Waziri wa Barabara na Ustawi wa Miji Iran Ali Nikzad ametangaza
rasmi uamuzi wake wa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini
na hivyo kufanya idadi ya waliotangaza azma ya kugombea kiti hicho kuwa
tisa.
Nikzad alitangaza uamuzi wake huo Jumamosi alipotembelea mji wa Ardebil ulio kaskazini magharibi mwa Tehran.
Uchaguzi wa 11 wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utafanyika
mwezi Juni na wagombea wote wanatakiwa kujiandikisha kati ya Mei 7 na
11. Rais Mahmoud Ahmadinejad anamaliza muhula wake wa pili na hivyo
kikatiba hawezi kugombea.
Kati ya waliotangaza kuwa tayari kugombea kiti
cha urais Iran ni pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya nje Manouchehr
Mottaki, manaibu spika wawili wa bunge Sheikh Mohammad Hassan
Aboutorabi-Fard na Mohammad Reza Bahonar.