EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, June 30, 2012

Wajerumani kuchukua hatua


Mashabiki wa Ujerumani
Wasimamizi wa soka Ujerumani kuwasilisha malalamiko kwa UEFA kufuatia picha za awali za mwanamke akilia katika matangazo ya moja kwa moja
Wasimamizi wakuu wa televisheni nchini Ujerumani wamesema watawasilisha malalamiko yao rasmi kwa wakuu wa soka barani Ulaya, kufuatia picha za shabiki mmoja aliyetokwa na machozi zikionyeshwa, mara tu baada ya Italia kufunga goli la pili katika michuano ya Euro 2012 katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Shabiki huyo, ambaye ni mwanamke, alikuwa amejipaka rangi zilizomo katika bendera ya Ujerumani, na alielezea kwamba alitokwa na machezo wakati timu ya Ujerumani ilipokuwa ikiingia uwanjani, na wala sio baada ya timu hiyo kufungwa.

Anasema alitokwa na machozi kwa msisimko wa kuwatizama wachezaji wa timu ya nyumbani.
Hii ndio pia Wajerumani wengi waliitizama wakiwa nyumbani.
Wakati Ujerumani ilipoingia katika mashindano hayo, ndio timu iliyotazamiwa na wengi kupata ushindi, na kinyume na hayo, picha walioitizama ya mwanamke kijana akibubujikwa na machozi, na aliyejipaka rangi za bendera ya Ujerumani, nyekundu, manjano na nyeusi, ni jambo ambalo liliwaudhi mashabiki wengi wa Ujerumani.
Suala muhimu hapa ni kwamba mambo hayakuwa hivyo.
Picha hiyo ilitumiwa wakati wa kuonyesha matangazo ya moja kwa moja, na wengi wakadhani mwanamke huyo alikuwa akilia wakati huo.

Hiyo haikuwa mara ya kwanza.
Mapema katika michuano hiyo, kocha wa Ujerumani, Joachim Loew, alionekana akifanya utani na kijana mmoja wa kukimbilia mipira uwanjani, huku akionekana kufurahi, na timu yake ikiendelea kupambana uwanjani, na haikueleweka kwa nini alikuwa akitabasamu na kufurahia hayo.
Picha hiyo ilikuwa imepigwa wakati wa mazoezi, na kisha kutumiwa katika matangazo ya moja kwa moja.
Sasa wanaosimamia matangazo ya televisheni nchini Ujerumani wanasema matangazo ya moja kwa moja lazima yawe hivyo, na pasipo udanganyifu kwa kutumia picha zilizonaswa mapema.

DR.ULIMBOKA AONDOLEWA MUHIMBILI..AMESHA KWEA PIPA S.AFRICA





Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.




Baadhi ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko wa ubongo.

Mwenyekiti huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege aliyosafiri nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na wanaharakati ambao walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja huo.

Mabango ya Madaktari leo...

Picture
Picture
Picture
Picture

Huyu ndo kocha mpya wa yanga



YANGA imethibitisha kwamba kocha Mbelgiji, Tom Saintfiet, atatua nchini kesho Jumapili tayari kusaini mkataba na kuanza kazi rasmi Jangwani.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 39, amewahi kuwa bosi wa Namibia, Zimbabwe, Ethiopia na Mkurugenzi wa Ufundi wa Nigeria.

Kiongozi wa Usajili wa Yanga, Seif Ahmed, aliiambia Mwanaspoti jana akisema: "Tumeshamalizana naye na atatua Jumapili, tutawatangazia mashabiki utaratibu wa mapokezi wakati wa mechi
yetu na Express (ya leo Jumamosi) lakini kimsingi kila kitu kimekamilika na wiki ijayo ataanza kazi baada ya kusaini mkataba.

"Tunataka awe na timu kabla ya mashindano ya Kagame kuanza ili aweze kuzoeana na wachezaji na kuijua timu vizuri."

Lakini ni wazi Kocha Msaidizi, Fred Minziro, ndiye atakayekuwa na kikosi muda mrefu kwani Tom atakuwa akiwasoma wachezaji.

Kocha huyo ana leseni ya kufundisha soka ya Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) aliyoipata mwaka 2000.

Kati ya mwaka 2006 na 2007 alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Emmen inayocheza Ligi Daraja la Kwanza Uholanzi.

Pia amefanya kazi za uchambuzi wa soka katika televisheni za Ubelgiji, Afrika Kusini na Namibia.

Kocha huyo ambaye amesomea saikolojia na uchumi, anazungumza lugha nane za Kiholanzi, Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Faroe, Kiarabu, Kiafrikaan na Kihispania.

Mchakato wa kuanzishwa Mahakama ya Kadhi Tanzania umefikia hatua nzuri - Pinda

Serikali imesema uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi itakayoshughulikia migogoro na masuala mbalimbali ya usatawi wa Waislamu nchini umefikia katika hatua nzuri.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema jana wakati akijibu hoja za wabunge zilizojadili kwenye hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na  Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Alisema itaanzishwa wakati wowote baada ya maandalizi kukamilika na kwamba utekelezaji wake uko katika hatua nzuri baada ya kamati ndogo iliyoteuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria yenye wawakilishi wa Waislamu na Serikali imetoa taarifa yake ya mwanzo ya  namna ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.

Waziri Mkuu alisema mambo yatakayoshughulikiwa na mahakama  hiyo ni pamoja na ndoa na talaka, mirathi, wosia, hiba/zawadi na wakifu vilevile itahusika na mashauri ya jinai.

Alisema, “upo umuhimu na dhamira ya kweli ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara aidha, mahakama hiyo itagharamiwa na kuendeshwa na Waumini wa Dini ya Kiislamu wenyewe.”

Alisema wataalamu wa kuanzisha mahakama hiyo watakwenda  nchini Kenya, India, Uingereza  na Zanzibar kujifunza jinsi ya kuanzisha chombo hicho na kwamba ziara hiyo itagharamiwa na serikali.

via Nipashe

Mali za Tanzania Heart Institute (THI) za Dkt. Masau kupigwa mnada kesho (?)

Kuna taarifa kuwa siku ya kesho, Jumapili, Julai Mosi, 2012, kila kitu kilichokuwa katika hospitali ya Taasisi ya Moyo (Tanzania Heart Institute - THI) kitapigwa mnada.

Wapo watu waliopelekwa huko kuthaminisha vitu vyote inasemekekana vitu vyote lazima vipigwe mnada.
Picture: Tanzania Heart Institute (THI) ya Dkt. Masau
Mwezi Aprili 2012, Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kupitia amri ya mahakama, iliifunga taasisi hiyo na kuwahamishia wagonjwa wote kwenye hospitali nyingine kwa kile kilichoripotiwa ni Taasisi hiyo kushindwa kulipa Shilingi bilioni 7 za pango.

Matangazo yaliyokuwepo kwenye majengo ya hospitali hiyo yalitoa taarifa ya kufungwa kwa hospitali hiyo na kudai kwamba tayari amepatikana mwekezaji mwingine anayetaka kutumia majengo hayo yaliyo barabara ya Tunisia karibu na klabu maarufu ya viongozi ‘Leaders Club’ wilayani Kinondoni.

Tangazo hilo lililokuwa na kichwa cha habari "taarifa kwa umma" lilisema NSSF inatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa, kwa mujibu wa amri ya Mahakama Kuu (kitengo cha Ardhi) iliyotolewa Septemba 11 mwaka jana katika shauri na 158/2007 kati ya NSSF na Taasisi ya moyo Tanzania, “Hospitali hii imefungwa kwa amri ya Mahakama. Jengo ni mali ya NSSF na limepata mwekezaji mwingine” “NSSF itatwaa jengo lake lililojulikana kama "Hosteli ya Tazara" ambapo kwa sasa limepangishwa na THI Julai 25 mwaka huu hivyo wagonjwa wote na familia zao wanashauriwa kufanya mpango mbadala ya hospitali ya kuhama au kuhamisha wagonjwa wao kabla ya tarehe hiyo kufika.” ilinukuliwa sehemu ya taarifa hiyo.

Akizungumza na gazeti la HABARILEO Jumapili kuhusu suala hilo, Meneja Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume, alisema ni kweli taasisi hiyo imefungwa na vifaa vyake kushikiliwa na madalali wa Mahakama kwa sababu mmiliki wake alishindwa kulipa kodi ya pango ya zaidi ya Sh. bilioni 7.

Akizungumzia hatua walizopata kuchukua kabla ya kuamua kuifunga ili walipwe, Chiume alisema walikuwa wakimkumbusha mpangaji kuhusu kulipa au kupisha jengo hilo bila mafanikio na badala yake, miaka mitatu baada ya kukabidhiwa jengo hilo na kushindwa kulipa, alikimbilia mahakamani kuzuia kuondolewa.

Taarifa za NSSF zinasema Dk. Massau alikabidhiwa jengo hilo mwaka 2004 na kuachiwa mwaka mmoja wa kuendesha shughuli zake bure, ili ajipange sawa sawa lakini aliendelea kulitumia bila kulipa hadi alipofungiwa.

Chiume alisema zimejitokeza hospitali kadhaa zinazotaka kupanga, ikiwamo ya Apollo ya India na kwamba wako katika mchakato wa kuangalia kwa undani wampangishe nani ili kuepuka yaliyotokea yasijirudie.

Dkt. Massau alikiri kudaiwa kiasi hicho cha pango na kusema sababu za kutolipa zilikuwa wazi kwa shirika hilo.

“Ni kweli wananidai, lakini wanajua kesi ilikuwa mahakamani na tulipaswa kurudi huko Aprili 24, ili kujua kinachoendelea, lakini wamekuja kuvamia usiku wa Aprili 10, na kupiga watu na kubeba wagonjwa kuwapeleka kusikojulikana, tumelalamika mpaka kwa Jaji Mkuu na tutafika mahakamani siku hiyo ya kesi, tukiwa na malalamiko yetu juu ya kukiukwa kwa sheria,” alisema Dkt. Masau.

Alikanusha kupangishwa mwaka 2004 na kudai kuwa alikabidhiwa jengo hilo la ghorofa mbili Mei 2005 likiwa na kasoro nyingi zilizofanya washindwe kuendesha shughuli za upasuaji wa moyo na hivyo kuendesha huduma za matibabu mengine ya moyo tofauti na makubaliano na wafadhili. 
Picture
Dkt. Masau
Mwaka 2008, Dkt. Masau aligoma kuhama katika jengo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa mkutano wa VC uliopo ndani ya Jengo la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) muda mfupi baada ya kumalizika kwa semina ya madaktari wa moyo mwaka huo, alisema yeye hawezi kuhama katika jengo hilo kwa sababu NSSF imeshindwa kutimiza makubaliano yao wakati walipompangisha na kuongeza, “Kwanza siwezi kuhama katika jengo hilo kwasababu kuna wagonjwa 15 wamelazwa ambapo kati yao wagonjwa 5 wanategemea kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati wowote, pili vitu ambavyo viko ndani ya jengo hilo ni zaidi ya bilioni, makubaliano yetu ilikuwa ni kutengeneza jengo hilo ili liwe na hadhi ya hospitali ya moyo kitu ambacho walishindwa kuyatimiza,” alisema Dkt. Masau.

Alisema moja ya makubaliano yao ni kwamba NSSF wamtengenezee jengo liwe na hadhi ya Hospitali ya Moyo.

Alisema baada ya makubaliano hayo NSSF walimpelekea taarifa kuwa kazi hiyo imeshamalizika hivyo anachotakiwa kufanya ni kukubali kusaini mkataba wa kulipangisha jengo hilo.

“Nilikubali kusaini mkataba wa kama mpangaji baada ya NSSF kunihakikishia kuwa wamenitengenezea jengo hilo kama nilivyowaeleza, lakini baada ya kusaini mkataba na kuingia ndani ya jengo nikagundua kuwa kuna baadhi ya maeneo hayajatengenezwa kama nilivyoyahitaji,”alisema Masau na kuongeza:

“Baada ya kubaini mapungufu hayo tulikubaliana niendelee kulitumia jengo hilo wakati marekebisho hayo yanafanyika, lakini hayo hayakufanyika badala yake nilishangaa kuona taarifa ya kuitwa mahakamani kwa kesi ya madai miezi miwili baada ya mkataba huyo,”alisema.

Alifafanua kuwa baada ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa mahakamani miezi miwili baadaye hukumu ilitolewa na mahakama ikaamuru aondolewe katika jengo hilo na kwama baada ya amri hiyo alimfuata Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambapo Waziri aliwataka wayamalize nje ya mahakama chini ya Wizara ya Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana.

Hata hivyo, kufuatia taarifa za ndani ya NSSF zilizonaswa na gezeti MWANANCHI, Serikali ilishawahi kutoa tamko kuwa haiwezi kingilia zaidi mgogoro huo na kuwataka wamalize mgogoro huo kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo za siri pia ilibaini kuwa Julai 5, Waziri wa Kazi Ajiri na Maendeleo ya Vijana wa wakati huo, Profesa Juma Kapuya alimuandikia Dkt. Masau barua iliyosema kuwa endapo atashindwa kulipa sehemu ya deni hilo kama walivyokubaliana katika kikao cha Julai Mosi mwaka huu NSSF itaendelea na uamuzi wake wa kumtoa ndani ya jengo hilo.

