EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, March 31, 2014

VIDEO: USIKU WA UTOAJI TUZO YA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 NDANI YA AFRICAN DREAMS, DODOMA

ROSE NDAUKA: SIWEZI KUZEEKA

STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema licha ya kujifungua, kamwe hawezi kuzeeka kama wengi wanavyomtafsiri.
Rose alisema, kwa upande wake hata siku moja hawezi kumuunga mkono mtu anayesema kuzaa au kulea kunamfanya mtu azeeke kwani inategemea na jinsi mtu anavyojiweka.

Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
“Nawashangaa hata wasanii wasiotaka kuzaa wakiona kama watakuwa wamemaliza ujana wao, asikwambie mtu hamna kitu kizuri kama kuitwa mama, nimejitunza na nimezidi kuwa mrembo hata baada ya kuzaa,” alisema Rose.

KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO MACHI 31, 2014


DIAMOND ATAMANI USHOGA!..BAADA YA KUTAJIRIKA, FEDHA ZAMCHANGANYA SASA

NYOTA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewashangaza watu kufuatia kuvaa wigi (nywele bandia) la mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni dalili ya kutamani mambo ya ushoga.
Diamond alinaswa akiwa amevaa wigi hilo kichwani kisha kupiga nalo picha.
ILIVYOKUWA
Hivi karibuni, Diamond alinaswa akiwa amevaa wigi hilo kichwani kisha kupiga nalo picha huku Wema akilitafuta ili alitinge bila mafanikio.
Habari zilieleza kuwa baada ya Wema kutoka nje akiendelea kulitafuta wigi hilo, alipigwa na butwaa kumkuta Diamond amelivaa, tena akionekana kuwa na amani.
Wema Isaac Sepetu na mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
WEMA AMWANIKA
“Jamani nimetafuta wigi langu muda mrefu sijaliona, nashangaa namkuta baby wangu (Diamond) amelivaa, lakini limempendezaje?” aliandika Wema kwenye ukurasa wake wa Instagram uliotembelewa na watu kibao.

MWANAMKE BORA WA MWAKA NI MAMA KAMM


Mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akihutubia kabla ya kukabidhi tuzo.
Stori: Mwandishi wetu, Dodoma
Pongezi! Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda juzi Jumamosi alikabidhi Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka (A Woman of the Year Award- 2013/14) mjini hapa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma.
Katika kinyang’anyiro hicho, Dk. Maria Kamm, ambaye kitaaluma ni mwalimu, aliibuka kidedea na kunyakua tuzo hiyo, medali pamoja na hundi ya shilingi milioni 5.
Wengine walionyakua tuzo hizo (bila medali) ni pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha Rose Migiro (aliwakilishwa na Anna Abdalah), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mbunge wa Same Mashariki, Mheshimiwa Anne Kilango Malecela.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.
Katika tukio hilo la kufana lililofanyika katika ukumbi wa kisasa wa The African Dream nyakati za usiku, watu mbalimbali maarufu walihudhuria wakiwemo wajumbe wengi wa Bunge Maalum la Katiba wanaoendelea na vikao vyao mjini hapa.

Sunday, March 30, 2014

WAZIRI MKUU PINDA AKABIDHI TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14, DK KAMM AIBUKA SHUJAA


Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo, Anna Margareth Abdallah, kwa niaba ya mshindi wa pili ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka aliyeibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo.
Mbunge wa Same Mashariki (CCM) Anne Kilango Malecela, akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kushika nafasi ya nne.
Dk. Maria Kamm akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kuibuka kinara wa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na washindi walioingia nne Bora. Kutoka kushoto; Anna Abdallah aliyechukuwa tuzo kwa niana ya Asha-Rose Migiro, Anne Kilango Malecela ,Dk. Maria Kamm na Profesa Anna Tibaijuka.
Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na washindi, waandaaji wa tuzo hizo kutoka Global Publishers Ltd.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL, DODOMA)

SIKILIZA WAWAKILISHI WA WANANCHI WAKIONGELEA KUHUSIANA NA SAKATA LA UJENZI WA MJI MPYA KIGAMBONI

Mchungaji Boniface Frank Mwenegoha akizungumza kuhusiana na sakata la ujenzi wa mji mpya Kigamboni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wananchi inayowakilisha malalamiko yao kuhusiana na ujenzi mpya wa mji wa Kigamboni,Bwa.Kassim Abdallah.

WANAFUNZI WA UDOM MWAKA WA MWISHO, WAAHIDI KUJIUNGA NA PPF

Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwenye semina iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambapo zaidi ya wanafunzi 500 walihudhuria semina hiyo Jumamosi Machi 29, 2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada kutoka kwa Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele.

TASWIRA MBALI MBALI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI ZA CCM KATA YA MANDERA




SIKILIZA WAWAKILISHI WA WANANCHI WAKIONGELEA KUHUSIANA NA SAKATA LA UJENZI WA MJI MPYA KIGAMBONI


Dk. Maria Kamm ametwaa tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 iliyotolewa na Global Publishers akiwashinda Dk. Migiro, Prof. Tibaijuka na Anne Kilango!

Saturday, March 29, 2014

KATIBA MPYA NA WANAWAKE!

"Ikipatikana Katiba yenye usawa wa kijinsia, tatizo la wanawake wanaojiuza litakwisha!" Hayo ni maneno ya mwanamke mpiganaji Bi Sophia Jonas alipozungumza na Super Woman Joyce Kiria kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na EATV kila Jumanne saa tatu kamili usiku.

WANANCHI WA MJI KOROGWE WAUPOKEA KWA KISHINDO MPANGO WA TIKA, WACHANGIA MIL. 1.3

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto). Pembeni ni Diwani wa Kata ya Mgombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) mbele ya mkuu wa mkoa wa Tanga.

Snura, Viuno Sitaki Tena Kwenye Video, Vimeniponza.

TRENI YA MIZIGO YAPATA AJALI ENEO LA GULWE WILAYA YA MPWAPWA

Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa kuamkia katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa. Katika ajali hiyo watu wawili wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.
Sehemu ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo imetokea saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba ngano, sukari na mafuta.

MUONEKANO WA SOKO LA KARIAKOO COCO BEACH



Friday, March 28, 2014

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA MAREHEMU TUPPA

Viongozi Dini wakiongoza ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,aliefariki ghafa siku kadhaa zilizopita.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,aliefariki ghafa siku kadhaa zilizopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Tambwe atangaza kuondoka Simba

Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe.
STRAIKA wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe huenda akavunja mkataba wake na klabu hiyo na kuondoka zake mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, ikiwa timu hiyo haitapata nafasi ya kuwakilisha taifa kwenye mashindano ya kimataifa.

Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe (kushoto) wakishangilia moja ya  bao katika Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Tambwe ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 19, amesema kuwa matarajio yake wakati anajiunga na klabu hiyo yalikuwa ni kuiona ikishiriki mashindano ya kimataifa, hivyo kukosa kushiriki michuano hiyo kutamtibulia mipango yake na ametamka wazi anafikiria kuondoka klabuni hapo.
Simba ipo katika nafasi ya nne na haina matumaini ya kushika nafasi ya kwanza wala ya pili kwa kuwa imesaliwa na michezo minne, ambapo imezidiwa pointi 10 na Yanga inayoshika nafasi ya pili.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe, raia wa Burundi alisema hatma yake ya kuendelea kubakia Simba itajulikana baada ya kumalizika kwa ligi ya msimu huu ambayo ipo katika hatua za lala salama.
Alisema anaweza kuondoka au asiondoke Simba lakini alisisitiza kuwa kila kitu kitajulikana baada ya Aprili 19 ambapo ligi itakuwa inafikia tamati.

“Wakati najiunga Simba, matarajio yangu yalikuwa ni kushiriki mashindano ya kimataifa, lakini ndoto hizo zinaonekana kugonga mwamba kutokana kwa kuwa hivi sasa timu yetu ipo kwenye nafasi mbaya ambayo haitupi kabisa matumaini ya kumaliza ligi tukiwa kwenye nafasi mbili za juu ambazo kwa sasa zinashikiliwa na Azam na Yanga.

“Kusema kweli hali hiyo inasikitisha na inaniumiza sana kwani natamani kushiriki mashindano ya kimataifa kama walivyo wachezaji wote wanaotaka mafanikio katika mchezo wa soka.
“Hata hivyo kwa sasa siwezi kuzungumza lolote kama nitaendelea kubakia Simba au la ila hilo litajulikana baadaye baada ya kumalizika kwa ligi kuu, lakini nafikiri juu ya hilo,” alisema Tambwe.
Simba ina pointi 36 nyuma ya Mbeya City yenye pointi 42, Yanga yenye ponti 46 na Azam inayoongoza msimamo ikiwa na pointi 50.

Wakati huohuo, Tambwe amesema kama atapata nafasi ya kucheza kwenye mechi dhidi ya Azam katika ligi kuu keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, atapambana ili kuhakikisha Azam inafungika.
“Azam ni timu tu kama timu nyingine, naiheshimu kutokana na ubora wake, tutahakikisha tunaivunja rekodi yao ya kutofungwa msimu huu,” alisema Tambwe.
CHANZO CHAMPIONI IJUMAA

WENGI WAMPA UBUNGE RIDHIWANI CHALINZE


Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwan Kikwete.
WANANCHI wa vijiji kadhaa vilivyomo katika Jimbo la Chalinze, ambalo Aprili 6, mwaka huu litafanya uchaguzi mdogo wa Ubunge, wamempa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Ijumaa katika vijiji saba vya jimbo hilo, wengi wa waliohojiwa kuhusu mshindi wa nafasi hiyo, walisema Ridhiwani anashika namba moja kwa vile ni mtu anayejua vizuri maisha ya watu wa Chalinze.

‘MWANAMKE WA MWAKA’ KUTANGAZWA RASMI DODOMA JUMAMOSI HII

UCHAGUZI CBE MWANZA 2014 NI ZAIDI YA URAIS

Huu ni msafara wa mmoja kati ya wagombea uchaguzi wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo cha Biashara CBE Mwanza. 
Hapatoshi.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate