AMA
 kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Hatimaye uliokuwa uhusiano wa
 chini kwa chini wa nyota wawili wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi 
‘Ray’ na Chuchu Hans, siyo siri tena baada ya wahusika hao wakuu 
kujiachia ‘live’, Ijumaa limeshiba.
 Ray na Chuchu Hans wakiwa katika pozi la kimahaba.
Ray na Chuchu Hans wakiwa katika pozi la kimahaba. 
KIMAHABA ZAIDI
Ishu hiyo ilitokea mapema wiki hii ambapo Chuchu 
alitundika picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Ray chumbani 
kimahaba.
Kufuatia tukio hilo kuliibuka gumzo kubwa na kulifanya 
jambo hilo kuwa ndiyo habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa 
filamu za Kibongo.
Katika picha hiyo, Chuchu anayetumia jina la Chukichuku kwenye 
Instagram aliambatanisha na maneno yaliyosomeka ‘Me n U’ akimaanisha 
yeye na Ray hivyo kutoa fursa kwa mashabiki wao kusema chochote.
Kwa mujibu wa mashabiki hao, Ray na Chuchu kwa sasa ndiyo love bird au ‘maua’ yanayopendezesha tasnia hiyo.
“Mmependezaaa…mapenzi waziwazi,” ilisomeka komenti ya mmoja wa mashabiki hao.
“Nilikuwa simuelewi Ray lakini hapa nimemsoma. Wamependeza sana,” 
ilisomeka komenti nyingine iliyoungwa mkono na mashabiki wengi kwa 
kupata ‘likes’ nyingi.
Mwingine aliandika: “Sasa walichokuwa 
wanagombea Mainda (Ruth Suka) na Johari (Blandina Chagula) kipo wapi? 
Ona sasa wamekosa wote… hahahaaa… wawaache miaka isiyohesabika.”
HAKUNA KIFICHO TENA
Katika kunogesha mambo, baadaye Chuchu aliweka
 picha ya Ray akimsifia jambo lililodhihirisha kuwa kwa sasa hawafanyi 
tena kificho kama miezi kadhaa iliyopita.
Habari za chini ya kapeti 
kutoka kwa wasanii wenzao wanaokuwa nao lokesheni zilieleza kuwa wawili 
hao wamekuwa wakionesha waziwazi kuwa wao ni item (kitu kimoja).
“Kuna siku tulikuwa tuna-shoot maeneo ya Sinza-Mori (Dar), yaani 
ungewaona wala usingeuliza maana kama hujui kusoma, ungeangalia hata 
picha. Yaani mapenzi kama njiwa!
“Sasa hivi ndiyo uhusiano ambao upo 
‘hoti’ kwenye tasnia yetu, sema ndiyo hivyo wenyewe walikuwa hawapendi 
ijulikane lakini naona wameshindwa kuendelea kujificha,” alisema 
mwigizaji huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.
CHUCHU ATAKA WASIINGILIWE
Baada ya kujikusanyia data, Ijumaa 
lilimtafuta Chuchu akiwa mmoja wa wahusika wakuu ambapo alipopatikana 
alikuwa na haya ya kusema: “Hayo ni mambo yetu binafsi, naomba 
tusiingiliwe katika mambo yetu.”
Ijumaa: Chuchu wewe ni kioo cha 
jamii na mashabiki wako wanataka kujua ukweli juu ya uhusiano wako na 
Ray. Unalizungumziaje hilo?
Chuchu: Weweee…sikia! Nimeshasema sitaki mtu aniingilie mambo yangu. Kwani mnataka nini nyiye?
Ijumaa: Je, hiyo picha mliyopiga chumbani ni hotelini au nyumbani?
Chuchu:
 Siwezi kukuelezea tumepiga wapi, iwe hotelini au nyumbani haiwahusu, 
naomba mniache jamani mbona hivyo? Kwani vipi? (kisha akakata simu).
KAKA MKUBWA VIPI?
Jitihada za kumpata Ray ‘Kaka Mkubwa’ katika 
tasnia ya filamu za Kibongo ili kupata neno lake juu ya ishu hiyo 
ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa 
na hata alipofuatwa ofisini kwake, RJ Productions pale Sinza-Mori, Dar 
hakupatikana.
KABLA YA PICHA
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai mazito kuwa Ray na
 Chuchu wanatoka lakini habari hizo zilikosa mashiko kwa kuwa hakukuwa 
na ushahidi wowote.
Ilidaiwa kuwa hata ile vita ya hivi karibuni ambapo Johari na Chuchu walizichapa kavukavu ilitokana na kugombea penzi la Ray.
JOHARI ASARENDA