“Tulikubaliana kuwa endapo taasisi yako itashindwa kulipa sehemu ya deni hilo kama inavyopendekezwa basi NSSF itaendelea na uamuzi wake wa kuitoa hiyo THI kwenye jengo hilo kama iliyoamuriwa na mahakama bila kutoa notisi nyingine,”ilisema sehemu ya barua hiyo ya Waziri Kapuya.

Hata hivyo, nakala ya barua ilipelekwa kwa Waziri Mkuu,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na NSSF. 
picha via Charaz.blogspot.com

‘Mama kanitia aibu’


Na Shakoor Jongo
Wema Isaac Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu hawapo vizuri tangu yale mahojiano aliyoyafanya mzazi wake huyo runingani wiki mbili zilizopita akiwachana marafiki wa staa huyo mkubwa wa picha za Kibongo, Risasi Jumamosi linafunguka.
ALIJISIKIAJE?
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi Alhamisi ndani ya Ofisi za Global Publishers, Wema alisema kuwa hawezi kusahau siku mama yake alipofanya ‘intavyu’ kwani aliposikia anaaza kutiririka ilibidi aipigie magoti runinga akiiomba inyamaze akidhani inamsikia.

TUJIUNGE NA WEMA AKITIRIRIKA!
“Kwanza sikuwepo wakati mama anafanya intavyu ‘so’ sikutarajia kama angezungumza vitu vya namna ile.
“Ni kweli mama yangu kama mzazi alikuwa na kila sababu ya kunizungumzia, alikuwa na uchungu na mwanaye sawa! Lakini ‘mai mom’ alipitiliza.”

ALITAKIWA KUHARIRIWA?
“Nadhani kuna vitu vilitakiwa kuondolewa kwa sababu mara baada ya kuzungumza, hali ilikuwa mbaya sana kuanzia kwenye mitandao ya kijamii na hata dada yangu alinipigia simu nikamweleza nilivyojisikia vibaya.”
KANITIA AIBU!
“Nilijua mama kanitia aibu lakini nikajikaza kwa sababu utakumbuka ndo’ kwanza nilikuwa kwenye maandalizi ya uzinduzi wa filamu yangu ya Super Star.
“Nilikaa kimya, nilijifanya kama hakuna kitu chochote kilichotokea lakini si unajua lazima moyo utakuuma tu hata kama ukijifanya kusahau.
“Baada ya kuona nipo kimya ‘aithinki’ siku iliyofuata alinitumia meseji mbaya na ninazo lakini hadi leo sikumjibu.”
TUNAWEZA KUSEMA ALIKUDHALILISHA?
“Yaah…ukweli ‘situwesheni’ haikuwa nzuri. Meneja wangu Martin (Kadinda) alimpigia mama na kumsisitiza mwaliko niliokuwa nimempa wa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu yangu lakini amini usiamini mama yangu hakuhudhuria. Kwa upande wa baba naye hakufika lakini alinipa sababu za msingi kabisa nikamwelewa na pia alikuwa akifuatilia kila kitu kwa kuchati na dada yangu kwani alijua niko bize.”
VIPI KUPELEKWA KWA WAGANGA?
“Sijui mama alipata wapi hiyo kitu ‘coz’ sijawahi na wala sijui mambo ya waganga kama alivyozungumza yeye.”
NISAMEHENI SANA
“Kwa yeyote aliyeguswa na mama kwa namna yoyote, naomba anisamehe sana. Yaani magazeti ya Global naombeni muwe wa kwanza kunisamehe kwani yule ni mzazi wangu pamoja na yote, nampenda sana.”
NENO LA RISASI JUMAMOSI
Wema ameamua kutoa la moyoni mwake akiamini kuwa yeye ni staa kwa hiyo ni kioo cha jamii, hataki kuwepo na chuki kati yake na vyombo vya habari, kwa maana hiyo AMESAMEHEWA.
 CHANZO CHA HABARI  Globa.

Bob Junior: Nimempata kitu cha ukweli


                                                                        Halima Ally
 Nyota wa filamu kutoka visiwani Zanzibar Halima Ally ‘Imma’ ndiye anayetarajiwa kulamba shavu la kuwa mke halali wa Bob Junior.Taarifa kutoka visiwani humo zimesema kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia uhusiano wa muda mrefu uliokuwepo baina ya wawili hao.Hakuna mwingine ni Halima, siku zote Bob junior amekuwa akija huku tunawaona wako pamoja na istoshe Halima alituambia kuwa wakati wowote atakuwa mke wa mtu” kilisema chanzo Halima alikuwa mmoja wa mastaa walioshiriki filamu ya Royal Prince iliyotayarishwa visiwani humo chini ya kampuni kubwa El- Fahad Production

MSANII machachari wa Bongo Flava, Bob Junior a.k.a Rais wa Masharobaro, anaachana na kambi ya ukapera na kuanza maisha mapya atakapofunga ndoa kesho Jumapili.

Msanii huyo aliyetamba na nyimbo za 'Oyoyo', 'Andazi', 'Mapenzi ya Kweli' pamoja na 'Nichumu' zinazoendelea kusumbua katika vituo mbalimbali vya redio na runinga ndani na nje ya Tanzania, amesema ameamua kuvuta jiko kwani wakati wake umefika.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bob alisema: "Huu ni muda wa kupata mwenzangu nitakayeshirikiana naye kwa kila jambo. Ninafanya hivi ili kujiepusha na anasa za dunia maana mambo ni mengi.

Anafafanua kuwa mwanamke anayetarajia kumwoa amekidhi vigezo ambavyo yeye binafsi anavihitaji kwa mke.

"Ndoa si kukurupuka. Nimekuwa makini mno kufikia uamuzi huu ili kuepusha migongano au migogoro ndani ya ndoa, nimechagua mwanamke ambaye naona kabisa amekidhi vigezo ninavyohitaji na mwenye tabia ambazo tunaendana, alisema.

Akivitaja vigezo hivyo anasema siku zote alihitaji kuwa na mke mwenye tabia njema, aliyelelewa katika maadili na misingi ya dini yake ya Kiislamu na mwenye kupenda kumcha Mungu.

Anasema ingawa katika hali ya kawaida ni ngumu kumpata mwanamke mwenye vigezo hivyo, lakini kwa upande wake amebahatika kumpata mwanamke huyo kutoka visiwani Zanzibar.
 
Nimelelewa katika misingi ya Kiislamu na ndiyo maana nahitaji mke ambaye pia atakuwa amejengwa vizuri katika misingi hiyo ili aweze kunisukuma niweze kumcha Mungu kama ilivyokuwa awali," alisema.

"Unajua kidogo siku hizi nimetawaliwa na mambo ya dunia sasa lazima kuwa na mtu atakayesaidia kuniweka sawa."

Anasema kutokana na hilo hapo kesho anatarajia kupanda boti mpaka visiwani Zanzibar ambapo ataenda kufunga ndoa na baadaye kumtambulisha rasmi mkewe kwa mashabiki wake kwenye shoo maalum itakayofanyika katika klabu ya Billicanas iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Nitapangilia kila kitu kwa muda wake kwani natakiwa nisiwanyime burudani mashabiki wangu na vilevile lazima niwajibike kwa mke wangu," aliongeza.

"Nina uhakika kwa kupanga ratiba vizuri, nitamudu bila wasiwasi wowote, naweza kusema ndoa itanipa changamoto ya kutafuta zaidi ili kuhakikisha familia ninayokwenda kuianzisha inapata mahitaji yote muhimu, mwanaume lazima uimudu familia.

Licha ya kuwa mwanamuziki, Bob Junior pia ni mtayarishaji wa muziki katika studio yake inayoitwa Sharobaro Records ambayo imefanikiwa kutengeneza nyimbo mbalimbali.

Miongoni mwa nyimbo zilizopita katika mikono yake ni pamoja na 'Lofa' ya Top C, 'Kamwambie' ya Diamond, 'Far Away' ya Big Jahman na nyinginezo kadhaa.

Dogo Janja bado apigwa danadana

WIKI mbili zilizopita msanii Dogo Janja alijitoa katika kundi la Tip Top Connection na kurudi kwao Arusha kwa basi, lakini sasa amerejea Dar es Salaam kwa ndege na kusaini mkataba na kundi la Watanashati linaloongozwa na Ostaz Juma.

Lakini katika hali ya kushangaza, meneja wake mpya huyo tayari ametangaza kuwa yeyote ambaye yupo tayari kumchukua kijana huyo anaweza kufanya hivyo. Kauli ya Ostaz Juma imezua maswali.

Dogo Janja alipokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita na wadau lukuki wa muziki wa kizazi kipya.

Mapokezi yake hata hivyo yameibua maswali kuhusiana na hatua ya wazazi wa kijana huyo kumwachia bila ya uangalizi maalum. "Unajua japokuwa watu wengi wamesema kuwa mimi nilikosea, lakini hawajui lolote. Ninayejua ni mimi mtendwa, wengi walikariri yaliyosemwa na Tip Top kuwa mimi nilikuwa mtoro, mkaidi," alisema Dogo Janja akiwa uwanjani hapo.
"Lakini mimi nasema kama kweli ningekuwa na vitendo hivyo wasingetokea watu wengine na kunifadhili."

Japokuwa mkataba wa makubaliano ya ufadhili huo na kampuni ya Watanashati uko tayari Janja amesema bado hajasaini mkataba huo. "Kuna watu wangu bado nawasubiri watakapouona huo mkataba na kuridhika nao basi kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga, unajua lazima ujiridhishe kwanza na hiyo ndiyo mipango," alisema.

Kuhusu shule, Dogo Janja, aliyekwama kuendelea na masomo ya Kidato cha Pili katika Sekondari ya Makongo, alisema ataendelea lakini katika shuke nyingine aliyoahidiwa na Ostaz Juma.
"Kuna mengi tumezungumza na kukubaliana kuwa katika suala la shule nitakuwa nikipelekwa kwa gari na nisome katika shule binafsi nzuri na pia niendelee na muziki," alisema.

"Mbali na muziki, sasa hivi nitakuwa naigiza na filamu pia pamoja na akina Kitale maana tuko nao kwenye kundi moja la Watanashati."HABARI NA HERIETH MAKWETTA

Serikali ya Tanzania kuleta Madaktari kutoka nje ya nchi - Bilioni 200 zatengwa kuwalipa

Serikali imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais Kikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote zilizofanywa kuboresha maslahi yao.

Kwa mujibu wa habari hizo, kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili ya kuwaleta na kuwagharimia  madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama  Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.

Habari zimedai kuwa madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki, zikiwemo India, China, Cuba na Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao wamegoma.

Inaelezwa kuwa mara baada aya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa kazini kwa masharti makali.

Hata hivyo, uamuzi wa serikali  kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.

Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni, lakini walikwama baada ya Spika Anna Makinda  kuzuia mjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani.

Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali ni kiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda  alisema serikali  haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani, “Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani, sasa imewezaje kuwafukuza madaktari wakati jambo lipo mahakamani?” alihoji Dkt. Kigwangala.

Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadiliano kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuru wa mahakama.

Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza  kulipwa posho zao za mwezi mmoja.

Hospitali zingine ambako madaktari wamefukuzwa kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.
Martin Malera, 
Tanzania Daima 
Dodoma  

Leo imetimiza miaka sita tangu baba yetu Mpendwa ulipotutoka Mzee Obel Benson Mwamfupe

Mzee Obel Benson Mwamfupe! 
Leo imetimiza miaka sita tangu baba yetu Mpendwa ulipotutoka. Kibinadamu ni ngumu sana lakini tunamshukuru Mungu baba wa mbinguni aliyeweza kututia nguvu na faraja tele mpaka leo hii tuko hivi tulivyo! Tunakukumbuka kwa upendo na hekima zako. 

Baba, ulikuwa kama mti mkubwa na sisi tulikuwa kama ndege tulioweka makazi kwako! ulipoanguka tuliyumba sana, tunazidi kumshukuru Mungu hata kwa hili maana hajatuacha! Akatukusanya tena. Unakumbukwa na familia yako yote wakubwa kwa wadogo. Mungu akupe pumziko la Amani.

Irine 'Uwoya' Sizari ndiye Redds Miss Ubungo 2012

 Redds Miss Ubungo 2012, Irine Sizari, akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo na kuwabwaga warembo wengine 14 usiku huu katika Ukumbi wa Land Mark Hotel jijini Dar es Salaam.
 Redds Miss Ubungo 2012, Irine Sizari (katikati) akipunga mono baada ya kuvukwa taji hilo na kupata tiketi ya kushiriki Miss Kinondoni 2012. Kushoto ni Mshindi wa Pili, Mwantumu Mustafa na kulia ni Mshindi wa tatu, Antonia Nyaragwinda. Shindano hilo limefanyika Juni 29, 2012 kuamkia Juni 30.
  Redds Miss Ubungo 2012, Irine Sizari (katikati) akipunga mono baada ya kuvukwa taji hilo na kupata tiketi ya kushiriki Miss Kinondoni 2012. Kutoka Kushoto ni Mshindi wa Tano, Joyce Raphael, Mshindi Pili, Mwantumu Mustafa, , Mshindi wa tatu, Antonia Nyaragwinda na kushoto ni Mshindi wa nne Wema Mwanga. Shindano hilo limefanyika Juni 29, 2012 kuamkia Juni 30.
 Kamati ya Miss Tanzania na warembo wa mawaka 2011 wakipiga picha na washindi
 Jaji Mkuu, Christina Manongi 'Sinta" akisoma majina ya washindi.
 Wadau wakifuatilia shindano
 Meza kuu iklifuatilia shindano
 Vimwana wa Miss Sinza inayotaraji kufanyika July 20.
Wanenguaji wa Kundi la FM Academia wakisakata ngoma za Bendi hiyo.Via  http://mrokim.blogspot.com

JK AFUNGUA HOSTEL YA MISHENI KATOLIKI JANA HUKO BAGAMOYO

1: Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kama Mgeni Rasmi kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris jana Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa
wa Pwani.

2. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wenyeji wake kwenye kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris aliyoizindua jana Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
3.Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa shangwe alipowasili katika ukumbi wa mikutano kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris jana Juni 29. 2012 huko Bagamoyo,

                 JK Na Form Six Wa Marian Girls

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wa Marian Girls Secondary school kwenye kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris aliyoizindua jana Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Picha: IKULU

WaEthiopia waliofariki Tanzania wazikwa Ipagala

Picture
Picture
Wahabeshi 21 kati ya 43 waliokufa wakivushwa katika ardhi ya Tanzania, walizikwa leo katika makaburi ya Ipagala, manispaa ya Dodoma huku wenzao wakilia kwa uchungu na simanzi kubwa.

Naibu  Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alihudhuria maziko hayo na kutaka kuwepo kwa juhudi za pamoja za nchi za Afrika Mashariki kukomesha biashara hiyo ya kusafirisha binadamu kwani zina madhara makubwa Kitaifa na Kimataifa.

Mmoja kati ya wahabeshi waliokuwa wazima amepoteza ndugu zake watatu alionekana kuwa na dhiki kubwa kiasi cha kulazimi atafutwe mkalimani wa kumfariji.

Waziri Silima pia alitoa pole kwa wananchi wa Ethiopia ambao wamepoteza watu wao na kusema kuwa atahakikisha matukio kama hayo hayatokei tena. Akasema Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi juu ya tukio hilo na kutaka wananchi wapewe elimu zaidi ili waache biashara ya kusafirisha binadamu.
Picture
Picture
Picture
via Lukwangule.blogspot.com

Tamko: Maazimio ya Madaktari Mabingwa wa Hositali za Mkoa wa Dar es Salaam

TAMKO LA MADAKTARI MABINGWA WA MKOA WA DAR ES SALAAM
(MNH, MOI, OCEAN ROAD NA HOSPITALI ZA MANISPAA YA MKOA WA DAR ES SALAAM)

-------------------------

Kutokana na kikao kilichofanyika leo tarehe 29/06/2012, Madaktari mabingwa tumeamua yafutayo:


  1. Tunalaani kwa kauli moja kitendo alichofanyiwa Daktari na Kiongozi wa Jumuiya yetu, Dkt. Steven Ulimboka, cha kutekwa, kuumizwa na kutupwa msitu wa Mabwepande. Kitendo hiki kimetuhuzunisha, kimetufadhaisha na kutufanya kuishia katika hofu ya hali ya juu.
  2. Tunazitaka Mamlaka husika kutuhakikishia mustakabali wa usalama wetu sasa na siku za mbeleni katika nchi yetu.
  3. Tunalaani juhudi zinazofanywa na wadhalimu wote katika fani ya Udaktari.
  4. Tunalaani vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa Madaktari wenzetu sehemu mbalimbali kama Bugando, Dodoma na Mbeya pamoja na kwingineko.
  5. Tunatamka wazi kuwa kitendo cha kuwafukuza, kuwanyima mishahara na haki nyingine za mwezi Juni, ni udhalilishaji na kinyume na amri ya mahakama.
  6. Kutokana na vitendo vyote tajwa hapo juu, (yaani kutekwa na kuteswa kwa Dkt. Ulimboka, Unyanyasaji wa Madaktari wenzetu) na pia kutokana na ukweli kwamba hali ya Dkt. Ulimboka inazidi kudorora; vile vile kwa kuwa siku zote Serikali imekuwa ikikubali kuwa madai yetu ni ya msingi (lakini haiyatafutii ufumbuzi wowote), TUMEAMUA KUSIKISHA KUTOA HUDUMA KATIKA HOSPITALI ZOTE TUKAZOFNYIA KAZI, yaani Muhimbili, MOI, Ocean Road, Amana, Mwananyamala, n.k. hadi hapo madai yetu ya msingi yatakaposikilizwa na kutekelezwa.
  7. Tunaomba Madaktari mabingwa wote hapa nchini watuunge mkono katika harakati hizi za kuboresha sekta nzima ya afya.
 
IMETOLEWA NA
DKT. C. MNG’ONG’O
MWENYEKITI WA MADAKTARI MABINGWA - KANDA YA DAR ES SALAAM

Friday, June 29, 2012

Mbunge ahoji faida ya mbio za Mwenge



MBUNGE wa Michewene, Haji Khatib Kai (CUF), jana aliihoji Serikali akiitaka kutoa maelezo ya kina juu ya faida zinazopatiana kwa Watanzania juu ya mwenge wa Uhuru.Kai alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali kwa Waziri Mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo ambayo huulizwa siku ya Alhamishi.

Mbunge huyo alisema katika kipindi kirefu amekuwa akishangazwa na kitendo cha Serikali kuendelea kupigia debe mbio za mwenge huku ikitambua kuwa unafanya kazi ya kuhamasisha mambo ya ngono katika mikusanyiko ya mikesha.

“Mheshimiwa Spika, mkesha wa mbio za mwenge mara nyingi huhamasisha masuala ya ngono ambayo hueneza Ukimwi na magonjwa mengine, je hamuoni kuwa jambo hilo ni kosa na halina faida kwa mustakabali wa nchi yetu,’’ alihoji Kai.Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa zipo faida nyingi katika mbio za mwenge Kitaifa na uwepo wake una umuhimu mkubwa zaidi kuliko inavyotazamiwa na wengi.

Pinda alisema kuwa kila Taifa duniani lina utaratibu wake katika kutengeneza mpango sahihi wa mambo ambayo hufanywa ili kusaidia kukumbuka mambo yao“Kwanza sio kweli kama mwenge unahamasisha mambo ya ngono, hapana, watu wanaweza kufanya mambo hayo wakati wowote, lakini kikubwa ni kwamba mwenge una faida kubwa zaidi na ninaomba ndugu zangu tuendelee kuamini na kuuheshimu,’’ alisema Pinda.
 
Alitolea mfano wa mbio za Olimpiki ambazo hukimbizwa katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha mambo kadhaa ikiwemo amani na mshikamo.Waziri Mkuu alisema wazo la Mwenge liliasisiwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alipotaka kuweka chombo ambacho kinaibua hisia za watu katika kukumbuka shughuli za kimaendeleo.Aliyataja baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na kuzindua miradi mbalimbali na kuweka mawe ya msingi kwa maeneo tofauti kila wakati.

Kwa mujibu wa Pinda, kauli mbiu zinazotolewa katika mbio za mwenge huwafikia wananchi kwa urahisi zaidi kwani mbio hizo hukusanya idadi kubwa ya watu kwa mara moja.
                          Habari na Habel Chidawali,Dodoma

Yanga yawatupia virago nyota 11

MABINGWA wa Soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga ya jijini Dar es Salaam, wametangaza kuwatema wachezaji wake 11 kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mchakato wa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara kuwasilisha majina ya wachezaji wanaoachwa ama kumaliza mikataba unafikia tamati kesho.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema jijini Dar es Salaam jana kwamba klabu yake imewaacha wachezaji hao, ambapo kati yao kuna waliomaliza mikataba yao na wengine kupelekwa kwa mkopo klabu nyingine za Ligi Kuu bara.

Aliwataja wachezaji walioachwa kuwa ni pamoja washambuliaji wa kimataifa, Mghana Keneth Asamoah na Mzambia Davies Mwape, huku wengine wakiwa Iddi Mbaga, Julius Mrope, Kiggi Makassi, Atif Amour, Abuu Ubwa, Zuberi Ubwa, Bakari Mbegu, Godfrey Bonny na Shaban Kado ambaye amepelekwa kwa mkopo Mtibwa Sugar.
Aidha Sendeu alisema kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi yake, ambapo kesho kitashuka katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na mabingwa wa soka nchini Uganda, Express.

Alisema, Express ilitarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam jana, ambapo kiingilio kitakuwa ni sh 20,000 kwa VIP A, sh 15,000 VIP B na C, sh 5,000 kwa watakaokaa viti vya kijani na wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na chungwa watalipa sh 3,000.
Katika hatua nyingine, klabu hiyo leo inatarajiwa kuendesha kisomo maalum ‘hitma’ kwa ajili ya kuwarehemu wanachama, mashabiki, wapenzi na wachezaji wa timu hiyo waliotangulia mbele ya haki, ambapo zoezi hilo litafanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko mitaa ya Jangwani na Twiga na kuongozwa na Katibu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali.

“Kama mnavyojua, kila msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unapokaribia kuanza, huwa tunasoma dua ya kuwarehemu wadau mbalimbali wa Yanga waliotangulia mbele ya haki, hivyo kesho (leo), majira ya saa sita mchana, hapa klabu tutaendesha kisomo hicho ambacho kitaongozwa na Sheikh Akilimali (Ibrahim), hivyo tunaomba Wanayanga kujitokeza kwa wingi,” alisema Sendeu.
Sendeu aliongeza kuwa baada ya dua hiyo, jioni ya leo kutakuwa na mkutano maalumu utakaohusisha wenyeviti na makatibu wa matawi yote ya Yanga ya jiji la Dar es Salaam.
                                 Chanzo cha habari na Dina Ismail wa Tanzania Daima

Rose Ndauka akubalika Ghana

Kipaji cha kuigiza cha msanii nyota wa filamu za Tanzania, Rose Ndauka kimewakuna Waghana na kumtabiria kuwa msanii atakayekuja kuwa juu sana barani Afrika.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa nchini humo, filamu za staa huyo zinanunuliwa kwa kasi ambapo amshabiki wengi walidhani ni msanii kutoka Nollywood kama si kubabaishwa na Kiswahili inayotumika kwenye filamu zake.

Miezi mitatu iliyopita, staa huyo alikwenda nchini Ghana kufanya kazi za filamu kwa kushirikiana na wasanii wa huko, kazi hizo zitaanza kuoneka na kwenye runinga za kimataifa hivi karibuni.
Kwa nchini Tanzania, Rose ambaye ni mchumba wa msanii wa Bongo Fleva, 
Maliki Bandawe, anazidi kufanya vizuri katika kazi zake za sanaa ambapo amefanikiwa kufungua kampuni yake ya kutengeneza filamu ya Ndauka Entertainment.
Kwa upande wa mchumba, Rose anatarajia kufunga ndoa mwaka huu ingawa tarahe haijapangwa. 

NAKAAYA ALIA KUPORWA BWANA



                        Nakaaya akiwa na Peter.
Na Musa Mateja
MWANAMUZIKI Nakaaya Sumari, juzikati alimwaga machozi huku akidai kuibiwa bwana’ke na mwanamke mwenzake aliyemtaja kwa jina la Beatrice, Ijumaa linakupa mchapo.  Kwa mujibu wa chanzo chetu, Nakaaya amekuwa hana raha baada ya kuzidiwa ujanja na Beatrice ambaye inadaiwa ni mzazi mwenza wa mwanaume huyo anayetajwa kwa jina la Peter.
“Yaani Nakaaya hana raha kabisa baada ya kuchukuliwa bwana wake. Lakini sisi uhusiano wake na Peter hatukuwa tunaujua na inaonekana walikuwa wakitoka kwa siri sana,” alisema sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake .
Ijumaa lilipozinasa habari hizi lilimwendea hewani msanii huyo ambaye alipopatikana alitoa ushirikiano kwa paparazi wetu akisema:

“Ni kweli kumetokea msuguano kati yangu na Peter ambaye nilikuwa nampenda sana na tukadumu kwa miaka miwili, lakini niligundua amempa mimba mwanamke mwingine,” alisema Nakaaya na kuongeza:
“Mimi sitaki shari naye kwa kuwa tabia yake haijanifurahisha, nina mambo mengi ya kufanya kama Peter bado anamzimia basi waendelee ila Beatrice asiwe ananisumbua maana nimechoka na mapenzi ya kushea bwana, bora nizame kwenye game la muziki kama mwanzo,” alisema Nakaaya.
Kwa upande wa Peter, alipoulizwa kuhusu madai hayo, alikiri na kusema kuwa ameamua kuendeleza uhusiano wake na Beatrice ambaye yuko naye kwa zaidi ya miaka mitano baada ya kuona Nakaaya haelekei.

“Nilikuwa nampenda sana Nakaaya lakini nimeshindwa baada ya kusikia ana bwana mwingine wa Kizungu, nisingeweza kuendelea naye bora niendelee kudili na kazi zangu na maisha mengine, mapenzi ya ki-supastaa yamenishinda,” alisema Peter.

RAY, MAINDA WABAMBWA LAIVU

 
Na Shakoor Jongo
MASTAA wawili katika tasnia ya filamu Bongo ambao wanatajwatajwa kuwa ni wapenzi wa siku nyingi, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Ruth Suka ‘Mainda’ juzikati walinaswa ‘live’ katika mapozi yaliyoacha vingi viulizo.
Wawili hao walibambwa ndani ya Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempinski, Posta jijini Dar, usiku wa Juni 23, mwaka huu kulikokuwa na uzinduzi wa Filamu ya Super Star ya Wema Sepetu.
Wakiwa ukumbini hapo, Ray alionekana akimshika mkono Mainda kama mtu aliyemtaka waondoke lakini pia akaonekana akimnong’oneza jambo demu huyo.
Haikuweza kufahamika mara moja walichokuwa wakiteta lakini baada ya muda, msanii Steven Mangere 

‘Nyerere’ alitokea na kumkumbatia Mainda huku akitaka kuondoka naye.
Wakati Steve akifanya hivyo, Ray alionekana akimuonya kitu Mainda huku akimnyooshea kidole ambapo mdau mmoja aliyekuwa ukumbini hapo alisikika akisema: “Mh! Sijui huyu Ray na Mainda bado ni wapenzi au wameshabwagana, maana mapenzi ya mastaa yamekuwa ni kizungumkuti siku hizi.”
Ijumaa lilizungumza na Mainda kutaka kujua kama bado anatoka na msanii huyo lakini alijibu kwa kifupi: “No Comment.”Habari na Global

Madaktari bingwa nao wagoma


Katibu wa Jumuiya ya Madaktari,Dk Edwin Chitage akitoa tamko la Jumuia hiyo kwa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam la kutokuwa na imani na Tume iliyoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio la kupigwa kwa Mwenyekiti wao Dk Stephen Ulimboka.Picha na Fidelis Felix
TUKIO la kutekwa nyara, kupigwa na kujeruhiwa vibaya, kisha kutupwa katika Msitu wa Pande uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka, limechochea kasi ya mgomo baada ya madaktari bingwa kutangaza kujitosa rasmi kwenye mgogoro huo.Awali madaktari hao hawakushiriki mgomo huo, lakini jana walieleza kwa nyakati tofauti kuwa, wameamua kuungana na wenzao kutokana na unyama aliofanyiwa kiongozi wao akiwa katika harakati za kutetea na kupigania haki zao.

Madaktari hao wa hospitali za Muhimbili, Moi, KCMC, Mbeya, Bugando na Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, jana walitangaza rasmi kuwa wameingia kwenye mgomo huo kushinikiza pamoja na mambo mengine, Serikali kutoa tamko kuhusu utata wa tukio hilo.

Tukio hilo la aina yake kutokea nchini, limeathiri upatikanaji wa huduma zote za matibabu katika hospitali hizo, huku madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Moi, wakielekeza nguvu zao kunusuru maisha ya mwenzao aliyeumizwa.

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitage, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mgomo huo utaendelea hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yao.

"Tunaitaka Serikali kuacha vitisho kwa madaktari nchini, tunaitaka itambue kwamba mgogoro huu hauwezi kumalizwa kwa njia yoyote vikiwemo vitisho bali ni kwa kukaa meza ya majadiliano na kukubaliana na madaktari," alisema Dk Chitega na kuongeza:

"Ninawashukuru madaktari wote nchi nzima, wauguzi na wafanyakazi wa sekta ya afya kwa ujumla wao kwa kusitisha huduma baada ya kupigwa mwenzetu. Tunaomba mshikamano huu uendelee," alisema Dk Chitega.

Gazeti hili lilishuhudia wagonjwa wakiwa wamekaa katika makundi bila kujua la kufanya, huku wengine wakiamua kuondoka na kwenda hospitali binafsi.

Waliliambia Mwananchi kwamba kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka ni cha kinyama na kuungana na madaktari hao kuitaka Serikali kutatua mgogoro huo haraka.

Wagonjwa waliofika katika eneo hili pia walielezwa bayana na maofisa wa Moi kwamba huduma zimesitishwa  kutokana na madaktari kugoma.

Ocean Road

Madaktari bingwa katika Taasisi ya Ocean Road nao waligoma kutoa huduma hatua iliyozua taharuki kwa wagonjwa waliofika kwa ajili ya matibabu.

Gazeti hili lilishuhudia ofisi za madaktari hao zikiwa zimefungwa na hata zile ambazo zilikuwa wazi, madaktari hawakuwapo.

Mmoja wa wagonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Joyce Dachi, alisema kuwa, wagonjwa wengi wamekuwa wakiandikishwa mapokezi, lakini wanachukua muda mrefu kumuona daktari.


Mgomo huo pia umeendelea katika Hospitali ya Amana wilayani Ilala huku uongozi wa hospitali hiyo ambao uligoma kuzungumza na vyombo vya habari, ukihaha kunusuru hali hiyo.

Katika Hospitali za Temeke na Mwananyamala huduma ziliendelea kutolewa kama kawaida.

Mbeya

Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ,madaktari bingwa ambao awali hawakugoma jana waliingia kwenye mgomo na kusababisha wagonjwa katika hospitali hiyo hususan kitengo cha wazazi, kusota bila matibabu.

Habari kutoka katika hospitali hiyo zilieleza kuwa hivi sasa madaktari bingwa wanatoa huduma kwa kujuana.

Mmoja wa madaktari hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema kitendo alichofanyiwa Mwenyekiti wa Jumuiya yao kimewakatisha tamaa.

Alisema kuwa, hali hiyo sasa imehamia hadi katika Kituo cha Wazazi cha Meta na kufafanua kuwa hali ni mbaya, tayari wajawazito wametakiwa kuhamia katika Hospitali ya Mkoa ambayo imefurika wagonjwa.

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo ya Rufaa, Dk Eliuter Samky hakuweza kuzungumzia tukio hilo jana kutokana na kile kilichoelezwa na katibu wake muhtasi kwamba ana kazi nyingi.

Mwanza
Madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) mkoani Mwanza nao wamegoma, huku kiongozi wa Kamati Ndogo ya hospitali hiyo inayoshughulikia migomo, akikataa kuzungumzia hali hiyo.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu baada ya kutoonekana katika maeneo ya hospitali, mmoja wa viongozi wa Kamati hiyo, Dk Geogre Adrian, alisema kwa sasa hawezi kulitolea ufafanuzi suala hilo na kwamba kufanya hivyo, ni kwenda kinyume na maagizo aliyopewa na Kamati Kuu.


Akizungumzia huduma katika hospitali hiyo alisema kuwa hajui lolote kwa kuwa hawajagusa maeneo ya kazi kwani  wapo kwenye mgomo.

Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia huduma katika hospitali yake, hakupatikana.

Watimuliwa
Jana Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Charles Majinge alitoa tangazo la kuwataka madaktari waliopo mafunzoni ‘Interns’ katika hospitali hiyo kurejea kazini na kama watakiuka agizo hilo, watakuwa wamejifukuzisha wenyewe.


Manyara
Mkoani Manyara, madaktari kumi katika Hospitali ya Haydom Wilaya ya Mbulu wamegoma tangu juzi.Idadi ya wagonjwa katika hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), inaongezeka siku hadi siku.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa masharti ya kutotaka kutajwa majina yao, madaktari hao ambao wanafanya mafunzo ya vitendo katika hospitali hiyo, wamesema kuwa hawatatibu wagonjwa mpaka madai yao yatekelezwe.


Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Anatory Choya, alithibitisha kutokea kwa mgomo huo na kufafanua kwamba wanaendelea kufanya mazungumzo ili kupata ufumbuzi.

Choya alisema kuwa madaktari wanaoendelea na kazi, wameelemewa  kutokana na wagonjwa kuwa wengi.

Alisema kati ya madaktari 11 wanaosoma kwa vitendo hospitalini hapo, mmoja tu anayesomeshwa na hospitali hiyo, ndiye hajagoma.

Via Gazeti la Mwananchi kusoma zaidi fata hii link Madaktari bingwa nao wagoma

RAY AZINDUA FILAMU YA SOBING SOUND KWA KUTOA MSAADA AKISHIRIKIANA NA STEPS


Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre   kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage
Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre   kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage
Msanii wa Filamu Nchini Visent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps.Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada ya lei kugawa vyakula mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre vilivyotolewa na Kampuni ya Steps wakati wa Uzinduzi wa filamu yao Mpya ya Sobing Sound.

Waziri wa zamani Misri afungwa jela

Waziri wa zamani wa Misri Sahem Fahmi amehukumiwa kifungo cha miaka  kumi na tano gerezani kutokana na kuiuzia Israel gesi asili kwa bei ya chini sana.
Bwana Fahmi amepatikana na hatia ya ubadhirifu wa mali ya umma.
Mfanya-biashara aliyehusishwa kwenye kashfa hiyo Hussein Salem naye amepewa kifungo kama hicho, akiwa mwenyewe hayuko Mahakamani.
 
Waendesha mashitaka wamesema mauzo ya gesi kwa bei nafuu kwa nchi ya Isreal yaliofanywa na serikali ya zamani ya Hosni Mubarak kumeigharimu serikali faida ya mamilioni ya dola.

NMB YAFUNGUA TAWI TEGETA


NMB inaendelea kupanua mtandao wake wa matawi na kusogeza huduma zake karibu na wateja wake. Sasa NMB ipo katika eneo la Tegeta  katika jengo la Kibo Commercial Complex, Tegeta Kibaoni.
NMB ndiyo benki ya kwanza yenyematawi mengi na ATM nyingi zaidi nchini, imekuwa kinara katika ubunifu Tanzania kwa kuanzisha akaunti mpya nyingi na ndiyo benki ya kipekee iliyopo takribani kwa asilimia 95 ya wilaya zote nchini.

Wateja wa Benki ya NMB wakipata huduma katika Teller za benki hiyo iliyopo Tegeta Jengo la Kibo mCommercial Complex Tegeta Kibaoni
NMB ni Full Mzuka.

Italia kupambana na Uhispania katika fainali


Italia na Ujerumani
Ballotelli aliifungia Italia magoli mawili na kuifikisha nchi yake katika fainali ya Euro 2012
Mario Balotelli alifunga magoli mawili ya kupendeza mno na kuiwezesha timu yake ya Italia kuishangaza 
Ujerumani kwa kuifunga magoli 2-1 katika nusu fainali ya Euro 2012, na nafasi ya kucheza mechi ya fainali mjini Kiev dhidi ya Uhispania.

Mabao ya mshambulizi huyo wa klabu ya Manchester City ya England, aliingiza goli la kwanza wavuni kupitia kichwa, na pili kwa mkwaju wa kasi mno katika uwanja wa mjini Warsaw, na Italia kuwathibitishia Wajerumani katika kipindi cha kwanza kwamba ilikuwa na nia kamili ya kufika fainali.
Wajerumani, kufuatia mshituko, walianza kucheza kwa makini zaidi, lakini bao lao la penalti, ambalo lilipatikana katika dakika ya 92, kupitia Mesut Ozil, lilichelewa mno, na halikuweza kuwaokoa.

Italia kamwe hawajawahi kushindwa na Ujerumani katika mashindano makubwa, na wamefanikiwa sasa kucheza mechi nane dhidi ya Ujerumani pasipo kushindwa.
Hii sasa itakuwa mara ya tatu kwa Italia kuingia fainali za michuano hii ya mataifa ya Ulaya, na wataingia fainali kama timu inayodhaniwa kuwa dhaifu ikilinganishwa na mabingwa watetezi Uhispania.
Timu hii ya meneja Cesare Prandelli ilistahili ushindi, kwani sio tu waliweza kupambana na Ujerumani ambayo iliwashinda wapinzani wao kwa urahisi, bali pia walifunga mabao yao mapema katika kipindi cha kwanza.

Timu hiyo ya Azzurri ilikuwa na nafasi ya kujiongezea magoli, lakini ilicheza kwa tahadhari kwa kuhofia kwamba iwapo ingeliongoza mashambulizi zaidi dhidi ya Italia, kulikuwa na uwezekano wa ngome yao kuachwa ikiwa dhaifu, na Wajerumani kuwashambulia.

Tamko la Jumuiya ya Madaktari Tanzania kuhusu tume iliyoundwa na Jeshi la Polisi ili kuchunguza ukatili aliofanyiwa Dkt. Ulimboka Steven

KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA
                                                                                                                                                                                                                
YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012 


Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka, Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.

Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

Imetolewa na Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

Thursday, June 28, 2012

Picha fupi: Rai ya Dkt. Ulimboka Steven leo Alhamisi, Juni 28, 2012

                                             Dkt. Ulimboka Steven leo Alhamisi

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate