Siku ya jana akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, mwanadada wema sepetu alipata nafasi ya kufanya interview na mtandao wa burudani wa bongo five.
Katika interview hii, wema sepetu ameongelea mambo mengi sana na
 makubwa yakiwema mapenzi, na maisha yake bunafsi kwa ujumla. Ifuatayo 
na sehemu ya interview hiyo kama iliyonukuliwa toka mtandao kwenye 
mtandao huo
Swali: Kuna wakati wowote uliwahi kujuta maisha ya ustaa baada ya kuwa Miss Tanzania?
Yes, nimewahi kujuta lakini mwisho wa siku huwaga nasema kwamba 
mwenyezi Mungu ndio anapanga kwasababu kama mwenyezi Mungu ndio 
amenipangia hivi nisingefika hapa kwanza, kwahiyo regrets zinatokea kwa 
kila mtu, lakini siwezi kusema kwamba zimetoka kwa mara nyingi, labda 
mara moja mara mbili na zinatokea pale tatizo linapotokea, hauwezi 
ukapata regrets kama hakuna tatizo.
Ukiwa staa kila mtu atataka awe rafiki yako, na kabla ya kuwa 
Miss Tanzania ni wazi ulikuwa na marafiki uliokuwa ukihang out nao hapa 
na pale, uliendelea kuwa na urafiki nao, ama baada ya kuingia maisha 
hayo ikakuwia vigumu kuwa nao tena pamoja?
Nina marafiki mpaka sasa ninahangout nao wanakuja mpaka nyumbani
 lakini hatushei sana zile common interests kama zamani because once 
upon a time tulikuwa tuko wote on the same rank. So nilivyokuwa nipo 
kwenye spotlight obvious nimekutana na watu wengine wapya watu ambao 
naonana nao katika kazi zangu za kila siku, because apart from being 
Miss Tanzania, I am also an actress, kwahiyo nakutana na wasanii wengine
 ambao labda nakaa nao kwa muda mrefu sana kwahiyo utajikuta tu unashare
 nao common interests sababu unafanya nao kazi pamoja.
Swali: Ulikuwa na boyfriend tayari?
Yes nilikuwa naye
Swali: Kuna wakati wowote aliwahi kujihisi inferior kutokana wewe kuwa maarufu? Ulifanyaje kumweka sawa?
Well, si unajua zile za kishuleshule, zile za kitoto naweza 
kusema. Sana sana ukishafika ile o-level nini utakuwa na yule boyfriend 
ambaye unaamka tu asubuhi umeshavaa unasema sasa hivi naenda kuonana na 
boyfriend wangu, ukisharudi kutoka shuleni from there nyumbani, no 
boyfriend. Yeah nilikuwa naye, in the beginning alivyojua kwamba 
nashiriki Miss Dar Indian Ocean akaniambia kwamba ‘ukishiriki mimi 
nisahau, sitaweza kuwa na wewe tena’, nikamwambia, why? Akaniambia 
‘utakuwa upo kwenye public’ nikamwambia ‘okay fine’, nikamdanganya 
kwamba sishiriki.
So siku moja gazeti la Mwananchi pale katikati kulikuwa na picha
 yangu kubwa ‘Miss Dar Indian Ocean kushindana kesho’ and lile gazeti 
kuanzia naingia shuleni naingia kila mtu ananiambia ameniona kwenye 
gazeti. So kitu cha kwanza nikafikiria ‘Mungu wangu yule mtu akiliona’ 
so sikuonana naye the whole day.
Nikiwa nyumbani ndio nikamuona anakuja kalishikilia, nikawa 
namsikiliza. Akaniambia, ‘nimeona gazeti lako and ndio hivyo kwahiyo 
umeshanidhihirishia kwamba umechagua hiyo issue, so fine we endelea’. 
Basi nikajaribisha kuongea naye lakini hakuweza kunisikiliza lakini 
luckily the next day wakati ndio nashiriki nimekaa pale time ya kujibu 
swali namuona pale anapiga picha kwahiyo he was there na alinisupport 
mpaka nilipofika Miss Tanzania lakini after that sababu nilikuwa 
ambassador wa Vodacom nikawa nafanya kazi Vodacom nikawa sionani naye 
vile kama kawaida, kila akinipigia simu nipo busy, yeye mwenyewe akasema
 tu ‘bwana mimi siwezi’. Basi tulielewana vizuri na mpaka kesho 
tunaongea, tunasalimiana’
Swali: Uwewahi kusema bila Kanumba usingeingia kwenye movies, marehemu alikuwa ana mchango gani kwako?
Nakumbuka nilipokutana na marehemu nilikuwa niko na dada yangu 
mimi nilikuwa nakaa na dada yangu, kwasababu once nilishawahi kuishi na 
mama yangu and then from there unajua baada ya kuingia kwenye nini nini 
nikawa busy. Dada yangu mimi kaolewa lakini kwa dada yangu nilikawa 
nahisi kama pako free zaidi, kwamba mama ukirudi ‘umetoka wapi sijui 
nini na nini hivyo, alikuwa haelewi. So ikabidi tu nianze kuishi na dada
 yangu.