…
“Ndiyo bosi…”
“Wako wapi muda huu..?”
“Naona wapo…ooooo, wapo sebuleni bosi…”

BAILEYS YADHAMINI ONESHO LA MAVAZI LA NECHA LA MBUNIFU DANIELA RAYMOND

 Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake cha Baileys imedhamini onesho la Mavazi lijulikanalo kama NECHA la mbunifu wa mavazi Daniela Raymond. Onyesho hilo lilifanyika ktik kituo cha Utamaduni wa watu wa Kamara.

Serikali yasalimu amri kwa wabunge

Dodoma. 
Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa mwaka 2013, jana ulipita kwa mbinde bungeni mjini Dodoma, huku Serikali ikisalimu amri kwa wabunge na kukubali kurekebisha baadhi ya vifungu vyake.
 
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Mohamed Keissy akichangia bungeni mjadala wa kupitisha muswada wa sheria ya taifa ya umwagiliaji wa mwaka 2013, ambapo alikuwa akipinga wawekezaji wa kilimo kwenda kuwekeza mkoani Rukwa, 

Bila kujali tofauti zao za kisiasa, wabunge jana walisimama kidete na kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, wakitaka sheria hiyo imlinde mzawa badala ya mwekezaji.
Moto huo wa wabunge uliwalazimisha Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chizza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema kusalimu amri na kukubali mapendekezo ya wabunge.

 Msimamo wa wabunge hao katika kuibana Serikali, pia ulililazimisha Bunge kutengua kanuni zake na kuendelea na shughuli za kupitia muswada huo hadi saa 7:35 mchana, badala ya kusitishwa saa 7:00 kwa ratiba ya kawaida.

LULU MICHAEL ALIVYO TOKELEZEA KATIKA UZINDUZI WA MUVI YAKE YA FOOLISH AGE - MLIMANI CITY.

1

Elizabeth Michael (Lulu) akiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam tayari kwa uzinduzi wa filamu yake inayokwenda kwa jina la Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion chini ya Mwenyekiti wake Jonson
Lukaza ambaye ameweza kujitolea kwa hali na mali mpaka kufanikisha utengenezaji wa filamu hii na uzinduzi kwa ujumla, Uzinduzi huo unafanyika usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki Lady Jay Dee aka Komando aka Anaconda akituzwa wakati akitoa burudani safi sana katika Uzinduzi wa Lulu ndani  ya Ukumbi wa Mlimani city.
8Elizaberth Michael (Lulu) akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa filamu ya Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion chini ya Mwenyekiti  wake Jonson Lukaza ambaye ameweza kujitolea kwa hali na mali mpaka kufanikisha utengenezaji wa filamu hii na uzinduzi kwa ujumla, Uzinduzi huo unafanyika usiku wa kuamkia leo.1aLulu akilakiwa kwa mbwembwe na vijana walioandaliwa kwa kazi hiyo. 2.Mwenyekiti wa kampuni ya Proin Promotion Bw. Jonson Lukaza katikati akizungumza na baadhi ya waigizaji wa filamu Rich Rich na mwenzake

CHEKA NOMA, AMCHAKAZA MMAREKANI KWA POINTI.

BONDIA Francis Cheka ameendeleza umwamba wake baada ya kumgonga Mmarekani Phil Williams kwa pointi. Cheka ameshinda pambano hilo la WBF lililokuwa la raundi 12 ambalo limepigwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Bondia Francis Cheka akiwa ulingoni na Mmarekani Phil Williams (kulia).
Francis Cheka (kushoto) akimtupia konde mpinzani wake kutoka nchini Marekani, Phil Williams. Cheka ameshinda kwa pointi.

CHELSEA YAPIGWA NA BAYERN KWA 5-4 SUPER CUP

BAYERN Munich imetwaa Super Cup ya Ulaya baada ya kuifuna Chelsea kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 na Jose Mourinho ameshindwa kutwaa taji la kwanza baada ya kurejea darajani mbele ya Pep Guardiola.
Katika mchezo huo, ambao Chelsea ilimaliza pungufu baada ya Ramires kutolewa nje kwa nyekundu dakika ya 84, mabao ya The Blues yalifungwa na Torres dakika ya nane na 
Hazard dakika ya 93, wakati ya Bayern yalifungwa na Ribery dakika ya 47 na Javi Martinez dakika ya 120.
Katika mikwaju ya penalti, Ashley Cole alifunga Cech akaokoa penalti Xherdan Shaqiri. 
Penalti nyingine zilizofungwa na David Luiz, Oscar na Frank Lampard kwa upande wa Chelsea, wakati za Bayern zilifungwa na Jerome Boateng, Toni Kroos, Philipp Lahm na Franck Ribery hivyo kuteneneza ushindi wa 5-4
Kikosi cha Bayern Munich kilikuwa: Neuer, Rafinha/Javi Martinez dk56, Dante, Boateng, Alaba, Muller/Gotze dk70, Lahm, Kroos, Ribery, Mandzukic na Robben/Shaqiri dk95.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Hazard, Oscar, Schurrle, Torres/Lukaku dk97.
Loss: Lukaku looks on after his decisive penalty miss in Prague
Loss: Lukaku looks on after his decisive penalty miss in Prague
Champions again: Bayern celebrate the win after Neuer's penalty save
Champions again: Bayern celebrate the win after Neuer's penalty saveLevel: Javi Martinez (right) scores for Bayern in the last minute of extra time
Level: Javi Martinez (right) scores for Bayern in the last minute of extra time

DAVID MWANTIKA ACHUKUA NAFASI YA KELVIN YONDANI TAIFA STARS.


DAVID MWANTIKA ACHUKUA NAFASI YA KELVIN YONDANI TAIFA STARS

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Mwantika ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye ni majeruhi. Wachezaji ambao ni majeruhi na Kim amewaondoa kwenye kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao ni Athuman Idd, Shomari Kapombe na John Bocco.
Taifa Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi siku jana  jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.

PENNY: YATASEMWA MENGI DIAMOND SIMUACHI



Baada ya hivi karibuni kuandikwa habari iliyoeleza kwamba nchini Kenya kuna demu aliyemzimikia ile mbaya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akiahidi kumpa penzi zito, mpenzi wa msanii huyo Peniel Mwingilwa ‘Penny’ ameibuka na kudai hatishwi na maneno hayo.

KUMBE ALIYEMPIGA CHUPA AUNT NDIYE ALIYEMCHANA LULU VIWEMBE.

Mrembo Yvonne aliyempasua kwa chupa Aunt Ezekiel usiku wa kuamkia Jumatatu Agosti 26, 2013 na kumcharanga Lulu kwa viwembe usoni Jumatatu ya Mei 2, 2011 saa 4: 48 usiku.
IMEVUJA! Mtuhumiwa aliyempiga chupa mwigizaji Aunt Ezekiel Jumapili iliyopita nje ya Ukumbi wa Bilicanas ndiye aliyewahi kumchana viwembe mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwaka 2011.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Data za Ijumaa zinaonesha kuwa, mwaka 2011 Lulu alivamiwa na wadada wa mjini baada ya kunaswa katika pozi tata na mwanaume wa watu maeneo ya Kariakoo, jijini Dar. Alipoulizwa juu ya sakata hilo, Lulu alitiririka hivi:
 

“Naweza kumkumbuka mwanamke mmoja, namfahamu kwa jina la Yvonne, alinivamia na kuanza kunishambulia huku mkononi akiwa ameshika wembe...”

MTITU ASHINDA VITA YA USAMBAZAJI.

BAADA ya kuwekewa vizingiti katika kazi yake ya usambazaji wa filamu, Mkurugenzi wa Kampuni ya 5 Effect, William Mtitu amesema anamshukuru Mungu kwani ameishinda vita hiyo.
Kabla ya kufanikiwa kusambaza filamu yake ya Omega iliyotoka Jumatatu iliyopita, inadaiwa kwamba kampuni moja maarufu ya usambazaji wa filamu jijini Dar ilimwekea vizingiti kwa kutoa filamu kila siku ambazo Mtitu alitangaza kuitoa kwa mara ya kwanza filamu hiyo.
 
“Najivunia kwamba nimeshinda vita maana jamaa walikuwa wakinifanyia mchezo mchafu. Kila nilipotangaza kutoa filamu na wao wakawa wanaingiza filamu mpya lakini nashukuru Mungu kwamba sasa hivi nimeweza.
 
“Huwezi kuamini, nilipoingiza sokoni Omega ndani ya masaa matano nililazimika kuongeza nakala nyingine kwani inanunuliwa kama karanga,” alisema Mtitu

Friday, August 30, 2013

Orodha kamili ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2013/1014.

Group A: Manchester United, Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen, Real Sociedad
 
Group B: Real Madrid, Juventus, Galatasaray, FC Copenhagen
 
Group C: Benfica, Paris St-Germain, Olympiakos, Anderlecht
 
Group D: Bayern Munich, CSKA Moscow, Manchester City, Viktoria Plzen
 
Group E: Chelsea, Schalke, FC Basel, Steaua Bucharest
 
Group F: Arsenal, Marseille, Borussia Dortmund, Napoli
 
Group G: Porto, Atletico Madrid, Zenit St Petersburg, Austria Vienna
Group H: Barcelona, AC Milan, Ajax, Celtic

Tukio zima la uzinduzi wa video ya Diamond - Number 1

HILI NDO GARI DIAMOND ALILO MZAWADIA MZEE GURUMO USIKU WA JANA

Msanii Diamond Platnum amefanya kufuru usiku wa jana kwa kutoa zawadi ya Gari kwa Mzee Ngurumo Mwanamziki wa miaka mingi na mkongwe nchini aliyestaafu majuzi kufanya kazi za mziiki.
Tukio hilo limetokea usiku wa jana ndani ya ukumbi wa SERNA HOTELkatikati ja jiji la DSM ambapo Diamond Platnum amezindua video yake ya wimbo wa #one fun.
Kiingilio cha show hiyo ni bureeeeeeeeeeeee....LAKINI UMEALIKWA?

Mzee Ngurumo amesema"Haamini macho na masikio yake,hanachakusema zaidi ya ASANTE kwa msanii huyo"Lakini pia amesema hajui hata mke wake atasemaje baada ya kumwona akiingia na gari ndani ya nyumba yake.
Mzee ngurumo amekuwa na matatizo ya kiafya siku za karibuni nakupelea kustaafu mziki kabisa.Wazee wa msondongoma ndio wanajua makali ya Mzee Ngurum

Majambazi yapora Sh900 milioni benki asubuhi.

Dar es Salaam.
 Watu wanane wanaodhaniwa kuwa majambazi, jana walipora zaidi ya Sh900 milioni katika Tawi la Benki ya Habib, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Wizi huo ulitokea saa tatu asubuhi kwenye benki hiyo iliyoko makutano ya Mitaa ya Livingstone na Uhuru.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alisema fedha zilizoibwa ni Sh700 milioni na Dola za Marekani 181,885 (Sh285,444,000).
Kamanda Kova alisema wameanza kuwasaka majambazi hao waliohusika katika tukio hilo.

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Kova alisema majambazi hao walifika kwenye benki hiyo na kuingia ndani moja kwa moja na kujifanya ni wateja ambao walikuwa wamesindikizwa na mtu mmoja aliyekuwa amevaa sare za polisi.

Baada ya kuingia ndani, alisema waliwaweka chini ya ulinzi wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na wateja wanne waliokuwepo ndani wakipata huduma.

Askofu Kulola afariki dunia wa EAGT.

Dar es Salaam. 
Vilio, simanzi na maombi ya kunena kwa lugha vilitawala jana katika Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Temeke Dar es Salaam wakati waumini na ndugu wa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk Moses Kulola (83) walipopata taarifa za kifo cha kiongozi huyo.
 
Katibu Mkuu wa EAGT, Brown Mwakipesile alisema kuwa Askofu Kulola alifariki dunia jana saa tano asubuhi kwenye Hospitali ya Africa Medical Invesment (AMI), Dar es Salaam.

Mwakipesile alisema afya ya Askofu Kulola ilianza kubadilika Mei mwaka huu akiwa mkoani Mwanza ambako alipelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando ambako alibainika kuwa na matatizo ya moyo.

 “Kanisa liliamua kuchukua jukumu la kumpeleka Hospitali ya Apollo, India kwa matibabu zaidi na baada ya kuona afya yake inatengemaa aliruhusiwa kurejea nchini, lakini Agosti 16, mwaka huu hali ilibadilika ndipo tukampeleka AMI alikofikwa na mauti,” alisema Mwakipesile.

Alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa ambalo haliwezi kuzibwa kwa sasa. Hata hivyo, wanafarijika kwa upande mwingine wakiamini kwamba Mungu amemchukua mtumishi wake kwa wakati alioukusudia.

IGP asafisha vigogo Uwanja wa Ndege.

Dar es Salaam. 
Siku chache baada ya kuibuliwa kwa kashfa ya kupitishwa kiholela kwa dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Jeshi la Polisi limemwondoa Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Kamishna Msaidizi (ACP), Deusdedit Kato pamoja na Mkuu wake wa Upelelezi, David Mwafwimbo.
Mbali ya maofisa hao, pia jeshi hilo limemwondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, 
 
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa, naye ikiwa ni miezi michache baada ya kutokea kwa ghasia wakati baadhi ya wakazi wa huko walipokuwa wakipinga mpango wa Serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.

Nafasi ya Kamanda Sinzumwa imechukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Zelothe Stephen kutoka Makao Makuu ya Polisi.

Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema amemteua, ACP Selemani Hamisi kuchukua nafasi ya Kato ambaye anahamishiwa makao makuu ya jeshi hilo. Kabla ya uteuzi huo, Kamanda Hamisi alikuwa Makao Makuu Idara ya Upelelezi.

IGP Mwema pia amemteua Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad kuchukua nafasi ya Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).

Thursday, August 29, 2013

ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA


 
Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake.
Askofu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T na mhubiri wa kimataifa wa siku nyingi, Moses Kulola amefariki dunia. Askofu Moses Kulola amefariki leo.

Mtoto wa Askofu Kulola, ambaye naye pia ni mhubiri wa kimataifa na mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala mpya,  Mch. Daniel Moses Kulola amethibitisha taarifa hizo kupitia katika akaunti yake ya Facebook. Kwa kuandika hivi: "WATU WA MUNGU SALAAM, NINA SALAAM ZA MAJONZI. BABA YANGU MZEE KULOLA AMEFARIKI MUDA SIYO MREFU."

Hivi karibuni  marehemu alilipotiwa kulazwa katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza kwa matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yanamkabili lakini Agosti 22 mwaka huu mwanaye Mch. Daniel Moses Kulola alieleza kuwa baba yake karuhusiwa  baada ya kupata nafuu.
MUNGU AILAZE ROHO YA ASKOFU KULOLA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN

MAJAMBAZI WAPORA MAMILIONI BENKI YA HABIB AFRICAN KARIAKOO.

 
-Walikuwa wamevaa sare za Jeshi la Polisi
-Jeshi la Polisi lathibitisha kutokea tukio hilo
WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliokuwa wamevalia sare za Jeshi la Polisi wamevamia Habib African Bank ililyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam na kupora mamilioni ya fedha. Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Chanzo: ITV

ALIYEMPASUA AUNT EZEKIEL KWA CHUPA HUYU HAPA.


Mrembo Yvonne aliyempasua kwa chupa Aunt Ezekiel usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas.
 
Mkono wa kushoto wa Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ uliopasuliwa na Yvonne kwa chupa.
Pichani juu ni mrembo aliyempasua mwigizaji wa sinema za Bongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ ajulikanaye kwa jina la Yvonne. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, ambapo Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto. Vurugu kubwa ilizuka baada ya tukio hilo na Aunt alikimbizwa hospitali ya Aga Khan huku Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa.

Arsenal yafuzu makundi Ulaya

London, England.
Aaron Ramsey alifunga mara mbili na kuiwezesha Arsenal kusonga mbele kirahisi hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Fenerbahce mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates usiku wa kuamkia jana.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kusonga mbele kwa ushindi wa mabao 5-0, kufuatia kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza.

Ramsey, aliyefunga bao moja kati ya matatu ambayo Gunners walishinda katika mchezo wa kwanza ili iliyopita nchini Uturuku, alifunga bao la kwanza dakika ya 25.
Pamoja na wageni kucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza, vijana wa Kocha Arsene 

Wenger walijihakikishia ushindi kwa Ramsey kufunga bao la pili dakika ya 72.
Nayo Vienna ilikata tiketi ya kucheza hatua za makundi kufuatia ushindi wa jumla mabao 4-3 Dinamo Zagreb.

Watu 13 wafariki ajalini Kahama.

Kahama.
Watu 13 wamepoteza maisha papohapo akiwamo mtoto mchanga wa miezi saba, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga lori la mizigo lililokuwa limeharibika barabarani katika Kijiji cha Ngongwa, wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
 
Ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 usiku wakati gari aina ya Toyota Hiace lilipoligonga lori.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kihenya Kihenya, alisema Hiace hiyo ilikuwa ikifanya safari zake kutoka mjini Kahama kwenda mji mdogo wa Ushirombo, katika Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.

Kihenya alisema watu 11 akiwamo dereva ambaye pia ni mmiliki wa gari hilo, Ezekiel Werema, walifariki dunia papohapo na wengine wawili walifariki dunia wakiwa katika 
Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa matibabu.

Alisema polisi wanahangaika kutafuta majina ya marehemu na majeruhi, ili ndugu na jamaa zao waweze kutaarifiwa.

Pia, Kihenya aliwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa ushirikiano walioonyeshwa kwa polisi baada ya ajali kutokea na kuongeza kuwa, hadi sasa baadhi ya watu tayari wamejitokeza Hospitali ya Wilaya ya Kahama kutambua maiti.

Kamanda Kihenya alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, huku akitoa wito kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari hasa nyakati za usiku.

YANGA ILIVYOVUTWA SHATI NA WAGOSI WA KAYA COASTAL UNION UWANJA WA TAIFA.


  
Hamad Juma akitafuta mbinui za kumtoka mchezaji wa Ynga, Mbuyu Twite huku Crispin Odula akiwa tayari kumsaidia.
                   Hapa Nadir Haroub akijaribu kumdhibiti 'toto tundu' Yayo Kato lakini alishindwa.

Abdi Banda kati kati ya wachezaji wa Yanga.

PICHA: CHELSEA YAMTAMBULISHA WILLIAN RASMI - APEWA JEZI NAMBA 22.

Amesaini mkataba wa miaka mitano
WillianWillian
All in blue: The Brazilian will wear the No 22 shirt

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate