EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, September 28, 2013

Watatu EPA waenda jela

Habari na Happiness Katabazi wa Tanzania Daima.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewahukumu kwenda jela miaka tofauti washitakiwa watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa sh bilioni 1.1 katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

Hatua hiyo ni baada ya kuwakuta na hatia katika makosa mbalimbali, likiwemo la kughushi hati ya kuhamisha deni toka Kampuni ya Marubeni ya Japan kwenda Kampuni ya Changanyikeni Residential Complex ya nchini.

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai iliyokuwa ikiwakabili Bahati Mahenge, Manase Makalle, Davis Kamungu, Geofrey Mosha na Edda Mwakale ambaye ni mke wa mshitakiwa wa pili, ilitolewa na jopo lililokuwa likiongozwa na Jaji Sekela Mushi, Jaji Sam Rumanyika na 

Hakimu Mkazi Lameck Mlacha ambaye aliisoma kwa niaba ya wenzake.
Mlacha alisoma hukumu hiyo kwa kuanza kuikumbusha mahakama kuwa hati ya mashitaka ilikuwa na mashitaka tisa na kwamba kosa la kwanza ni kula njama kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu ya mwaka 2002.

Alisema kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Desemba 23 mwaka 2003 na Oktoba 26 mwaka 2005, ambapo kwa pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani walitenda kosa hilo na kuiibia BoT.

Hakimu Mlacha alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vyote, mahakama yake inawatia hatiani Mahenge na Manase na kuwahukumu kwenda jela miaka mitano huku akiwaachia huru washitakiwa wengine.

Wasichana 55,000 wakosa masomo kwa ujauzito.

ZAIDI ya wasichana 55,000 wa shule za msingi na sekondari Tanzania Bara, wamekatisha masomo yao kwa sababu za ujauzito.

Licha ya kukatisha masomo, wasichana hao walitengwa na jamii baada ya kupata ujauzito na kuwaharibia mtiririko bora wa maisha yao katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Hayo yalibainika Dar es Salaam juzi usiku wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti namna Wasichana wa shule nchini Tanzania wanavyofanyiwa kwa nguvu vipimo vya ujauzito na kufukuzwa wanapokutwa wajawazito.

Utafiti huo ulifanywa na Kituo cha Kutetea Haki ya Uzazi kiitwacho Centre for Reproductive Rights kati ya mwaka 2012/2013 na kubainisha hayo huku ukieleza kwamba asilimia 44 ya wasichana Tanzania Bara wamepata mimba wakiwa na umri chini ya miaka 19 huku wengi kati yao wakitengwa na jamii.

Akizungumzia utafiti huo mkurugenzi mkazi wa kituo hicho kanda ya Afrika Evelyne Opondo alisema utafiti huo umehusisha shule za bweni za serikali na binafsi.

“Tumegundua kwamba wakuu wa shule wanawapima mimba wananfunzi kwanza kwa njia za kienyeji, pili wanafanya hivyo bila kujua kwamba hakuna sheria wala sera inayowaruhusu kuwapima mimba wanafunzi hao.

Atupwa jela kwa kuendesha bodaboda bila leseni.

MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela mshitakiwa Lupembe Majebele (25), mkazi wa Kijiji cha Lutende, Wilaya ya Uyui mkoani Tabora kwa kosa la kuendesha pikipiki bila leseni.

Awali akisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi, Mwendesha Mashtaka wa Polisi Dezidery Kaigwa aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili.

Aliiambia mahakama kuwa kosa la kwanza ni kuendesha chombo cha moto bila leseni kinyume na sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1963 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 inayozuia kufanya makosa kama hayo na kosa la pili ni kumgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake.

IANPHI KUFANYA MKUTANO WAKE WA 8 TANZANIA


 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kuratibu mkutano wa nane wa mwaka wa  taasisi hiyo  na kupata nafasi ya kuing'arisha nchi katika ramani ya dunia na hatimaye kuweza kutangaza maliasili zake na vivutio vya Utalii vilivyomo. Mkutano huo wa nane wa IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka huu jijini Arusha katika Hoteli ya Ngurdoto.
 Akizungumza hii leo jijinni Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii(IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dr. Mwele Malecelaamesema mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama.

Bodi yatangaza wanafunzi waliopata mikopo katika mwaka wa masomo 2013/2014.

SERIKALI imetangaza kuwapatia mikopo wanafunzi wa elimu ya juu 29,754 kati ya wanafunzi 31,647 katika mwaka wa masomo 2013/2014.


Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa, alieleza hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa utoaji wa mikopo hiyo kwa wanafunzi wapya na wanaoendelea na elimu ya juu.

Alisema uchambuzi wa maombi ya mikopo kwa mwaka huu wa masomo umekamilika na kwamba lengo la serikali ni kuwawezesha wanafunzi wa elimu ya juu kupata fedha kwa muda muafaka.

Alisema kuwa mchanganuo wa utuoaji wa mikopo hiyo ulizingatia vigezo na masharti ya uombaji mikopo na ruzuku.

Alisema idadi ya waombaji wapya waliotuma maombi yalikuwa 53,239, waombaji wanaoendelea na masomo 43,032, waombaji waliokuwa na maombi yenye matatizo ni 6,364.

“Wengine ni waombaji waliorekebisha matatizo kwenye maombi yao 3,151 na waombaji ambao hawakurekebisha matatizo kwenye maombi yao 3,213,” alisema.

Akifafanua zaidi kuhusu mchanganuo huo alisema waombaji wapya 53,630 watakaosoma  ndani na nje ya nchi wamepata mikopo hiyo.

Alisema maombi ya mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea 61,692 ambao wanasoma ndani na nje ya nchi wamepangiwa kupata mikopo hiyo.

Friday, September 27, 2013

Mrisho Ngassa amelipa Milioni 45 za Simba.

Mrisho Ngassa (katikati) akionyesha risti ya malipo aliyopewa TFF baada ya kulipa deni la mil 45, kushoto kwake ni mhasibu wa Yanga, Rose Msamila na kulia ni Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Young Africans Mrisho Khlafani Ngassa leo amelipa jumla ya mil 45, deni la mil 30 pamoja na faini ya mil 15 za klabu ya Simba SC kwa Shirikisho la Soka nchini TFF ili aweze kuitumikia timu yake kuanzia kesho.

Ngassa ambaye aliambatana na viongozi wa klabu ya Yanga mjumbe wa sekretariat Partick Naggi, Afisa Habari Baraka Kizuguto na mhasibu Rose Msamila alikabidhi hundi za malipo kwa idara ya fedha ya shirikisho hilo.

Mara baada ya kukabidhi hundi hiyo Ngassa aliongea na waandishi wa habari nje ya ofisi za TFF na kusema ameamua kulilipa deni hilo ili aweze kuitumikia klabu yake, kwani kukosa michezo sita kumemnyima fursa ya kuisaidia timu yake.

MASTAA WAAIBIKA KWA MADENI

Mastaa wa kada mbalimbali Bongo, akiwemo mtangazaji Maimartha Jesse, mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, wanamuziki Elias Barnaba, Aneth Kushaba wa Skylight Band na wanawake wa mjini, Maila Msafiri na Devotha, wanadaiwa kuaibika kisa madeni.
Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Habari zinadai kuwa mastaa hao wamekuwa wakihenyeshwa na madeni ya nguo kutoka kwenye duka moja lililopo maeneo ya Kinondoni, Dar linalomilikiwa na mtangazaji ambaye pia ni mwigizaji, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Akizungumza na gazeti hili huku akidondosha chozi, Aunty Lulu alisema anasikitishwa na kitendo hicho alichofanyiwa na mastaa wenzake.
“Niliwaamini, nikawakopesha nguo lakini wamekuwa wakinisumbua kwenye kunilipa. Inauma sana kwa sababu wanataka kunirudisha nilikotoka.

BABA MZAZI KANIBAKA MIEZI TISA...BINTI DARASA LA TANO.


Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan KWELI dunia haina huruma! Binti wa umri wa miaka 15 tunayemtambulisha kwa jina moja tu la Zaina, mkazi wa Kimara jijini Dar ameamua kufunguka na kusimulia jinsi alivyokuwa akibakwa na baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina moja la Mohamed, Ijumaa ndiyo lina habari hii ya kusikitisha.
 
Binti wa darasa la tano aliyebakwa na baba yake kwa miezi tisa.
ANAANZA KWA KUANIKA HISTORIA YAKE FUPI!
Akisimulia kwa uchungu, Zaina alianza kwa kuanika historia yake kwa ufupi kwamba tangu atoke tumboni, hakuwahi kumuona mama yake zaidi ya kuoneshwa kwenye picha tu!
 
Akasema hiyo yote ilitokana na hadithi aliyowahi kusimuliwa kwamba, akiwa kichanga, baba huyo alimuiba kwa mama yake anayeishi Kigamboni, Dar na kwenda kumlea Kimara kwa ushirikiano na mama yake wa kufikia.
 
Lakini akasema: Hata huyo mama wa kambo mwaka jana aliachana na baba baada ya kutufumania chumbani mimi na baba, akakasirika na kuondoka zake.
Kamanda Suleiman Kova.
SIKIA FILAMU KAMILI SASA
“Nakumbuka ilikuwa mwanzoni mwa mwaka jana, nikiwa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kimara ndipo baba alipoanza tabia ya kunilazimisha tufanye mapenzi. Alisema anataka tufanye kwa njia ya kawaida na ya kinyume na maumbile.
 
“Nilikataa lakini akawa ananilazimisha na vitisho juu. Tulianza kwa kufanya mchezo huo na baba lakini si kwa kupenda kwangu, nililazimika kwa sababu niliamini ni baba ambaye anaweza kunifanya lolote kama nitakataa, mbaya zaidi hakuwa akitumia kinga,” alisema na kuongeza:
 
“Kuanzia hapo, zoezi hilo liliendelea kila siku hadi mwishoni mwa mwaka jana nilipoamua kutoroka na kwenda kuwaeleza ndugu wa baba, kule Tanga.”

Miss Universe Tanzania kujulikana leo

SWALI la nani atatwaa taji la Miss Universe Tanzania 2013, linatarajiwa kupata jibu leo wakati warembo 15 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania watakapochuana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, mkabala na IFM jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja kamili usiku.

Warembo hao mbali ya kuwania taji la Miss Universe Tanzania, ambalo kwa sasa linashikiliwa na Winfrida Dominique, pia watawania taji la Miss Earth Tanzania na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

Warembo hao kwa nyakati tofauti, wamekuwa wakitambiana huku kila mmoja akijigamba kutwaa taji hilo na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika jijini Moscow, Russia Novemba 9.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications inayoandaa mashindano hayo, Maria Sarungi, alisema kuwa kila kitu kimekamilika na warembo wamepania kufanya makubwa jukwaani, ambapo warembo wote wana ari ya juu na kila mmoja akiwa na shauku ya kutwaa taji hilo.

“Kwa upande wetu, kila kitu kiko tayari, warembo wamejiandaa vilivyo na tumeandaa shoo bora na fupi, hivyo mashabiki wa masuala ya urembo wanatakiwa kufika mapema ili kuona nani anatwaa taji na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi kimataifa,” alisema Maria.Warembo watakaochuana leo ni Aziza Victoria, Irene Nsiima, Betty Boniface, Kundi Mlingwa, Mariam Ngwangwa, Naomi Kisaka, Glady Msemo, Salsha Lukiko, Upendo Dickson, Vestina Mhagama, Angela Lutataza, Consolata Mosha, Clara Noor, Agnes Thobias, Dinah David na Clara Noor.

Madiwani Bagamoyo waishukia Tasaf..watumikisha wananchi kazi za miradi mbalimbali huku fedha wakichukua wao.

Habari na Zawadi Chogogwe wa Tanzania Daima.
MADIWANI wa Halmashauri ya Bagamoyo, mkoani Pwani, wamelaani kitendo cha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kufika katika vijiji vya Bagamoyo na kuwatumikisha wananchi kazi za miradi mbalimbali huku fedha wakichukua wao.

Madiwani hao waliibua hayo mjini Bagamoyo juzi katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka 2012 na 2013 kilichofanyika katika ofisi za mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambacho kilihudhuriwa na wataalamu mbalimbali.

Diwani wa Kilomo, Hassan Usinga, alisema Tasaf wamekuwa na tabia ya kutofika kwa watendaji wa vijiji pindi wanapofanya kazi zao za miradi na badala yake wanaenda moja kwa moja kwa wanakijiji na kuwatumikisha katika miradi ya maendeleo huku wakiwalipa fedha kidogo.

“Kitendo cha kwenda kwa wanakijiji kuwafanyisha kazi na kuwalipa fedha kidogo kumechangia miradi mingi kuwa mibovu huku mingine ikiwa imekufa kama vile miradi ya kuku,” alisema Usinga.

Alisema taarifa za maendeleo ya vijiji zinaonyesha kuwa dawa za mifugo na matumizi zimetolewa kwa wanakijiji na kueleza kuwa taarifa hizo zikiwa hazina ukweli.

“Kutowashirikisha watendaji wa vijiji katika mikutano ya maendeleo kumepelekea kukosa wanakijiji wengi kushiriki katika mikutano yao,” alisema.

Alisema wanaoshiriki wanakuwa wachache hali inayowafanya Tasaf kuwavalisha fulana na kofia huku wakiwapiga picha na kuzipeleka kwa wafadhili kwa kuonyesha ushahidi kuwa wanakijiji wameshiriki mkutano huo wakati sio kweli.

Soko la Kariakoo laelemewa na wateja kutokana na idadi kubwa ya watu 62,000 wanaoingia.

SOKO la Kariakoo jijini Dar es Salaam limeelemewa na wateja kutokana na idadi kubwa ya watu 62,000 wanaoingia na kutoka kila siku kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

Meneja Mkuu wa soko hilo, Florence Seiya, alibainisha hayo alipozungumza  ofisini kwake jana na kusema kwa siku soko hilo linahudumia watu 62,000.

Alisema mbali na kuelemewa na wateja, soko hilo linahitaji ukarabati utakaogharimu sh bilioni moja.

Alisema soko hilo lililojengwa miaka 39 iliyopita lina wafanyabiashara halali 1,558, mbali na wale wanaouza biashara za mkononi wanaojulikana kama ‘wamachinga’.

“Wafanyabiashara waliomo shimoni ni 600, walioko nje soko dogo ni 190, walioko ndani soko dogo ni 289, soko kubwa ni 189 waliobaki ni Mtaa wa Swahili eneo la soko,” alisema Seiya.

Seiya alisema kadiri siku zinavyokwenda nafasi inazidi kuwa ndogo, baada ya Shirika la Masoko Kariakoo kushindwa kujenga soko jingine la ghorofa la kisasa litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 4,000 kwa wakati mmoja.

Pia alisema kumekuwapo na ufinyu wa barabara za kuingilia sokoni hapo kutokana na magari mengi yanayoegeshwa katika soko hilo, mikokoteni, pikipiki na wale wafanyabiashara wanaofanya biashara zao kwenye barabara za lami.

‘Wajumbe wa Tume hawatajiuzulu’.

Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hakuna mjumbe wa Tume hiyo aliyetishia kujiuzulu licha ya kwamba wanafanya kazi kwenye mazingira magumu.

 
Amesema katika awamu ya pili ya kukusanya maoni kupitia Mabaraza ya Wilaya ya Katiba wajumbe hao wamefanya kazi ngumu huku wakikabiliwa na changamoto nyingi, lakini wamevumilia kwa sababu wanafuata sheria.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema: “Naona kwamba wajumbe wa Tume wanaeleweka vibaya kwamba wanataka kujiuzulu, lakini jambo hilo halipo kwani wanafanya kazi kwa kufuata sheria.

Warioba: Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ina upungufu.

Dar es Salaam. 
Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.

 
Warioba alisema jana kwamba ni jambo la kushangaza sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, wakati huohuo ikieleza kuwa itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni.


Kauli hiyo ya Warioba imekuja wakati vyama vya NCCR Mageuzi, Chadema na CUF, vikifanya mikutano nchi nzima kuwashawishi wananchi kupinga kile wanachokiita hujuma dhidi ya upatikanaji wa Katiba Mpya.


Sheria hiyo ambayo Warioba amesema ina upungufu, muswada wa marekebisho yake ulijadiliwa na kupitishwa wa wabunge Septemba 6, mwaka huu katika Mkutano wa 12 wa Bunge Mjini Dodoma, ikiwa ni baada ya kubadilishwa kwa baadhi ya vifungu na hivi sasa Rais Kikwete anasubiriwa kuusaini ili iwe sheria kamili. 

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU MWANAMKE ALIYEONGOZA UGAIDI KENYA.

Mwanamke anayedaiwa kuongoza ugaidi Westgate, Samantha Lewthwaite.
Na Mwandishi wetu:
TUKIO kubwa la kigaidi lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika jengo la maduka makubwa na ya bei mbaya jijini Nairobi la Westgate, limeelezwa kuwa liliongozwa na mwanamke raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite.
Yafuatayo ni mambo kumi usiyoyajua juu yake.
1. Samantha, mwenye umri wa miaka 29, ni mzaliwa wa Buckinghamshire, Uingereza anayeelezewa na magaidi wa kundi la Al Shabaab kama mwanamke mwenye akili nyingi, akiwa ni mama wa watoto watatu ambaye alikata mawasiliano na familia yake baada ya kuhamia Kenya mwaka 2007.

2. Ripoti za kipolisi zinaonesha kuwa ni mkufunzi wa wanawake wa kikundi hicho cha kigaidi wanaochukua mafunzo ya jihad, mke wa zamani wa Germaine Lindsay, ambaye alijiua baada ya kuhusika na shambulio la bomu kwenye treni ya chini ya ardhi jijini London, Julai 7, 2005.

3. Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali zinazoaminika kuwa ni zake, ambazo zilitangazwa na Gazeti la Daily Mail la Uingereza, mwanamke huyo anawalea watoto wake ili waje kuwa wanaharakati wa imani kali. Mumewe wa pili, Habib Saleh Ghani naye ilidaiwa kuwa aliuawa kwenye tukio lingine la ugaidi.

4. Baadhi ya nyaraka zinaonesha kuwa katika baadhi ya mawasiliano na mumewe, aliwahi kusema: “Ghani alizungumza na kijana wangu wa miaka nane na binti yangu wa miaka mitano akiwauliza wanachotaka kuja kufanya wakiwa wakubwa, wana majibu mengi lakini wote wanakubaliana kwamba watakuja kuwa Mujahidina.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate