EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, January 31, 2015

NAPE AANZA AMSHA-AMSHA YA MIAKA 38 YA CCM MJINI SONGEA

 Wananchi wakiwa katika shamrashamra za kumpokea Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye jana kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Ruvuma mjini Songea jana, alipowasli kwa ajili ya kuanzisha amsha amsha ya Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM ambayo inafanyika Jumapili hii, Kitaifa mjini Songea kwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
 Mratibu wa Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM, Emaanuel John Nchimbi akiwasili kwenye Ofisi hiyo ya CCM mkoa wa Ruvuma kumpokea Nape.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza wananchi kwenda katika maeneo mbalimbali kuzindua mashina ya Wajasiriamali wa CCM na kuhutubia mkutano wa hadhara, baada ya kuwasili mjini Songea.

Shakira na Gerard Pique wa Barcelona wapata mtoto wa pili

Msanii kutoka Colombia Shakira mwenye miaka ’37’ amebarikiwa kupata mtoto wa pili na mpenzi wake ambaye ni mwanasoka wa Barcelona ‘Gerard Pique’. Mtoto wao wa pili amepewa jina ‘Sasha’ . Sasha maana yake ni Alexander kwa tafsiri ya lugha ya Kirusi.
Shakira na Gerard walilipia floor nzima ya hospitali ya Quiron Teknono mjini Barcelona kwaajili ya kujifungua kwa Shakira na kukimbia mapaparazzi. Daktari aliyemzalisha Shakira mara ya kwanza ndio amemzalisha tema mara ya pili.
shakira 2

UNYAMA, UDHALILISHWAJI MTALAKA WA ISHA MASHAUZI UKWELI NI HUU


Stori: Musa Mateja/Risasi
HATIMAYE ukweli wa kutekwa, kuteswa kwa kudhalilishwa kwa aliyekuwa mume wa mwimba  taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’, umejulikana, Risasi Jumamosi limechimba.
Mfanyabiashara, Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa amefungwa kamba na watesi wake.
Januari 28, mwaka huu, picha za Tevez akiwa ametoka kuteswa kwa kudhalilishwa zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku wengine wakidai kisa ni kukutwa na mke wa  mtu, wengine wakisema ni dhuluma.
RISASI LAINGIA MTAANI KUCHIMBA
Risasi Jumamosi halikufanya haraka kuichapisha habari hiyo mpaka kuichimba kwanza ili kujua kisa na mkasa kamili ndipo iwapelekee wasomaji wake. Na ndivyo ilivyofanyika!

ASIAN MORGANI: NITAMPA SLIM TALAKA!

MREMBO ambaye aliwahi kunyakuwa Taji la Unique Model, Asia Morgan ambaye pia ni msanii wa filamu anayechipukia, amefunguka kuwa endapo mwigizaji Slim Omary aliyekuwa mumewe hatampa talaka, atampa yeye.
Msanii wa filamu Bongo anayechipukia, Asia Morgan.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Asia ambaye alitengana na Slim akimtuhumu kuwa na wivu wa kupindukia, alisema licha ya kudai talaka mahakamani Slim amekuwa mzito kuitoa hivyo dawa yake ni yeye kumpa.
“Unajua mimi na Slim tusingeachana kwa malumbano kiasi hiki yeye ndiyo chanzo sasa kwa kuwa anagoma kuniandikia takala yangu, nitamuandikia yeye ili tuondoe mzizi wa fitna,” alisema Asia.

DIAMOND AMTUSI X WA ZARI!

ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’,  juzikati aliamua kumtolea uvivu, aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King lawrenc kwa kumuita mpuuzi anayetafuta kiki kwa vile kila kukicha kazi yake ni kumfuatafuata kwa maneno ya kejeli na kumtusi.
X wa Zari, King lawrence akipozi.
Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, staa huyo alisema mara nyingi amejitahidi kumpuuza kwa kitendo chake cha kumkejeli katika mitandao ya kijamii, lakini kitu alichogundua ni kwamba mpenzi huyo wa zamani wa Zari anataka yeye amjibu ili aweze kulikuza jina lake, kitu ambacho  ni cha kijinga.
Zarinah Hassani ‘Zari’.
“Nimejitahidi sana kukaa kimya kila anaponitusi huyu jamaa, lakini kumbuka mimi ni binadamu, najaribu kuliangalia jambo hili nagundua kwamba hana chochote cha msingi anachoongea zaidi ya matusi,  anatafuta nimjibu kitu ili apate kiki aweze kutimiza ndoto zake,” alisema Diamond na kuongeza:

MSANII WA MAREKANI SUGE KNIGHT AKAMATWA KWA MAUAJI

Msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight.
Polisi nchini Los Angeles inasema kuwa msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight amekamatwa kutokana na mashtaka ya mauaji baada ya kumgonga mtu mmoja na gari lake hadi kumuua na baadaye kutoroka.

ZIARA YA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII KWA SOKO LA MAREKANI YAENDELEA LOS ANGELES


Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi akiongea katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (kulia) akiwa pamoja na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa soko la Marekani.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki ziara maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani.

Friday, January 30, 2015

KIJANA WA KIUME ANAYEVIZIMIKIA VIBIBI VYA ZAIDI YA MIAKA 60


Kyle Jones (31) akiwa na mpenzi wake, Karen, anasema huvutiwa tu na wanawake wanaomzidi umri kwa makumi kadhaa ya miaka.
Huyu ndiye Kyle, kijana mtanashati anayeachwa hoi na penzi la vibibi vizee.
Kyle and Karen wakiwa katika ‘mahaba niue’ walipokutana mara ya kwanza.

PAC YAISHAURI SERIKALI NAMNA YA KUINUSURU KAMPUNI YA TTCL‏


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu.
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa mapendekezo ya kuinusuru Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kutokana na hali mbaya ya kampuni hiyo kifedha kwa sasa ambapo inaendeshwa kwa hasara huku ikiwa na madeni makubwa. PAC imetoa mapendekezo hayo katika taarifa yao kwa bunge ya mwaka juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mashirika ya umma iliyotolewa Januari 28 mwaka 2015.
Kwa mujibu wa taarifa ya PAC hali ya mapato na matumizi ya TTCL kwa mwaka 2012 ilipata hasara ya bilioni 20.883 huku kwa mwaka 2013 ikipata hasara ya bilioni 16.258. PAC ilisema majumuisho ya hasara ya TTCL kupata hasara kwa takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na hasara ambayo kwa mwaka 2013 ilifikia bilioni 334.48, jambo ambalo limeiondolea mvuto wa kukopeshwa na taasisi za fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.

MWAKA MPYA NA MAMBO MAKALI ZAIDIII NDANI YA #AKCLASSICOSMETICS


NANI ASIYEWATAMBUA #AKCLASSICOSMETICS WAO NI MWENDO WA VITU VYA UKWEE NA ORIGINAL KABISA??? SASA MALI MPYA IMEINGIA #TEAMNATURALHAIR MPOO? SAFARI HII HAMJASAHAULIKA!!

 
PIA KUNA HABARI NJEMA KWA WADAU WOTE WANAOSUMBUKA NA MATATIZO MBALI MBALI KUHUSU NGOZI ZAO KAMA VILE KUUNGUA KWA MIKOROGO,WEUSI WA MACHONI(DARK CYCLE),KUSWEAT KULIKOPITILIZA,AKCLASSIC WAMEAMUA KUCHIMBA NA KUJA NA MAJIBU YA MATATIZO YENU TENA MADINI YASIYO NA MADHARA KABISAAA KWA NGOZI YAKO!!

   WALE WALIOTOKA KUJIFUNGUA NA YALE YOTE YATOKANAYO HATUJAWASAHAU PIA KUANZIA CORSETS,NYWELE(T444Z JBCO NA HAIRFINITY,SHEAR MOISTURE),WEUSI WA KWAPA NA SHINGO NA OFCOUZ NA BIDHAA ZA KUPIGA USO NA MWILI MSASA!!
 
  INGIA   www.akclassic.blogspot.com KUONA PICHA ZAIDI NA MAELEZO!!

Mrisho Ngassa: Nimerudi Yanga kuaga, naondoka

Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa.
Na Wilbert Molandi
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa, amesema kuwa amerejea kundini kuitumikia timu hiyo kwa moyo mmoja lakini kubwa zaidi ni kuwa anataka kuwaaga mashabiki wa Jangwani.
Tangu siku kumi zilizopita, Ngassa hakuonekana Jangwani huku Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Kiboroha akisikika akisema wamedokezwa kuwa staa huyo amekwenda Afrika Kusini kufanya majaribio lakini Ngassa mwenyewe amesema alitimkia Tanga kupumzisha akili kutokana na deni la shilingi milioni 45 analodaiwa na benki, ambalo amesusiwa na viongozi wa Yanga walilokubaliana walilipe kwa pamoja.

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MAJENGO YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wafanyakazi wa ubalozi baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.

KEKI YA JOKATE KWA MILLARD AYO YAIBUA MAMBO!


‘Mtu wa Nguvu’ Millard Ayo na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakifurahia jambo kwenye ‘bethidei’ yake. 
Stori: Hamida Hassan na Musa Mateja/Ijumaa
Keki iliyoandaliwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa ajili ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Millard Ayo ‘Mtu wa Nguvu’ imeibua mambo kwa mashabiki wao.
TUJIUNGE NA MILLARD
Ishu hiyo ilijiri Januari 26, mwaka huu ambapo Jokate alimpekea keki ofisini kwake Mikocheni jijini Dar, na kujumuika na jamaa zake kukata keki hiyo.
Kwenye pati hiyo, Millard ambaye ni mtangazaji mkali wa Vipindi vya Amplifaya na Top 20 vya Clouds FM, alidaiwa kumwalika Jokate ambaye mashabiki wao walimpa jina la Special Girl (msichana maalum).
Pia katika pati hiyo, ‘ubuyu’ ulienea kwamba Jokate ndiye aliyekaangariza madikodiko na kupakua nyumbani kwa jamaa huyo kisha akamwandalia bonge la keki.

PARTY YA AMANDA, FULL KUDENDEKA

Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ akimlisha keki rafiki yake, 'wastara'.
Na Hamida Hassan/Ijumaa
Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alifanyiwa pati ya bethidei ambapo kwenye zoezi la kuwalisha keki mashosti zake, aliwashangaza watu kwa kusema wote atawalisha kwa mdomo ‘staili ya kudendeka’.

JACK DUSTAN ADAIWA ANA MIMBA YA MWARABU!

Msanii wa filamu ambaye ni zao la Shindano la Maisha Plus, Jack Dustan.
Na Imelda Mtema/Ijumaa
Msanii wa filamu ambaye ni zao la Shindano la Maisha Plus, Jack Dustan anadaiwa ni mjamzito huku mlengwa wa mzigo huo akidaiwa kuwa Mwarabu aliyewahi kuripotiwa kuwa anatoka naye.
Jack alitua hivi karibuni akitokea Dubai alikokuwa akiponda maisha na mara kadhaa amewahi kutundika picha mtandaoni akiwa kimahaba na mwanaume huyo wa Kiarabu.
Akizungumzia madai hayo, Jack alisema: “Mimi ni mwanamke bwana, kuzaa ni wajibu kwa hiyo sioni kama ni skendo mimi kuwa na mimba.”
Jack Dustan akipozi.
Alipoulizwa kama ni ya mwanaume Mbongo au yule Mwarabu wake, mwanadada huyo alipata kigugumizi na kuishia kusema: “Msubiri nikijifungua.”

Thursday, January 29, 2015

KUHUSU WIMBO MPYA WA AY ‘ZIGO’, INFO NDIO HIZI

ay 3
Elchapo aka Ambwene Yessaya aka AY anatarajia kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Zigo’ February 02, 2015 uliyofanywa na mtayarishaji wa muziki Nahreel na kufanyiwa mixing na Marco Chali.
AY amesema kuwa wimbo wake mpya ‘Zigo’ sio collabo, Ana collabo nyingi tayari, hii kaamua kufanya mwenyewe.
 ay 2

IYOBO: MIMBA YA ‘BABY’ NI FARAJA KWANGU

Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul  ‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty  Ezekiel.
Moses Iyobo akiwa na mpenziwe ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty  Ezekiel.
Akizungumza na Amani hivi karibuni,  Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.
“ Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

JIPATIE NAKALA YAKO YA GAZETI LA UWAZI MIZENGWE YA UCHAGUZI KILA IJUMAA

WAZAZI WA MANAIKI WAMTOLEA NJE WOLPER

Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga,amesema kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwa sababu wazazi wake wamemtolee nje ishu ya kwenda kumposa staa wa kike Bongo, Jacqueline Wolper.
Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga akiwa na Jacqueline Wolper.

SIMULIZI YA KUSIKITISHA YA MAMA ALIVYOUA WANAYE WAWILI

Stori: Mwandishi Wetu, Tabora/Amani
BADO hali ni tete kufuatia mwanamke mmoja, Zuhura Sudi (26), mkazi wa Mtaa wa Utusi Kata ya Chemchemi Manispaa ya Tabora kudaiwa kuwaua kwa kuwakaba shingo watoto wake wawili, Mwamvua (6) na Sudi Mrisho (miezi saba) kisha kuwazika kwenye mashimo mawili ndani ya nyumba.
Mwanamke (Zuhura Sudi) anayetuhumiwa kuwaua watoto wake.
Tukio hilo ambalo limeishangaza nchi hasa kufanywa na mama mzazi ambaye anaujua uchungu wa kuzaa, lilijiri Jumapili usiku ndani ndani ya nyumba ya mwanamke huyo.
SIKU MOJA KABLA
Taarifa kutoka vyanzo vya uhakika, siku moja kabla ya tukio, mwanamke huyo ambaye ni mtata kiasili alionekana akicheza na watoto wake na watoto wa jirani huku akionesha uchangamfu mkubwa.
“Kama wale watoto wake wangejua mama yao mzazi ndiyo safari ya kifo chao naamini wasingemchangamkia mama yao.
“Walicheza kwa amani, kwa upendo. Kumbe mama ana mahesabu yake. Haiwezekani leo niambiwe kuwa mawazo ya kuwaua watoto wake aliyapata ghafla,” alisema shuhuda mmoja.
Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi.
USIKU, JIRANI ASIKIA KISHINDO
Jirani mmoja na nyumba ilipotokea tukio alisema:
“Mimi awali ya siku ya kuelekea usiku wa tukio, nilimwona yule mama. Nikasalimiana naye. Alionekana yupo kawaida tu.

MGANGA WA DIAMOND JELA MIAKA 7

Stori: Richard Bukos/Amani
Yule mganga aliyejitapa kumtengenezea nyota ya mvuto staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ustadh Yahya amehukumiwa kifungo cha miaka saba (7) jela baada ya kukutwa na hatia katika kisa cha kuchanganya akihusishwa na wizi wa gari.
Ustadh Yahya akiwa chini ya ulinzi.
TUJIUNGE MAHAKAMA YA WILAYA YA ILALA
Habari za uhakika zilieleza kwamba aliyehitimisha kesi hiyo ni Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar, Hassan Kisailo mapema Jumatatu wiki hii wakati jua la asubuhi likiwaka.

MALI, IVORY COAST NAZO ZATINGA ROBO FAINALI AFCON

 

Mali wakipambana na Guinea.
TIMU za Mali na Ivory Coast nazo zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa Afrika 2015 kutoka Kundi D huku Guinea na Cameroon wakiyaaga mashindano hayo.
 
Ivory Coast wakipongezana kwa ushindi dhidi ya Cameroon usiku huu.
Mali wamesonga mbele baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Guinea huku Ivory Coast wakiwachapa Cameroon bao 1-0.
Kwa matokeo hayo Mali na Ivory Coast zimeungana na Ghana, Algeria, Congo, Equitorial Guinea, Tunisia na DR Congo katika hatua ya robo fainali.
Katika hatua hiyo ya robo fainali, DR Congo watavaana na Congo, Tunisia na Equitorial Guinea, Ghana na Mali huku Algeria wakikipiga na Ivory Coast.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA SHERIA

Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Othman Chande (Kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini mwaka 2015. Maadhimisho hayo yanaongozwa na maudhui yasemayo “ Fursa ya kupata haki: wajibu wa Serikali, Mahakama na wadau”. Kushoto ni Mh. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama.
Msajili Mkuu wa Mahakama, Ignas Kitus (kulia) akizungumza akifafanua jambo wakati Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Othman Chande alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo leo. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
 
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 Rais Jakaya Kikwete anatarijiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya sheria nchini (Law Day) itakayofanyika Februari 4, 2015, katika viwanja vya mahakama vilivyopo mtaa wa Chimala jijini Dar es salaam.

Wednesday, January 28, 2015

WASTARA AKIRI KUSHUKA KISANAA

STAA wa filamu nchini, Wastara Juma amesema anajihisi kupoteza mwelekeo unaomfanya kushuka kisanaa tokea kufariki kwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kwani ari yake ya kufanya kazi imepotea.
Staa wa filamu nchini, Wastara Juma.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, alisema Sajuki alikuwa ni msaada mkubwa sana kwake kisanaa mbali na maisha ya kawaida, kwani anashindwa kupita njia alizokuwa anapitishwa na mumewe huyo kiasi cha kujikuta akitoa filamu kati ya mbili hadi tatu kwa mwaka.
“Nikiri tu kwamba nimeshuka kisanaa, kasi ya kipindi kile imepungua, mume wangu alikuwa akijituma kuhakikisha mikakati yetu inaenda, kwa mwaka mzima nilitoa filamu hata tatu lakini toka asa naambulia moja tu mwaka mzima,” alisema.

Lipumba,wafuasi 32 wa CUF watiwa ndani Jijini Dar


Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba akizozana na polisi muda mfupi kabla ya kukamatwa pamoja na wafuasi wengine 32 wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana. 
 Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba akiwa chini ya ulinzi,eneo la Mtoni Mtongani jijini Dar jana,baada ya  Polisi kusitisha maandamano ya chama chake.
 ====== ======  ========
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho,Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WETE-KASKAZINI PEMBA,AWATAKA VIONGOZI WA CUF KUTENDA HAKI KWA WANANCHI

Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukikatiza mapema jioni ya leo katikati ya msitu akielekea katika kijiji cha Mnarani -Makangale kuzungumza na wanachama wa chama hicho,micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Vijana wapatao 105 waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM,katika kijiji cha Mnarani Makangale,ambapo alikwenda kushiriki ujenzi wa tawi lao liitwalo Maskani tuheshimiane.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Vijana wapatao 105 waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM.Wakisoma taarifa yao kwa Ndugu Kinana walieleza manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF,walieleza kuwa tangu wamehama chama hicho wamekuwa wakibugudhiwa na kufanyiwa fujo kiasi ambacho wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao za kimaendeleo ikiwemo na shughuli zao za uvuvi kusimama,hivyo wamemuomba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kulishughulikia jambo hilo ili waweze kuendelea na shughuli zao bila kubugudhiwa kwani wanataka kuishi kwa amani na utulivu.

UNESCO YATAKA UBIA NA MWEDO

DSC_0005
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (kushoto) akimkaribisha Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues kwenye ofisi za asasi hiyo kwa ajili ya mazungumzo jijini Arusha.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, limesema kwamba litaingia ubia na asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO) ili kuimarisha mradi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan.
Mradi huo mkubwa unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Samsung umelenga kuinua maisha ya jamii ya wafugaji wa kimasai kwa kuwawezesha kielimu, kitamaduni na kiujasirimali.
Kauli ya kutaka kuingia ubia imetolewa na Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues wakati alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwedo, Ndinini Kimesera katika ofisi za Mwedo mkoani Arusha.
Alisema Unesco inataka kutumia uzoefu wa Mwedo katika ushirikishaji wananchi hasa katika uwezeshaji ujasirimali na elimu kufanikisha moja ya miradi mikubwa ya kisayansi katika kijiji cha Ololosokwan.
DSC_0031
Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (katikati) alipotembelea ofisi hizo jijini Arusha. Kulia ni Mshauri wa kiufundi, usimamizi na tathmini wa MWEDO, Bw. Paul Wilson.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate