MCHUNGAJI wa kanisa moja la kilokole lililopo Kichangani, Majohe, Dar
aliyetajwa kwa jina moja la Benard anadaiwa kutiwa mbaroni kwa tuhuma za
ulawiti wa mtoto wa kiume (jina tunalo) mwenye umri wa miaka 15.
Hivi karibuni, gazeti hili lilipenyezewa kuwepo kwa sakata hilo ambapo
lilitinga eneo la tukio na kuweka ‘patroo’ ili kunasa habari kamili.
Kwa mujibu wa mdogo wa mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Hamis, kaka yake huyo alikamatwa wiki iliyopita baada ya watu
waliojitambulisha kuwa ni askari kufika nyumbani na kumuweka chini ya
ulinzi.
Alisema kuwa katika kuishi na kaka yake huyo, aliwahi
kumuona huyo mtoto anayedaiwa kulawitiwa mara moja tu kwani yeye bado ni
mgeni.
Kwa mujibu wa dogo aliyedaiwa kuingiliwa, alikutana na
mchungaji huyo mwaka jana maeneo ya Stendi ya Banana-Ukonga, Dar ambapo
alimuomba na kumwambia kuwa alikuwa anatafuta mtoto wa kumfanyia
biashara ya mayai huko Majohe nyumbani kwake.
Alisema kuwa alikataa na kumwambia hawezi kwenda naye bali aende akazungumze na wazazi wake nyumbani.
Alisimulia kuwa baada ya hapo, aliongozana na baba mchungaji hadi kwa
wazazi wake ambapo walikubaliana kuwa kila mwezi atamlipa mshahara wa
shilingi 30,000.
Baada ya makubaliano hayo ‘dogo’ alisema kuwa
aliondoka na mchungaji na baada ya kukaa kwa muda mfupi huku akiendelea
na biashara ya mayai, mchunga kondoo huyo wa
Mungu alianza tabia ya
kumfanyia unyama huo huku akimdanganya kuwa atampa simu.
“Kuna wakati kweli ananipa simu kwa muda na kuninyang’anya.
“Kwa siku moja alikuwa ananiingilia mara mbili, asubuhi na jioni,” alisema mtoto huyo kwa uchungu.
Alisema kuwa baba mchungaji aliendelea kumfanyia ‘usodoma’ kwa muda mrefu.
Alisema baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wake, mama yake alimgundua na kumtaka kueleza ukweli.
“Nilimweleza baba na mama jinsi mchungaji anavyonifanyia ukatili,
walimwita nyumbani wakiwa tayari wameshaandaa polisi jamii, alipofika
aliwekwa chini ya ulinzi lakini aliwaomba msamaha polisi jamii hao
pamoja na wazazi huku akiahidi kutorudia tena.
“Kila mtu alikubaliana na msamaha na kumpa masharti kwamba afilisiwe vitu vyake vyote kama faini ya kosa.