-Viongozi
 wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka 
walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es 
Salaam jana. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), 
Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na 
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba 
na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk. Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.
 Makatibu
 wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada
 ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa 
Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. 
Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na 
Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.