EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, April 30, 2015

KINONDONI TALENT SEARCH, KAJALA NA MC PILIPILI WAFUNGUKA

MJAMZITO AJIFUNGUA NAZI! ASIMULIA MKASA MZIMA, INATISHA

Maajabu! Msichana aliyefahamika kwa jina la Dora mkazi wa Magomeni Bagamoyo mkoani Pwani, hivi karibuni amejikuta akijifungua nazi badala ya mtoto, jambo lililomshangaza kila mtu.
Ushirikina watajwa

Dora anayedaiwa kujifungua nazi.
Ilidaiwa kuwa, chanzo cha Dora kujifungua nazi ni maneno aliyoambiwa na mke mwenzake aliyefahamika kwa jina la Jamila ambapo aliambiwa hatajifungua kiumbe cha kawaida na ndipo alipokimbilia Dodoma kukwepa matatizo.
Msikie Dora

Akizungumza na Amani hivi karibuni akiwa nyumbani kwake Bagamoyo, Dora alisema:
“Nilihamia Bagamoyo nikitokea Mwanza, nikakutana na mwanaume anayeitwa Pascal, tukakubaliana tuishi kama mke na mume.

“Baada ya kukubaliana hilo, nikapata ujauzito lakini nikashangaa siku moja akaja mwanamke na kusema yeye ni mzazi mwenzake na Pascal.“Alifanya vurugu, akanijeruhi kisha akachukua TV na vitu vingine, akaondoka huku akiniambia lazima nijifungue kiumbe cha ajabu. Nilipata hofu kubwa, mara nikaanza kusumbuliwa na tumbo, nikapelekwa kwa mganga ambapo niliambiwa nimerogwa.

KAJALA APEWA SIKU 5 ZA KUISHI

MASIKINI! Staa mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni amejikuta akiwa katika wakati mgumu na wa hatari kufuatia watu wasiojulikana kuvamia nyumbani kwake na kutoa onyo kwamba wanampa siku tano tu za kuishi, Amani lina mkasa kamili.Ishu hiyo ya kushtusha ilitokea usiku wa saa nane ya kuamkia juzi, Jumanne nyumbani kwa staa huyo, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Staa mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja.
WALIKUWA KWENYE TOYOTA RAV 4
Kwa mujibu wa chanzo chetu, watu hao wapatao watatu walitinga nyumbani hapo usiku huo mnene huku wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Rav 4 milango mitano rangi ya bluu ya kuiva na kumkuta mlinzi getini ambaye yupo kwa ajili ya kulinda usalama wa msanii huyo mwenye maadui kila kukicha.“Walikuwa watano, walikuwa kwenye Rav 4 milango mitano, rangi ya blue ya kuiva. Wakamkuta mlinzi, walimuuliza kama Kajala yupo, mlinzi aliwadanganya kwamba hayupo.”

CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND KWA MARA YA TATU AFRIKA MASHARIKI

 Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya Alliance Insurance.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi Fauzia Kullane.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe
KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.

 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.

Utafiti huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini  Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.

Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000 zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.

Wednesday, April 29, 2015

Indonesia: watu 8 waliohukumiwa adhabu ya kifo wauawa

Makati, Ufilipino, maandamano ya kuunga mkono Mary Jane Veloso ambaye ameponea kuuawa baada ya adhabu yake kuahirishwa Jumanne Aprili 28 mwaka 2015.
Makati, Ufilipino, maandamano ya kuunga mkono Mary Jane Veloso ambaye ameponea kuuawa baada ya adhabu yake kuahirishwa Jumanne Aprili 28 mwaka 2015.
REUTERS/Erik De Castro

Nchini Indonesia, watu wanane waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya wameuawa Jumanne usiku wiki hii kwa kupigwa risasi.

Raia saba wa kigeni ikiwa ni pamoja na raia wawili kutoka Austalia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria na raia mmoja wa Gabon ni miongoni mwa waliouawa. Raia mmoja kutoka Ufilipino ambaye ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu ya kifo amenusurika na adhabu hiyo katika dakika za mwisho.
Kama walivyotangaza, viongozi wa Indonesia wametekeleza adhabu hiyo ya kifo usiku wa manane Jumanne wiki hii. Raia hao ikiwa ni pamoja na raia wawili wa Australia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria, raia mmoja wa Ghana na raia mmoja wa Indonesia wameuawa kwa kupigwa risasi katika jela la kisiwa kiliyo mbali cha Nusakambangan.
Pamoja na shinikizo mbalimbali za kimataifa na maombi kutoka kwa ndugu na jamaa za watu hao waliokua wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa ajili ya msamaha, Jakarta ilibakia na msimamo wake mpaka mwisho. Rais Joko Widodo, ambaye aliingia madarakani katika majira ya joto kufuatia sehemu ya kampeni yake ya kupambana na madawa ya kulevya, ambapo alisema kutowasamehe watu watanojihusisha na madawa hayo ya kulevya. Utekelezaji wa adhabu kwa watu hao waliohukumiwa ulikuwa unatarajiwa.

NCCR-Mageuzi yadaiwa kuwasilisha hoja ya kujitoa UKAWA; CUF watoa masharti magumu!

Kikao cha viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimeshindwa kuendelea baada ya baadhi ya wajumbe kushindwa kuafikiana kuhusu hoja iliyowasilishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi, ya kutaka kujitoa kwenye umoja huo, imefahamika.

Viongozi hao walikutana jijini Dar es Salaam jana katika Ofisi Kuu ya Chama cha Wananchi (CUF), ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa wakijadili hatima ya kuachiana majimbo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Katika kikao hicho ambacho kilitarajiwa kuanza saa 4 asubuhi kama ilivyokuwa imepangwa na badala yake kilianza saa 6 mchana, ajenda kuu zilikuwa ni kujadili namna ya kuachiana majimbo ambayo bado mwafaka haujapatikana pamoja na utaratibu wa kumpata mgombea urais kupitia Ukawa.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kilichokuwa chini ya Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, kilishindwa kutoa mwelekeo wa majimbo 18 yenye mvutano huku kila chama kikitaka kugombea kivyake.

Hata hivyo hoja hiyo iliibua mvutano mkali baina ya wajumbe wa kikao hicho ambapo kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ujumbe wake uliongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu.
Kwa upande wa CUF, ujumbe wake uliongozwa na Profesa Lipumba, Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya na Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shaweji Mketo.

NCCR-Mageuzi kiliongozwa na Mwenyekiti wake James Mbatia ambaye baada ya kuwasilishwa hoja ya chama chake alishindwa kuendelea na kikao na kulazimika kutoka nje ya ukumbi wa mikutano.

Shamsa Ford:Mnikome Kuanzia Leo Naishi Nitakavyo Mimi na Kufanya Kile Ambacho Nahic Kinafaida Kwangu

Ustaa kazi: Baada ya kuchoshwa na maneno ya watu kuhusu maisha yake binafsi, staa mrembo wa Bongo Movies, Shamsa Ford ameamua kuweka wazi msimamo wake kwa mashabiki zake wote.

Siku zote nimekuwa muoga kuishi maisha yangu kwa kuogopa watu but hao watu naowaogopa hata siku moja hawajawahi kuogopa kuishi maisha yao kwa kuniogopa mm..from today nitaishi nitakavyo mimi na kufanya kile ambacho nahic kinafaida na kunifurahisha katika maisha yangu.Mashabiki wangu wa ukweli kabisaa alionipangia Mungu hata niweje hawawezi Kunitoka na nitaendelea kuwapenda na kuwaheshimu kila siku..I love my family….” –Shamsa ameandika hayo leo kwenye ukurasa wake mtandaoni.

Monday, April 27, 2015

KIPA WA SIMBA MANYIKA JR NDIYE MCHEZAJI PEKEE EAST AFRIKA MWENYE MCHUCHU MZURI KULIKO WOTE

 
 

DIAMOND PLATINUMS AKIBUSU MIMBA YA ZARI


Diamond Platinums akibusu Tumbo la Mpenzi wake Zari the big Boss Lady jana zanzibar walipokuwa Mapumzikoni mara baada ya Diamond Jana usiku kuangusha Bonge la Show bab kubwa Katika viwanja vya Ngome Konge Zanzubar.
Zari ambaye ni Mjamzito wamwkuwa wakitenda Vyombo vya habari Pamoja na Mitandao ya Kijamii kutokana na Uhusiano wao,Katika Mitandao ya Kijamii kwa sasa Ni Nadra sana Kupita siku mbili bila uhusiano

Staa wa rnb mwenye mpango wa kupunguza makalio yake,Picha,sababu, viko hapa



kmichelle-780x520
Wakati wanawake wengi wanafanya upasuaji kuongeza ukubwa wa makalio yao, msanii wa rnb K. Michelle amesema anampango wa kupunguza makalio yake.
K Michelle aliwahi kukiri kuongeza makalio yake amemjibu shabiki twitter kuwa anapunguza makalio yake iliaweze kuigiza kwenye filamu mpya anayocheza.
Good for you! I’m about to decrease mine for a movie,”
k 4

Tambwe awatupia dongo Simba SC

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, ameitupia dongo kiaina timu yake ya zamani ya Simba akisema anashukuru kwa kuwa yupo Yanga ambako ana nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara lakini kama angeendelea kukaa Msimbazi, asingepata nafasi hiyo.
 

Msimu uliopita, Tambwe alikuwa Simba na kuibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao 19 lakini alishindwa kupata ubingwa huo, baada ya timu yake kushika nafasi ya nne. Yanga sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 52 na kama leo itafanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Polisi Moro kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, itakuwa tayari imeubeba ubingwa huo unaoshikiliwa na Azam FC. 

Akizungumzia kuchukua ubingwa wa kwanza wa ligi kuu, Tambwe ameliambia Championi Jumatatu kuwa, atafurahia kuchukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza akiwa na Yanga baada ya kushindwa kufanya hivyo akiwa Simba, ingawa alidumu klabuni hapo kwa muda mrefu.

Simba yapiga mabao saba bila straika

KLABU ya Simba sasa imeamka na kuisogelea nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, lakini habari ni kuwa imeshinda mabao saba katika michezo miwili mfululizo bila ya kuwa na ‘orijino’ straika katika kikosi chake.
Simba sasa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 41, huku Yanga wakiendelea kutesa kileleni na pointi 52 wakifuatiwa na Azam FC wenye 45.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jumatano iliyopita, Simba ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Mgambo JKT kabla ya juzi Jumamosi kuifunga Ndanda FC mabao 3-0, michezo yote ikipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Katika michezo hiyo, kuanzia namba sita mpaka 11 Simba iliwatumia viungo wakabaji na viungo washambuliaji, lakini bado ilifanikiwa kuwatesa wapinzani wake, tena kwa idadi kubwa ya mabao. Simba iliwatumia Said Ndemla, Jonas Mkude, Awadh Juma, Emmanuel Okwi, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Ibrahim Ajibu ambao kiuhalisia hakuna hata mmoja ambaye ni mshambuliaji wa kati.
Okwi na Ajibu walikuwa wakibadilishana nafasi ya kucheza ‘sentro straika’ kulingana na mazingira ya mchezo husika yalivyokuwa, ambapo wachezaji hao wote wana uwezo wa kucheza nafasi hizo wakiwa uwanjani. Mabao hayo saba katika michezo hiyo miwili yalifungwa na Okwi aliyetupia matatu, Singano alifunga mawili, huku Mkude na Ndemla kila mmoja akifunga bao moja.
Wachezaji wa Simba ambao ni orijino straika ni Elias Maguri na Mganda Dan Sserunkuma ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi hicho kinachonolewa na Mserbia, Goran Kopunovic ambaye amejiunga na kikosi hicho siku 117 zilizopita.

WEMA: MAMA’NGU AMEPOTEZA UWEZO WA KUONA KWA 75%!

Pole sana mama! Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa mama yake mzazi, Miriam Sepetu anasumbuliwa na macho ambapo madaktari wamegundua kwamba amepoteza uwezo wa kuona kwa asilimia sabini na tano (75%).
Kwa mujibu wa Wema, aliamua kumpeleka mzazi wake huyo hospitalini (hakuitaja) ndipo alipohakikishiwa tatizo hilo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
“Kumnusuru mama yangu asipate upofu wa moja kwa moja inabidi afanyiwe operesheni ya macho,” alisema Wema kwa huzuni kwa kuwa hakuna kama mama.

KAZI IPO!!! MASTAA WANAOONGOZA KUTUKANA\KUTUKANWA MTANDAONI


Imekuwa ikielezwa kuwa wasanii ni kioo cha jamii. Kwa maana hiyo wanatakiwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na wale wanaowatazama. Hata hivyo, maisha wanayoishi baadhi ya wasanii hayaakisi msemo huo.
Wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo mbalimbali zinazowafanya wasiwe na vigezo vya kuitwa kioo cha jamii.
Miongoni mwa mambo yanayowafanya wakati mwingine wadharaulike ni kutoa maneno machafu, ‘live’ au kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
Katika makala haya nitawazungumzia mastaa wanaoongoza kwa kutukana mitandaoni lakini pia wale ambao wanaongoza kwa kutukanwa katika siku za hivi karibuni.
Wastara Juma
Huyu Wastara amekuwa akiheshimika kwenye jamii kwa muda mrefu na alikuwa ni miongoni mwa mastaa wa kike ambao wangesimama na kuamua jambo wangesikilizwa kutokana na jinsi alivyokuwa amejiweka na kuwaaminisha watu.

Saturday, April 25, 2015

TUME YA TAIFA YASEMA KURA YA MAONI HAITAPIGWA SAMBAMBA NA UCHAGUZI MKUU 2015

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
TUME ya uchaguzi nchini Tanzania (NEC), imetoa ufafanuzi juu ya suala la upigaji wa kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa kuchanganywa na uchaguzi mkuu na kusema kuwa mambo hayo hayatafanyika kwa pamoja.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa mpaka sasa tume haijaamua ni lini kura ya maoni itafanyika ila kwa sasa wanachofanya ni kuendelea na uandikishaji wa Daftari la mpiga kura katika Mikoa iliyobaki.

Jaji Lubuva ameongeza kuwa uchaguzi mkuu wa rais utakuwepo kama kama ulivyopangwa kuwa katika juma la mwisho la mwezi octoboa ambapo tayari uandikishaji wa Daftari la mpiga kura kwa mfumo wa BVR, utakua umekamilika.
Mwenyekiti huyo amesema kuna upotoshaji unaofanywa na baadhi ya vyama vya siasa kwamba tume imesema itachanganya upigaji wa kura ya maoni na uchuguzi mkuu na kusema kuwa suala hilo halina ukweli wowote.

Lubuva amesema kuwa hakuna sheria inayokataza kuchanganywa kwa zoezi hilo kwa wakati mmoja lakini amesema kufanya hivyo kuna changamto nyingi ambazo zitaweza kuharibu chaguzi hizo ikiwa ni pamoja na jinsi ya kufanya kampeni.
Aidha jaji lubuva amekanusha tuhuma za kwamba tume hiyo imeanza uandikishaji katika mikoa ambayo ni ngome ya chama Tawala ili kuhujumu vyama vya upinzani na kusema tuhuma hizo si za kweli na ni upotoshaji na kusema kuwa tume inafanya kazi kwa misingi na taratibu ilizojipangia.

Ameongeza kuwa kwa kuanza mikoa ambayo yamechagua kwa ajili ya zoezi hilo kunatokana na idadi ya watu katika mikoa hiyo kuwa ndogo hivyo na kutokana na vifaa vya kujiandikishia kuwa vichache ndio maana wakaanzia mkoa wa Njombe na sasa wataendelea na mikoa mingine ya Iringa, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Hatua hiyo inafuatia kutokana na shutuma za vyama vya siasa ikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambapo naibu Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zanzibar Salumu Mwalim, amesema kuwa tume ya taifa Uchaguzi (NEC) isije ikathubutu kuuchezea uchaguzi mkuu kwa kuuchanganya na kura ya maoni ya Katiba Pendekezwa wakithubutu hawata shiriki uchaguzi mkuu Oktoba.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Njombe Mwalimu amesema kuwa chama hicho hakita shiriki uchaguzi mkuu kama kutatokea uchaguzi mkuu kuchanganywa na kura ya maoni ya Katiba Pendekezwa.

Amesema kuwa kitu hicho kitavunja historia ya nchi na dunia kwani hakijawahi kutokea ulimwenguni pote na kuwa itakuwa ni Tanzania pekee kupiga kura mbili tofauti kwa wakati mmoja.

Pengo aonya kuhusu urais, ashtushwa na wanaotumia fedha

Dar es Salaam.
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ambaye alizua kizaazaa bada ya kutofautiana na maaskofu wenzake kuhusu Kura ya Maoni, jana alizungumzia suala la urais, akivitaka vyama vya siasa kuwaengua makada wake wanaotumia fedha kusaka urais.

Kardinali Pengo alisababisha mkanganyiko wakati alipotofautiana na tamko la Jukwaa la Wakristo lililotaka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa, kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura na siku ya Kura ya Maoni, wapige kura ya hapana kukataa mabadiliko hayo ya Katiba.
Tamko hilo lililotolewa na maaskofu wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, lilieleza sababu kadhaa za kupingana na mchakato wa kuandika Katiba Mpya, hasa suala la Serikali kuahidi kuingiza Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba kwa lengo la kutaka Waislamu waipitishe Katiba Inayopendekezwa.

Lakini Kardinali Pengo akakosoa tamko hilo akisema waumini hawana budi kuachiwa kufanya uamuzi wao bila ya kushurutishwa, kauli ambayo ilisababishwa akosolewa na wengi, akiwamo Askofu Josephat Gwajima ambaye amefunguliwa mashtaka ya kumdhalilisha kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.
Jana, Pardinali Pengo alizungumzia masuala ya kisiasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya saba ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph (SJUIT) ambako alionya dhidi ya matumizi ya fedha.
Akionya juu ya matumizi ya fedha katika harakati za kuingia Ikulu, Kardinali Pengo alisema kwa mujibu wa imani na kanuni za dini, uongozi ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu na 
“Kama wapo watu wanaotumia fedha kutaka kuingia Ikulu, ni bora wakaachwa mara moja na vyama vyao. Hata wasipitishwe na kuja kuomba kura kwetu. Ni vyema wakatambua kuwa uongozi haununuliwi,” alisema Pengo.
Alifafanua kuwa rushwa ni kitu kibaya kama itatumika kupata kiongozi katika ngazi yoyote ile na kwamba endapo mtoaji atapewa nafasi aitakayo, bila shaka gharama alizozitumia atataka zilipwe na wananchi anaowatumikia.
“Rushwa ni kitu ambacho kila kiongozi anapaswa kukiepuka ili kuwaondolea wananchi uwezekano wa kuingia katika mchakato wa kulipa deni ambalo kiongozi atataka alipwe (akiwa Ikulu) ingawa alitoa kwa hiari yake wakati wa kujinadi na kuwawishi wapigakura,” alisema. “Ni bora tumchague Rais maskini ambaye hatakuwa na madeni binafsi ya kuyalipa na kwa pamoja tuelekeze nguvu zetu katika ujenzi wa uchumi wa Taifa kwa ujumla. Watoa rushwa mwisho wa siku watataka tulipe gharama walizotumia kutushawishi,” alisema kiongozi huyo wa kiroho nchini.
Pamoja na hayo yote, Askofu Pengo alisema ni lazima ushindani uwepo kuanzia ndani ya vyama kabla havijapata mwakilishi atakayesimama kuviwakilisha mbele wa wananchi ili wachague anayefaa zaidi kulitumikia Taifa.
Alisema ni vyema demokrasia ikaanzia huko kabla haijahubiriwa nje kwani hilo huonekana kabla hata vyama hivyo havijasema namna vinavyojiendesha.
Askofu huyo ametoa kauli hiyo wakati Taifa likiwa kwenye mjadala kuhusu sifa za wagombea urais, huku kukiwa na malalamiko mengi, hasa kutoka chama tawala cha CCM, dhidi ya makada wanaotuhumiwa kutumia fedha kushawishi wanachama wao wawapitishe kuwania urais.

CCM, ambayo mgombea wake ndiye amekuwa akishinda urais tangu siasa za ushindani wa vyama ziliporejeshwa mwaka 1992, imekuwa ikieleza mara kwa mara kuwa makada hao hawatavumiliwa na vikao vya uamuzi vitawaondoa katika mbio za kuwania kuteuliwa kugombea urais.
Mapema wiki hii, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula aliwaambia viongozi wa chama hicho mkoani Dar es Salaam kuwa fedha zinazotumiwa na makada kununua wanachama “kama maandazi”, zitakuwa kitanzi chao kwenye Uchaguzi Mkuu, akisisitiza kuwa wanachama hao watang’olewa.
Hata hivyo, chama hicho kimekuwa hakiripoti vitendo hivyo kwenye vyombo vilivyoundwa kwa ajili ya kuzuia na kupambana na rushwa na juzi, Takukuru ilisema chama hicho kikitoa ushirikiano, itaweza kukomesha uovu huo.
Akizungumzia demokrasia ndani ya vyama, Kardinali Pengo alitaka wagombea wengi zaidi kujitokeza ili kuwapa wananchi wigo mpana wa kuteua mtu anayefaa.
“Wajitokeze wengi zaidi ndani ya vyama vyao. Endapo vyama hivi vitadhihirisha demokrasia baina ya wanachama wao, ni dhahiri itakuwa sifa ya ziada kwa wananchi ambao ndiyo wapigakura wenye uamuzi wa mwisho,” alisema Kardinali Pengo.
Afya yake
Kwa muda wote wa sherehe hizo, Kardinali Pengo alikuwa ameketi kutokana na afya yake kutokuwa nzuri ikiwa ni muda mfupi tangu atoke India kwa matibabu ya mgongo na alitumia fursa hiyo kuwatoa hofu wote kuhusu hali yake.
Alisema kuwa maradhi hayo yalianza tangu mwaka 2013 na baada ya kwenda Ujerumani alibainika kuwa na tatizo hilo ambalo baadaye alishauriwa akatibiwe Hospitali ya Manipal iliyopo Bangalore, India.
“Ninaendelea vizuri. Maumivu yamepungua kwa kiasi kikubwa. Naomba wote wanaonitakia mema wasiwe na wasiwasi kwani matibabu niliyopata yalikuwa mazuri na yenye msaada mkubwa kwangu,” alisema kiongozi huyo ambaye anatembelea mkongojo.
CHANZO; MWANANCHI

WEMA ADAIWA KUTIBUA NDOA YA PETIT MAN

MUSA MATEJA NA IMELDA MTEMA
Hatimaye lile sekeseke la ndoa ya meneja wa wasanii wa Bongo Fleva wanaosimamiwa na Kampuni ya Endless Fame, Petit Man na mdogo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz limemdondokea Wema Isaac Sepetu anayedaiwa kuitibua kiasi cha kuwatenganisha na kila mmoja kuchukua hamsini zake.
Mdogo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz.
Habari kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, Wema amehusika kwa asilimia kubwa kutibua ndoa hiyo kwani amekuwa akimtafutia mademu Petit Man, jambo ambalo Esma alilishtukia na kuamua kumbwatukia Wema kwa kuandika maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.

NAY WA MITEGO, SHAMSA MKE NA MUME!

Musa Mateja
Mara baada ya kuelezwa kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana ‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.
Mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’ wakizungumza jambo.
Baada ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili  liliwadamkia nyumbani kwa Nay maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.
Habari zilizopatikana zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto.
...Wakipozi kimahaba.

Friday, April 24, 2015

JACK: WAUME ZA WATU WATATUUA

Staa aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus, Jacqueline Dustan amefunguka kuwa mastaa wamepachikwa nembo ya kuwa ni vinara wa kubeba waume za watu jambo ambalo linawapa sifa mbaya.
Staa aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus, Jacqueline Dustan.
Akizungumzia mwenendo wa mastaa wengi kuhusishwa na skendo ya kutembea na waume za watu, Jack alisema:
“Yaani sisi mastaa tumepachikwa nembo ya kupora waume za watu. Imefika wakati hata kama umempata mpenzi wako mtu anakuuliza umempora nani. Huwa inaniuma sana.“Kimsingi tuna sifa mbaya na tusipobadilika waume za watu hawa watatuua.”

DIAMOND PLATNUMZ UK CONCERT TOUR TICKETS NOW ON SALE!!!!!‏


diamond_platinumz-slider-2ZURII HOUSE OF BEAUTY AND BONGO DEEJAYS PRESENT!!
Londons Rugby 7's After Party, Appearing Live, Bongo Flava recording artist from Tanzania most famous for his song "Number One". Diamond Platnumz will be preforming with his WCB dancers and special guests at the Royal Regency Banquet Hall for one night only.
THE ROYAL REGENCY
501 HIGH STREET NORTH
MANOR PARK 
For Front Row V.I.P Tables and Info Please Contact our Ticket Hotline: 07853482158 or 07421167123
Dont be left out, tickets are running out quickly. We are counting down to the most Epic event of the Year!!

IN SUPPORT OF ALBINO CRUELTY IN TANZANIA. TOGETHER WE SAY: "IMETOSHA"

Follow the link below or clck "Buy Tickets" to get your tickets A.S.A.P

http://buytickets.at/zurii-house-of-beauty-and-bongo-deejays/26052


Buy tickets for Diamonds are forever UK live concert

MAMA KANUMBA, MAMA LULU KIMENUKA!

Mwandishi wetu
Taarifa zilizotua kwenye dawati la gazeti hili zinadai kuwa, wale wamama wa mjini ambao walikuwa mashosti hadi kufikia hatua ya kusema ni kama ndugu, mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, sasa kimenuka!
Mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.
DALILI KUWA PAKA NA CHUI
Chanzo chetu cha kuaminika kilidai kuwa, dalili za wawili hao kuelekea kugeuka kuwa paka na chui zilianza muda mrefu lakini hali ikazidi kuwa mbaya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Kanumba, Aprili 7, mwaka huu alipokuwa akitimiza miaka mitatu kaburini.
CHANZO NI LULU
Ubuyu ulidai kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kunumba, Mama Kanumba alimtuhumu Lulu kutotoa ushirikiano na kufikia hatua ya kutoa maneno makali zaidi yaliyomkera mama Lulu.

Mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
MAMA KANUMBA NA SMS MBAYA KWA MAMA LULU
Ilidaiwa kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kanumba, mama Kanumba alimtumia mama lulu sms mbaya ya kejeli (kuiandika hapa siyo busara) ndipo mama Lulu ‘alipofyumu’ na kuona kwa hali hiyo bora kama mbwai na iwe mbwai.“Ile sms mama Kanumba alimtumia mama Lulu siku ile (Aprili 7) majira ya saa 11:00 alfajiri.

RAY, BASTOLA UKIIFANYA SHOO, ITAKUTOA SHOO!



Muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’.
INGAWA bado anaonekana kijana mdogo kiumri, tofauti na unavyoweza kumchukulia mtu kama Amri Athuman ‘King Majuto’, lakini katika uigizaji wa filamu, Vicent Kigosi maarufu kama Ray, ni mmoja wa wacheza filamu wakongwe hapa nchini.
Hii ni kwa sababu wao ndiyo vijana wa mwanzo mwanzo kujiingiza katika sinema za kizazi kipya, pale filamu ya Girl Friend ilipofungua pazia mwanzoni mwa miaka ya 2000, kwani kabla ya hapo, tulizoea michezo ya maigizo katika runinga na redio, heshima kwao King Majuto, Mzee Small, Bi Chau, Mzee Jangala na wenzao.
Ninamfahamu kidogo Ray, tangu wakati ule akiwa na Kaole na wenzake wakifanya tamthiliya zilizorushwa na Kituo cha ITV. Hii siyo mara yangu ya kwanza kumzungumzia hapa, kwa maana hiyo, sina maneno mengi yanayoongelea kuhusu yeye ana umahiri gani hasa kwa sababu mashabiki wa tasnia ya filamu watakuwa wanamfahamu vyema.
Ni vigumu kumkuta shabiki wa filamu za Kibongo akiwa hana CD ya Ray, ingawa pia wanaweza kuwa wapo ambao hawathamini mchango wake katika game. Kwa sisi tunaofahamu kidogo, ni jambo lisilowezekana kuizungumzia tasnia hii bila kuliweka mbele jina la Vicent Kigosi.

Thursday, April 23, 2015

DOKTA AMZUIA AUNT KUJIFUNGUA MAREKANI

DOKTA amempiga stop staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel kwenda kujifungulia nchini Marekani kwa sababu hali yake ya ujauzito aliyofikia haruhusiwi kusafiri kwa kutumia usafiri wa anga kwenda popote.
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Chanzo makini kilisema kuwa, Aunt alijiwekea mpango wa kwenda kujifungulia nchini huko kwa muda mrefu lakini alikuwa akisubiri mimba ikue kidogo kitendo ambacho hakikutakiwa kwa kuwa ujauzito umekuwa mkubwa na kusafiri kungemletea tatizo la presha ya kushuka.
  “Imebidi nikubaliane na daktari alivyosema kwa kuwa wao wanajua hivyo siwezi kupingana nao naogopa nisije kupata matatizo, bora nijifungulie hapahapa nyumbani na nimelikubali hilo na mawazo ya nyuma nimefuta japokuwa nilikuwa nimeandaa kila kitu kwa safari hiyo,” alisema Aunt alipopigiwa simu.
Awali Aunt alipanga kwenda kujifungulia nchini Afrika Kusini lakini baadaye aliahirisha baada ya kupata shavu kwa marafiki zake waishio nchini Marekani waliomtaka kwenda kujifungulia huko na kukaa kwa miezi mitatu.

BASATA WAMPONGEZA MAYUNGA KWA KUWAKILISHA VYEMA TANZANIA‏


Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (kulia)akipokea tuzo aliyoipata Nalimi Mayunga mara baada ya kuibuka  mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Afrika.  Shughuli hii imefanyika jana katika halfa ya kumpongeza  Mayunga kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars iliyofanyika  katika ofisi za BASATA. Akishuhudia  kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (Katikati) akiongea katika halfa ya kumpongeza mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo na kuiwakilisha vyema Tanzania . halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za BASATA Ilala Dar es Saalam. kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
Baraza la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .
Mwisho mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya  na kumtakia kila  laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Star wa Afrika
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua katika halfa fupi ya pongezi kwa Nalimi Mayunga katika ofisi za BASATA alisema”  Ushindi huu ni  furaha kubwa kwetu sisi Baraza la Sanaa la Tanzania kwani tunayo dhamana ya kuhakikisha tunaendeleza sanaa nchini  kwa tunashirikiana na wadau mbalimbali nchini katika kuwawezesha   vijana wenye vipaji kukuza sanaa zao ndani na nje ya nchi.
Nachukua fulsa hii kwa niaba ya BASATA kumpongeza Mwakilishi wetu Nalimi Mayunga kwa kufanya vizuri na kushinda mashindano haya. 
Nawashukuru sana Airtel kwa kufata taratibu stahiki na kushirikisha BASATA tangu mashindano haya yaanze ikiwa ni kusajili  kampuni yao na kupata hati ya kufanya shughuli za sanaa na pia kutushirikisha katika mchakato mzima wa mashindano haya na kumleta mshindi huyu kuchukua hati maalumu ya kusafiri na kuagwa rasmi wakati wa kuondoka kwenda kwenye mashindano ya Afrika.  Kwakweli huu ni mfano wa kuigwa na wadau wengi na wasanii kwa ujumla, kufata taratibu na kupata vibali maalumu pindi wanapoenda nje ya nchi kufanya shughuli za sanaa na kuwakilsisha nchi yetu.
Natoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi pindi awamu ya msimu wa pili wa mashindano haya ya Airtel Trace yatakapotangazwa ili nao waweze kupata nafasi ya kushiriki na kuinua vipaji vyao. Aliongea Shalua
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw Jackson Mmbando alisema  Tunawashukuru watanzania wote walioshiriki katika shindano hili  tangu tulipolizindua.  tunampongeza sana mayunga kwa ushindi huu. Nalimi Mayunga ameweza kujishindia dili la kwenda marekani na kupata mafunzo chini ya usimamizi wa Akon,na pia kuweza kurekodi wimbo na video yake ya kwanza vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekai 500,000/= Tunategemea baada ya mafunzo hayo na kutoa wimbo wake na Akon basi mayunga ataendelea kufanya vizuri na hatimae kuweza kuzifikia ndoto zake.
Airtel ilimkabithi Mayunga zawadi ya shilingi million 50 za kitanzania kufatia ushindi wake hapa nchini  na sasa anajiandaa kwenda marekani na kufanya kazi na msaani nguli Akon.
Akiongelea ushindi wake Mayunga alisema, nawashukuru sana watanzania kwa kunipigia kura toka mashindano haya yaanze, najisikia furaha kupata nafasi hii ya pekee na naamini safari yangu nchini marekani itakuwa ya mafanikio makubwa na mwanzo wa mafanikio katika kuzifika ndoto zangu za kuwa mwanamuziki nyota ndani na nje ya nchi.
Nawashukuru Airtel  kwa kuanzisha mashindano haya na BASATA kwa kunipa ushirikiano wakati wote wa mashindano. Natoa wito kwa watanzania na vijana wenzangu kuchangamkia fulsa hii pindi msimu wa pili wa mashindano haya yatakapotangazwa na kuanza .
Mashindano ya Afrika yalimalizika  kwa mtanzania kushika nafasi ya kwanza , Nigeria nafasi ya pili  na Congo Brazavile nafasi ya tatu.
 

MAYA: MIMI SIYO MGUMBA

MSANII mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kwamba siyo mgumba wala hana gundu ila ni muda tu haujafika wa kuzaa au kuolewa.
Maya aliyasema hayo kutokana na maneno ya watu wanaomuandama kwamba hazai na ana gundu ndiyo maana haolewi ambapo alisema siyo kweli ila anasubiri wakati ukifika atazaa kwani ana uzazi na hajawahi kutafuta mtoto na kumkosa.
“Bado sijapata mwanaume wa kunioa na sina gundu, kuzaa bado wakati haujafika ila ukifika naamini Mungu atanipatia maana mayai ya uzazi ninayo ya kutosha,” alisema Maya.

FILAMU YA PISHU KUINGIA SOKONI MEI MOSI

KITABU CHA 'THE 7 HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE' CHAZINDULIWA UPYA KWA LUGHA YA KISWAHILI‏

DSC_0006
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia) akimwonyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
DSC_0007
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto) akipitia kurasa mbalimbali za kitabu hicho kabla ya uzinduzi rasmi. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege.
DSC_0053
Mwezeshaji wa Franklin Covey, Alice Levora akichambua kwa ufupi tabia 7 zilizomo kwenye kitabu hicho kwa wageni waalikuwa (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi rasmi.
Na Mwandishi wetu
UWEKEZAJI mkubwa unatakiwa kufanywa katika eneo la raslimali watu, kama taifa hili linahitaji kuondokana na malalamiko kuhusu maendeleo na ajira.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu wakati akizindua tafsiri ya kiswahili ya kitabu cha “The 7 Habits of Highly effective people” kilichoandikwa na Mmarekani, Stephen Covey.
Hii inakuwa tafsiri ya kwanza ya kitabu hiki kwa lugha za asili zinazotumika bara la Afrika .
Alisema malalamiko mengi kuhusiana na taifa kuwa na raslimali nyingi na umaskini kuendelea kuwepo yanatokana na kutoendelezwa kwa raslimali watu kwa lengo la watu kujitambua, kutambua wanachotaka na kusababisha kiwepo.
Alisema inasikitisha kuona kwamba watanzania wengi wanalalamika kuhusu hali ngumu kumbe ilhali wao huenda ndio wakawa sababu za matatizo hayo ya ukosefu wa maendeleo.
Alisema ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika kwa kuwa vitabu hivyo vina tafiti nyingi za miaka mingi ambazo watanzania wakitumia kwa muda mfupi watafanya mabadiliko katika maisha yao.
Alisema uwapo kwa tafsiri ya Kiswahili kwa moja ya vitabu vyenye sifa kubwa duniani katika masuala ya menejimenti na ambacho kimekuwa katika 20 bora za vitabu duniani kwa miaka 20, kutasaidia watanzania wengi kujiangalia na kujifunza kuwa na dira na nidhamu ya kutekeleza yale ambayo wanayafikiria.
Alisema kwamba ari ya kusoma kazi mbalimbali kutasaidia watanzania kuwa na upeo mpana wa kujituma na kuwa na nidhamu ya malengo wanayostahili ya kufikia kwa muda mfupi na kwa ufanisi mkubwa.
Tafsiri hiyo ya kitabu ambayo imewezeshwa na Baraza la Kiswahili nchini Tanzania (BAKITA) na imeandaliwa taasisi ya ushauri wa masuala ya maendeleo ya raslimali watu (NFT).
NFT ambayo makao makuu yake yapo mjini Kampala, Uganda ina matawi Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Wajibu wake mkubwa taasisi hiyo ni kukabilina na changamoto mbalimbali za wafanyakazi kwa kutoa mafunzo yenye kutengeneza manufaa kwao na kwa menejimenti ya uhuru na kutegemeana katika kufanikisha maono ya taasisi husika.
Kutumika kwa kitabu hicho chenye kurasa 380 kwa kuangalia tabia zenye manufaa kunatokana na haja ya kubadilisha mfumo wa uongozi na ushirikishaji wenye lengo la kuchochea kutegemeana katika kuleta ufanisi.
DSC_0115
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kulia) na Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa (wa pili kushoto) pamoja na wadau wengine wakifuatilia uchambuzi wa kitabu hicho.
DSC_0081
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wageni waalikwa.
DSC_0248
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo alitoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika.
DSC_0149
Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa akielezea changamoto alizokutana nazo wakati wa kutafsiri kitabu hicho.
DSC_0278
Pichani ni kikundi cha burudani kutoka Tanzania House of Talent (THT) wakitumia sanaa "Choreograph" kuzindua rasmi kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
DSC_0291
DSC_0303
Sasa kimezinduliwa rasmi.
DSC_0308
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akipokea kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia). Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa
DSC_0313
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akionyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani).
DSC_0316
Kutoka kushoto ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Vida Mutasa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege, Mkurugenzi wa NFT Consult, Nambie Kiwanuka pamoja na Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong.
DSC_0339
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania.
DSC_0252
Mratibu wa shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People"kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kutoka JB's PR & Events, Babbie Kabae akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani).
DSC_0061
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa ambao ni maafisa rasilimali watu na wadau kutoka makampuni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.
DSC_0055
DSC_0100
DSC_0103
DSC_0106
DSC_0379

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate