Pasificus Cleophace Simoni akirudishwa ndani ya mahakama.
(Picha na Francis Godwin)
Na Francis Godwin, IringaSAKATA la mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limezidi kuchukua sura mpya baada ya askari waliomfikisha mtuhumiwa huyo wa mauaji askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) kumtibua hakimu na kuagiza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani kwa kudharau mahakama hiyo.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 5.35 asubuhi kwa askari hao watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja kumshusha kizimbani mtuhumiwa huyo wa mauaji na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo lilitokea mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo.
Huku bado mahakama ikiwa inaendelea kwa hakimu kutaja tarehe ya kesi hiyo ya mauaji namba 1 ya mwaka 2012 mtuhumiwa huyo alishuka kizimbani akiwa kavaa kofia ya sweta (mzula) na miwani ya nyeusi na kuanza kuondoka.