Lagos Nigeria WANAMUZIKI maarufu wa Nigeria, Wizkid na Yemi Alade,
walishindwa kunyakua tuzo za Watumbuizaji Bora za Kimataifa baada ya
mwanamuziki wa Ghana, Livingstone Etse Satekla a.k.a Stonebwoy kuwapiga
kikumbo.
Yemi Alade.
Washindani wengine katika kundi hilo walikuwa ni Sarkodie (wa Ghana),
Fally Ipupa (Congo), The Sauti Sol na AKA wote a Afrika Kusini..
Na Kulwa Mwaibale MSIBA!
Mohamed Juma (14) ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Shule
ya Sekondari ya Toangoma wilayani Temeke, Dar amefia bwawani wakati
akiogelea. Tukio hilo lililoacha majonzi kwa ndugu, jamaa, marafiki na wanafunzi wenzake, lilijiri Juni 26, mwaka huu, majira ya alasiri.
Mwanafunzi
wa kidato cha kwanza, Shule ya Sekondari ya Toangoma wilayani Temeke,
Dar, Mohamed Juma (14) amefia bwawani wakati akiogelea.
Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko makubwa ya
kumpoteza mwanaye, baba mzazi, Juma Shaha alisema familia yake imepata
pigo kubwa kwa kuondokewa na mtoto wao wa kiume. “Nashindwa nianzie
wapi kuzungumza maana tumepata pigo kubwa sana kuondokewa na mwanangu wa
kwanza katika uzao wetu wa watoto watatu wa kiume, inauma sana kwa
kweli,” alisema Juma. Juma alisema, majira ya saa 4 asubuhi ya siku
ya tukio, Mohamed aliaga kwenda twisheni na baadaye saa 8 kuelekea 9
alasiri alikwenda kwa rafiki zake Kilakala, Kongowe. “Jambo la kushangaza, hadi inafika saa 2 usiku, Mohamed hakuonekana nyumbani ndipo tulianza kumtafuta,” alisema mzazi huyo.
KUJULIANA
hali ni jambo la muhimu kwa binadamu, niwafahamishe mashoga zangu kuwa
hali yangu na familia ni njema hakuna mushikeri wowote juu ya afya zetu,
mategemeo yangu kuwa nyie pia ni wazima na mambo yenu yanasonga kama
kawaida.
Kabla sijaianza mada ya leo inayosomeka “Si lazima mumeo akuanze
mnapokuwa faragha” niwape pole ndugu zangu ambao mko kwenye mfungo wa
Ramadhani, leo ni siku ya kumi na tatu mkiwa kwenye swaum Mungu awatie
wepesi mmalize salama.
Nikiuliza mjitokeze mashoga ambao mna uwezo wa kuwaanza waume zenu
muwapo faragha ni hakika yangu kuwa wengi wenu mtainamisha vichwa chini
au kuangalia pembeni mkimaanisha ni vigumu sana kuonesha uhitaji kwa
waume wenu.
Deogratius Mongela na Chande Abdallah INASIKITISHA!
Mmiliki wa Shule ya Msingi na Awali (International) ya Mount Zion
iliyopo Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili, 47, (pichani) ameuawa
na mwili wake kutupwa ndani ya shule yake baada ya kupotea kwa zaidi ya
miezi sita huku mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Tatu Ntimizi, Said Ntimizi akidaiwa kuwa mmoja kati ya
watuhumiwa wa mauaji hayo.
Mmiliki
wa Shule ya Msingi na Awali (International) ya Mount Zion iliyopo
Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili enzi wa uhai wake.
Duru za awali za upelelezi wa polisi, zinamtaja Said kuwa alikuwa na
uhusiano wa karibu na marehemu bila kufafanua alihusikaje na mauaji hayo
ya kinyama yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana, siku na tarehe
isiyojulikana na mwili wake kutupwa kwenye shimo la maji taka ndani ya
eneo la shule aliyokuwa akiimiliki. Aidha, nyuma ya taarifa hiyo ya
mauaji, deni la shilingi milioni mia tisa (900,000,000) ambalo mwanamke
huyo alikuwa akimdai mmoja kati ya watuhumiwa hao ambao majina yao yote
bado hayajafahamika likitajwa kuwa ndiyo chanzo cha Annah kutolewa uhai.
ALIANZA KWA KUTOWEKA
Wakisimulia kwa uchungu namna Annah alivyotoweka nyumbani kwake, ndugu
wa marehemu walisema, awali Desemba 26, mwaka jana kwenye Sikukuu ya
Boxing Day, kuna wageni walifika nyumbani kwake, Boko, Dar, wakazungumza
na baadaye wakaondoka naye na hakurudi tena.
Mtoto
wa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tatu
Ntimizi, Said Ntimizi anayedaiwa kuwa mmoja kati ya watuhumiwa wa mauaji
hayo.
NDUGU WAPATA WASIWASI, WATOA TAARIFA POLISI
Ndugu hao walisema kuwa siku za kwanza hawakupata wasiwasi kwa vile
ilikuwa kawaida ya marehemu kuwa mtu wa safari kutokana na biashara zake
na kuongeza kuwa walianza kupata wasiwasi baada ya siku nne kupita huku
kukiwa hakuna mawasiliano kati yao na marehemu, jambo lililowalazimu
kuripoti Kituo cha Polisi cha Wazo Hill ambao walianza uchunguzi.
Genevieve Nnaji
Hili ni jumba la mwigizaji Genevieve Nnaji ambalo alilinunua jijini
Accra, Ghana. Jengo hilo lina thamani ya dola milioni nne (Sh. Bilioni
8.6) likiwa eneo la Achimota. Daniella Okeke Huu ni mjengo unaotisha wa Daniella Okeke ambao una thamani ya mamilioni. Ini Edo
Haya ni makazi ya Ini Edo, mmoja wa nyota maarufu wa filamu nchini
Nigeria ambako anaishi baada ya kuachana na mfanyabiashara Philip
Ehiagwina. Mjengo huo una thamani ya Naira milioni 70 za Nigeria. Mrembo
huyo anaishi humo na wadogo zake. Wasiu Ayinde Haya ni makazi ya mwigizaji Wasiu Ayinde ambaye anamiliki majumba kadhaa jijini Lagos na mji wa nyumbani kwao huko Ijebu.
Mjengo huu unaoitwa ‘Omoojusagbola House’ ulimalizika kujengwa Machi
2012 wakati akiadhimisha mwaka wa 55 tangu kuzaliwa kwake. Ayinde ambaye
anajulikana kama K1 pia ana nyumba jijini Ontario, Canada, ambako mke
na watoto wake wanaishi. Dencia Haya ni makazi ya kuvutia ya mwigizaji
Reprudencia N. Sonkey almaarufu kama Dencia. Mrembo huyo mwenye asili ya
Cameroon na Nigeria, ambaye ni mwimbaji, modo, mjasiriamali na mtoa
misaada kwa maskini, alilionyesha jengo hilo lililoko Los Angeles,
Marekani, ambako anaishi, katika akaunti yake ya Instagram. Inasemekana utajiri wake unakadiriwa kuwa dola milioni 3.1 au Naira milioni 617 za Nigeria. Don Jazzy Haya ni makazi ya Don Jazzy- Mkurugenzi Mkuu na mmiliki wa Mavin Records ambaye pia ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na prodyuza.
Don ni prodyuza tajiri zaidi wa muziki nchini Nigeria na mwanamuziki
anayeshika nafasi ya pili kwa utajiri barani Afrika. Mjengo huu uko eneo
linaloitwa Lekki, ukiwa na thamani ya Naira milioni 160 za Nigeria
ambapo aliununua mwishoni mwa mwaka 2012. Chika Ike
Hapa anaishi mwigizaji mrembo Chika Ike eneo la Lekki tangu mwaka
2013 ambapo alinunua jengo hilo kwa mamilioni ya Naira za Nigeria.
Katika eneo la jumba hilo kuna bustani, eneo la michezo, ofisi, maegesho
ya magari, bwawa la kuogelea na kila aina ya anasa.
Chika Ike ni mmoja wa wanawake matajiri zaidi katika tasnia ya filamu
nchini Nigeria. Mbali na mjengo huo pia ana duka linaloitwa Fancy Nancy
jijini Abuja.
Ofisa wa sanaa kutoka Balaza la sanaa (BASATA)Augustino Kihiyo(kushoto) John Saimon 'Joh Makin'(katikati) pamoja na G-Nako.
Baadhi ya wasanii na wanafunzi wa Chuo Cha Habari cha DSJ wakifuatilia mkutano huo.
...Wakifuatilia mkutano huo.
STAA wa muziki wa Hip Hop Bongo, ambaye pia ni memba wa Kundi la
Weusi kutoka Arusha, John Simon ‘Joh Makini leo amefungukia wasanii
wenzake kukubali kukosolewa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Jukwaa la Sanaa
linalofanyika kila baada ya wiki mbili katika Ukumbi wa Basata-Sharif
Shamba, Ilala jijini Dar es Salaam, Joh amesema kuwa ili kuweza
kupambana changamoto za muziki katika jamii ni lazima kukubali
kukosolewa.
“Tunatakiwaa kutengeneza muziki unaokubalika katika soko kwani msanii
anayetaka kutoka kimuziki lazima ajitambue katika jamii yake,” alisema
Joh Makini anayetamba kwa sasa na Wimbo wa Nusunusu. (PICHA/HABARI: DENIS MTIM/GPL)
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, akitoa maelezo ya kongamano kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kulifungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma ambalo liliandaliwa na taasisi yake.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya akisoma hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo kwa niaba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika hoteli ya St. Gasper mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa salamu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) wakati wa kongamano hilo la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini (TIC), Lilian Mwamdanga akishiriki kuchangia maoni wakati kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama akichangia maoni wakati wa kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na Kamishna Mipango wa Tume ya Mipango Zanzibar, Ahmed Makame Haji wakifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali ya wadau yaliyokuwa yakitolewa kwenye kongamano hilo.
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania bara na visiwani walioshiriki kongamano hilo la siku mbili ambalo liliandaliwa na taasisi ya ESRF.
Muonekano wa nje wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania lililopo ndani ya Karume Hall wanaoshiriki katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya sabasaba yaliyoanza kurindima jana kwenye katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania wapo katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima mapema jana.
UN Tanzania ambao wapo katika banda la Karume ndani ya mabanda hayo ya Sabasaba, kutoa elimu inayolenga kuionyesha jamii mafanikio, changamoto na fursa zilizopo katika Umoja wa Mataifa ambapo mwaka huu unafikisha miaka 70 tangu shirika hilo lianzishwe.
“Huu ni mwaka muhimu sana kwani safari ya Umoja wa Mataifa ilianza mwaka 1945, hadi kufikia sasa kuwa umefikia wapi, tupo wapi na tunaelekea wapi katika kushughulikia changamoto za kidunia ikiwemo Amani na usalama, changamoto za maendeleo, changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, na changamoto zingine”, alieleza Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Aidha, alibainisha kuwa, UN ambayo imeweza kufikisha miaka 15 ya malengo ya Milenia yaliyokubaliwa na nchi wanachama wa Umoja huo mwaka 2000, yanafikia kilele hapo Desemba 30, mwaka huu hivyo wakuu hao wanchi watakutana tena mwezi Septemba mwaka huu, kupanga malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yatakapokubalika yataanza kutumika mwakani.
“Huu ni mwaka muhimu sana. wa kuonyesha hayo mabadiliko, tumekuwa na miaka 15 ya milenia kuna vitu tumefanikiwa na tumekuwa na changamoto. Kwa hiyo malengo hayo yalikuwa ni shirikishi kutoka kwa kada zote”alieleza.
Pia alieleza kuwa katika mkutano mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi ambao utakuwa mkutano mkubwa wa 21, utakaofanyika Paris-Ufaransa Disemba mwaka huu. Wakuu wa nchi watakuja na makubaliano ya kuona watafanya nini hivyo makubaliano hayo ni muhimu sana.
Nchi zote duniani zimeona suala la mabadiliko ya tabianchi si la nadharia tena bali ni la wote kuungana kupambana nalo kwani wote tunaathirika.
Hivyo tunawakaribisha sana watanzania kutembelea katika banda letu kujionea na kufahamu na kujifunza na kwa Tanzania mwaka huu tunamalizia program yetu ya kwanza ambayo tunashirikiana mashirika yote kufanya kazi kwa pamoja (Delivering as one) katika kutatua changamoto zinazotukabili hapa Tanzania kwa kushirikiana na serikali.
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akitoa maelezo ya taarifa mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye jarida la vijana lililoandaliwa na Shirika linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) kwa mmoja wa wakinamama aliyetembelea banda kwa ajili ya kufahamu shughuli mbalimbali na mchango wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa serikali Tanzania.
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisikiliza swali kutoka kwa raia wa kigeni mwenye asili ya asia aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya sabasaba yaliyoanza kurindima jana katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Gladness Mallya na Mayasa Mariwata
MSHTUKO! Wakati wimbi la wasanii Bongo likizidi kuwa kubwa katika
kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye siasa
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, mtabiri maarufu nchini,
Maalim Hassan Yahya Hussein amefunguka mazito juu ya vifo vya mastaa hao
kutikisa upya huku wale watakaosalia wakipata nafasi za uongozi. Staa wa bongo movie Steven Mangele ‘Steve Nyerere’.
TUJIUNGE MAGOMENI-MWEMBECHAI
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Magomeni-Mwembechai jijini
Dar, mapema wiki hii, mtabiri huyo alisema kuwa, mwaka huu kinyota ni wa
mafanikio makubwa kwa wasanii lakini pia vifo navyo vitakuwa vingi
kwao.
Miss tanzania 2006 na muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu.
NI MWAKA WAO KINYOTA
Alisema kwamba, kwa wale watakaosalimika huku wakiwa wamejiingiza kwenye
kinyang’anyiro cha kugombea uongozi wa kisiasa, wote watafanikiwa kwa
kuwa mwaka huu ni wao.
Maalim alisema kuwa, mwaka huu kinyota ni wao ndiyo maana wamejitokeza
wengi kwenye kuwania nafasi hizo tofauti na vipindi vingine vya uchaguzi
vilivyopita.
Saa
zisizopungua 48 baada ya klabu ya Manchester United kuripotiwa kutuma
ofa ya kumsajili beki wa kimataifa wa Spain, Sergio Ramos, klabu yake ya
Real Madrid imepokea ofa hiyo na imetoa uamuzi.
Manchester
United, juzi walituma ofa ya £35million kwa ajili ya kupata saini ya
Ramos na klabu ya Madrid wameipiga chini ofa hiyo.
Mwanamuziki nguli wa dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’.
Gladness Mallya BAADA ya uvumi kuzagaa mtaani kwamba mwanamuziki wa dansi,
Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefariki dunia, Banza amesema amechoshwa
na watu kumuua sana.
Baada ya uvumi huo, ndugu zake wamesema watu waache kumuua kwa maneno kwani bado yupo hai.
‘Banza Stone’ akiwa katika ofisi za Global Publishers (Picha na Maktaba).
Ndungu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Hamis, alisema uzushi wa
kifo cha Banza umewasumbua sana kwani watu mbalimbali walikuwa wakipiga
simu na wengine kufika nyumbani jambo ambalo lilimuumiza sana Banza
japokuwa anaumwa lakini akawa analalamika kwa nini watu wanamuua kwa
maneno na si mara moja kutokea.
“Jamani yupo hai japokuwa anaumwa lakini anaongea tatizo lipo kwenye
kusimama na kula, watu waache uzushi kwani wanamuumiza zaidi kwa uzushi
wao huo,” alisema Hamis.
Mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuh Mziwanda.
Mpenzi msomaji tunakutana tena katika safu hii
ambapo mastaa mbalimbali hujibu maswali kumi kikamilifu, leo tunaye
mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye amefunguka mambo
mengi alipokuwa akizungumza na Mwandishi Wetu IMELDA MTEMA. Ili kujua aliyoyasema endelea kusoma. Ijumaa: Vipi kuhusu sakata lako la nguo kukuvuka ukiwa jukwaani limekuathiri kivipi? Shilole: Halijaniathiri chochote hiyo ni kama mtu anapata ajali akiwa kazini. Ijumaa: Wakati zile picha zilipokuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii, mpenzi wako Nuhu alilizungumziaje hilo? Shilole: Hakuzungumza chochote kwani tulikuwa pamoja siku ya tukio hivyo anajua nini kilitokea. Ijumaa: Najua una wakwe, je, walipoziona hizo picha hawakumsumbua Nuhu na kuona kama unawadhalilisha?
STAA wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Nimempata, Pamela Daffa ‘Pam D’ akifakamia ugali.
STAA wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Nimempata, Pamela
Daffa ‘Pam D’ hivi karibuni aliwaacha watu hoi baada ya kunaswa
akifakamia ugali mkubwa.
Tukio hilo lilitokea katika Pub moja iliyopo Uwanja wa Sanaa,
Legho-Ubungo jijini Dar ambapo ‘wadaku’ waliokuwepo hapo walishangaa
staa huyo kufika eneo hilo na kuagiza ugali mkubwa na nyama kisha kuanza
kuufakamia wote bila kubakiza kitu.
Baadhi ya washiriki wa shindano
hilo wakiwa kwenye pozi la pamoja ndani ya Hoteli ya Colloseum maeneo ya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa mashindano hayo Jacqueline Chuwa (katikati) akizungumza jambo mbele
ya wanahabari waliokuwa Hoteli ya Colloseum Mnazi Mmoja jijini Dar.
Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa mashindano hayo Angerls Faber na Mratibu
wa Shindano hilo Sebu Panya.
Angerls Faber akielezea namna mashindano hayo yatakavyo kuwa.
Mbunge
wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi ametangaza rasmi kutogombea tena
ubunge katika jimbo, katika mkutano wa hadhara ambapo baadhi ya
wanachama wa CCM wameonesha kutokubaliana na uamuzi huo.
Dkt. Emmanuel Nchimbi akihutubia mkutano wa hadhara
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi wakiwemo wanachama wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma,
wamejikuta katika hali ya sintofahamu huku wengine wakimwaga machozi
baada ya mbunge wa jimbo hilo, mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza rasmi
kutogombea tena ubunge katika jimbo hilo.
Wakala
wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, Jamal Kisongo
amesema hatma ya mshambuliaji huyo kucheza soka la kulipwa Ulaya sasa
itasubiri mwakani kutokana na rais na mmiliki wa klabu yake yake TP
Mazembe Moise Katumbi kuonesha bado anahitaji huduma yamchezaji huyo
hususan katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika.
“Katumbi ameonesha bado anahitaji
kumtumia katika kikosi chake kwenye michuano ya champions league kwa
maana hiyo makusudio yetu na matarajio yetu, kunatimu moja kubwa ilitaka
kumsaini kwa ‘Euro’ milioni moja lakini bahati mbaya Katumbi alitaka
amuache baada ya champions league kuisha”, amesema wakala huyo wa
Samatta.
Brighton Masalu KUJISHUSHA! Staa wa filamu Bongo, William Mtitu amesema yupo
tayari kumaliza ugomvi na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kutokana na
shinikizo kutoka kwa wasanii wenzake, wadau na mkewe.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kikao kizito kikimhusisha Mtitu na
wasanii nguli kiliitishwa na kumuonya juu ya suala hilo kabla ya
kukubali kuwa yuko tayari kumalizana na Steve.
Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Kilikuwa ni kikao kizito kaka, Mtitu ‘alipewa vipande’ vyake huku
wasanii wakimpa hasara za mabifu yasiyokuwa na faida na yeye alielewa,
na sasa yuko tayari kwa suluhu,” alisema mmoja wa wasanii mwenye jina
kubwa.
Mwandishi wetu alimtafuta Mtitu ili kusikia chochote kutoka kwake ambapo alisema;
“Duh! Umeipata na hiyo! Ni kweli kabisa, hakuna haja ya kuwa na
mabifu katika zama hizi za maisha mafupi, wakiandaa mpango wa
kutukutanisha, niko tayari.”
Kwa upande wake, Steve Nyerere alisema asingeweza kulizungumzia suala
hilo kwa wakati huo kwani alikuwa na kazi anaifanya. Aliahidi kumtafuta
mwandishi baadaye, lakini hadi Risasi Mchanganyiko linakwenda
mitamboni, alikuwa hajawasiliana naye.
Miss
Tanzania 2006 na Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akipokea maelekezo
kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Bw. Alluu Ismaili Segamba
kwenye Mkutano uliofanyika Mkoani Singida wiki iliyopita.
Gladness Mallya BARAKA! Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri
kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea
ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka
mrembo huyo kwa uamuzi wake huo.
…Wema akipokelewa na Makada wa Chama cha Mapinduzi, CCM mkoani Singida.
Akistorisha na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule
ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti
maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.
“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza
ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM
mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu
barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza
kugombea,” alisema Nape.
Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama
hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki
kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka
2010.
Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha
ya Wema ni Ndumbagwe Misayo ëTheaí (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara
Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini).