Friday, March 8, 2019
WASANII WA KIKE WA KIAFRIKA NA WA HIP HOP WAUNGANA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE
Johannesburg, 8 Machi 2019: Wakati dunia ikijiandaa kutoa heshima kwa wanawake duniani kote katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, chapa ya bia ya kibunifu zaidi Africa, Castle Lite, imeanza safari ya kusherehekea wanawake katika bara zima kwa kuwezesha ushirikiano mkubwa uliopata kutokea wa wasanii wa kike katika muziki wa Hip-Hop kwenye ardhi mama.
Lengo lilikuwa ni kuonyesha nguvu pale wanawake wanaposimama pamoja na kuimarisha umoja kwa kupitia muziki, hivyo chapa yetu ilishirikiana na kikundi cha wasanii wakubwa watano (5) wa muziki wa kufoka na kutengeneza tena nyimbo ya msanii malkia wa Hip Hop Queen Latifah iliyokuwa maarufu katika miaka ya 90 ya, U.N.I.T.Y.
Afrika ya Kusini, Tanzania na Nigeria kwa pamoja waliungana kutengeneza wimbo huu, huku wasanii kama Moozlie (South Africa), Gigi Lamayne (Afrika ya Kusini), Rouge (Afrika ya Kusini), Rossa Ree (Tanzania) na Mz Kizz (Nigeria) wakiwa nyuma ya kipaza sauti. U.N.I.T.Y kutoka Castle Lite ni zaidi tu ya “wimbo mwingine unaoshirikisha wasanii wa kike wa Hip-Hop”, ni wimbo wa kusherekea na wito, sio tu kwa wanawake wote barani kote bali katika kila sehemu ya dunia, kuweka uhai katika nguvu ya wanawake katika muungano.
Wasanii watano kwa wakati mmoja waliimba U.N.I.T.Y mubashara asubuhi ya leo katika Instagram; Jambo la kwanza kabisa kufanyika kwa Castle Lite na kwa bara zima la Afrika kwa ujumla. Akizungumza baada ya onyesho (livestream), Mkurugenzi wa chapa ya Castle Lite Silke Bucker alisema: “Msingi wetu kama Castle Lite kila siku umekuwa ni kuvuka mipaka kwa kutumia ubunifu, na ili kuweka kumbukumbu katika siku hii ya kipekee, hakukuwa na njia nzuri zaidi kwetu kuunganisha wanawake zaidi bali kwa kutumia jambo ambalo kiukweli tunalolipenda – muziki.”
“Mshikamano wa kimuziki katika bara zima ulifanya jambo hili la wasanii kuja pamoja kufanya wimbo pamoja na chapa yetu kuwa la asili, na Castle Lite imebahatika imeamua kuwaweka wanawake katika hip-hop mbele. Leo sote tunasherekea nguvu ya wanawake katika UMOJA na tunazidi kung’ara zaidi na kwa fahari kubwa tukisherekea na wanawake wote duniani kote katika siku hii ya kipekee na ya kimataifa,” Bucker alimalizia kusema.
“Ni hesima kubwa sana kuwa sehemu ya harakati ambazo sio tu kwamba zinasherekea na wanawake, lakini zinachochea UMOJA kwa kupitia muziki.
Muziki una uwezo wa kuunganisha watu kutoka katika mazingira tofauti, na ni kwa kupitia suala hili tuliweza kufanya jambo la tofauti kwa namna yetu ya kipekee ili kutengeneza wimbo huu mzuri ukiwa na ujumbe wenye nguvu.” Moozlie Aliongeza Mwaka jana, chapa hii yenye bia ya baridi ilivunja mipaka ya kimuziki ilipokuwa mwenyeji wa onyesho la kwanza na la kipekee la wasanii wa kike wa Hip Hop lililoitwa Hip Hop Herstory, ambalo lilijikita katika kuonyesha nafasi ya wanawake katika mabadiliko ya Hip Hop.
Onyesho la Hip Hop Herstory kutoka Castle Lite lilifanikiwa na baada ya kujifunza kutokana na hilo ilimaanisha kwamba ushirikiano wa U.N.I.T.Y sio tu kwamba ulikuwa na mantiki lakini pia ni hatua kwenda mbele katika kuonyesha na kutoa heshima kwa vipaji na michango ya wasanii wetu wenyewe kutoka Afrika.
Wednesday, March 16, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), David Mattaka Ashitakiwa Tena Kwa Uhujumu Uchumi
Mkurugenzi
Mtendaji wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka
na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka sita
yakiwamo ya matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kuisababishia
hasara Serikali kupitia ukodishaji wa ndege.
Wakili
Mkuu wa Serikali, Timon Vitalis akishirikiana na mawakili wa Takukuru,
Joseph Kiula na Stanley Luoga waliwataja washtakiwa wengine
wanaokabiliwa na kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage
kuwa ni Ofisa Mtendaji Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi
ya Umma (PPRA), Ramadhan Mlinga na Mwanasheria wa mamlaka hiyo, Bertha
Soka.
Wakili
Vitalis alidai kuwa Oktoba 9, 2007 katika ofisi za ATCL zilizopo
wilayani Ilala, Mattaka alitumia vibaya madaraka kwa kutia saini mkataba
wa ukodishaji wa ndege A320-214 iliyotengenezwa kwa namba 630 baina ya
Wallis Trading Inc na ATCL.
Husna, Mobeto ndani ya bifu zito
Husna Maulid.
Na Mwandishi wetu RISASI mchanganyikoDAR ES SALAAM: Bifu la chinichini linaendelea kuwatafuna warembo wawili ambao wote waliwahi kunyakua taji la urembo wa Miss Kinondoni kwa nyakati tofauti, Husna Maulid (pichani)na Hamisa Mobetto baada ya kudaiwa kumgombea bwana, ambaye ni raia wa DRC, aitwaye Mwami Rajabu.
Chanzo chetu makini kilisema kuwa Husna ndio wa kwanza kuanza kumtuhumu Hamisa kuingilia mapenzi yake na mtu wake huyo wa muda mrefu, kiasi cha kuanza kurushiana vijembe vikali mpaka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mpashaji wetu alizidi kuweka wazi kuwa wakati Hamisa akirusha vijembe, Husna mara nyingi amekuwa sio mzungumzaji zaidi ya kuangalia mchezo unavyokwenda huku akiwaambia baadhi ya marafiki zake hataki kumpa kiki mrembo huyo.
Hamisa Mobeto akiwa na Mkongo.
“Mara nyingi Mobeto amekuwa sio mtu wa
kuzungumza kabisa na kila wakati anawaambia marafiki zake kuwa hataki
kabisa kumpa kiki Husna kwa kumjibu chochote kile”
Gazeti hili liliwaendea hewani wasichana hao wawili, lakini Husna aliposomewa mashtaka yake alisema yeye Hamisa na mambo yake hivyo hawezi kumfuatilia.
Gazeti hili liliwaendea hewani wasichana hao wawili, lakini Husna aliposomewa mashtaka yake alisema yeye Hamisa na mambo yake hivyo hawezi kumfuatilia.
“Hamisa ana mambo yake bwana achana naye, ana mambo ya kisichana.”
Kwa upande wake, Hamisa alisema yeye anaona kama Husna ndio anamchokonoa, kwani yeye anajiheshimu na hayuko tayari kumpa mtu kiki kwa kugombana naye kwa vyovyote vile.
“Mimi sasa hivi ni mama na vitu vingi keshafanya huyo Husna, ila mimi
nanyamaza sipendi kumpa mtu faida maana mtu anapokuona una matatizo
ndio hapohapo anapotafuta sababu ambazo hazina maana,”alisema Hamisa.
Kwa upande wake, Hamisa alisema yeye anaona kama Husna ndio anamchokonoa, kwani yeye anajiheshimu na hayuko tayari kumpa mtu kiki kwa kugombana naye kwa vyovyote vile.
Thursday, February 25, 2016
Wadaiwa 16 Waliotorosha Makontena Bandarini Kuanza Kufilisiwa Leo
Wadaiwa
16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya
kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam
mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.
Mkurugenzi
wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia
wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella
alisema hayo Dar es Salaam jana.
Kevela
alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa
kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria.
Kevela
alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza
wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa
wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa
kulipa.
Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni
Alitaja
wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao
watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh
28,249,352.50, Strauss International (45,393,769.95), Farid Abdallah
Salum (52,185, 614.97).
Wengine
ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro
(64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem Abdul
(130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading
Co.Ltd (448,690,271.90).
Pia
wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff Tyres General Co Ltd,
(7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel
Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan
(68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah
Salem Sh 75,334,871. 85.
Akizungumzia
wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14 walizopewa na zikaisha juzi, alisema
wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza kulipa madeni baada ya kampuni
yake kuwafuatilia.
Steven Wasira Amkunja Shati Mwandishi Baada Ya Kesi Yake Kupinga Ushindi wa Ester Bulaya Kutupiliwa Mbali Na Mahakama
Mwanasiasa
mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia mpigapicha wa gazeti la
Mwananchi aliyekuwa akichukua picha zake wakati akitoka mahakamani,
lakini akashindwa kutimiza azima yake ya kufuta picha.
Wasira,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika wa Serikali ya Awamu ya Nne
(SA4), alifanya kitendo hicho akitoka kwenye jengo la Mahakama ya
Biashara ambako maombi yake ya kukata rufaa ya kupinga matokeo ya
uchaguzi wa ubunge, jimbo la Bunda yalitupwa na Mahakama Kuu.
Katika
kinyang’anyiro hicho cha ubunge, Wasira, ambaye amekuwa mbunge wa
Mwibara tangu mwaka 1970 na baadaye mbunge wa Bunda hadi mwaka 2015,
aliangushwa na Ester Bulaya wa Chadema katika uchaguzi wa Oktoba 25
mwaka jana. Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari akiwamo
walishuhudia tukio hilo.
“Wasira alimkimbiza Jamson akitaka kumnyang’anya kamera, lakini hakuweza,” alisema Nyange,mwandishi wa gazeti la Mtanzania.
“Baadaye alitaka kumgonga kwa gari lake wakati akiondoka lakini ikashindikana.”
Akisimulia
tukio hilo, Jamson alisema Wasira, ambaye amefanya kazi na serikali za
awamu zote tangu katikati ya miaka ya 70, alichukizwa na kitendo chake
cha kumpiga picha.
“Wasira alinifuata na kuniuliza sababu za kumfuatilia kila mara. Aliniuliza picha nazopiga nazipeleka wapi,” alisema Jamson.
“Njoo,
njoo hapa wewe kijana. Nakuambia futa hizo picha kwa usalama wako.Hivi
mnatafuta nini maana mnanifuatilia tangu nikiwa kule Mahakama Kuu hadi
huku Mahakama ya biashara,” alisema Wasira
Jitihada
za Wasira kumnasa Jamson ziliendelea hadi nje ya eneo la mahakama
ambako alimfuata kwa kutumia gari aina ya Toyota Land Cruiser (namba
tunazihifadhi).
Katika
kumfuatilia, gari la Wasira nusura limgonge mpigapicha huyo, lakini
waandishi wenzake walimnusuru kwa kumsukumia pembezoni mwa barabara.
Juhudi
za kumpata Wasira kuzungumzia sababu za kutaka kumshambulia mpiga picha
huyo kwa kuchukua picha za tukio hilo, hazikuzaa matunda.
Awali,
Jaji Sirilius Matupa alitupilia mbali maombi ya ruhusa ya kukata rufaa
dhidi ya uamuzi wa kufuta shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Bunda
baada ya kubaini waliowasilisha maombi hayo, Magambo Masato na wenzake
wanne, hawakufuata sheria.
Uamuzi huo ulisomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Eugenia Rujwahuka kwa niaba ya Jaji Matupa.
Katika
maombi yao ya msingi, Magambo Masato na wenzake waliiomba mahakama
kutengua matokeo yaliyompa ushindi Bulaya wakidai licha ya Wasira
kunyimwa haki kuhakiki na kuhesabu upya kura, mchakato wa uchaguzi huo
pia uligubikwa na vitendo vya rushwa.
Akisoma
maamuzi hayo kwa niaba ya Jaji Sirilius Matupa, Naibu Msajili wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Eugenia Rujwahuka alisema maombi hayo
yamewasilishwa kwa kutumia kifungu cha sheria kisichohusika.
“Badala
ya kuwasilisha maombi yao kwa kutumia kifungu cha 15 (c) cha Sheria ya
Uchaguzi Sura namba 141, waleta maombi wametumia kifungu cha 15 (a)
(b),” alisema Rujwahuka akimnukuu Jaji Matupa.
Wakati
huohuo, shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Nyamagana,
iliyofunguliwa Ezekiah Wenje, imesikilizwa jana na kuahirishwa hadi
Februari 29, mwaka huu.
Akiahirisha
shauri hiyo iliyoahirishwa mara mbili mfululizo Jumatatu na Jumanne
iliyopita, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kakusulo
Sambo aliziagiza pande zinazohusika kuhakikisha zinakamilisha taratibu
zote za kisheria ili shauri hilo lianze kusikilizwa mfululizo.
Donald Trump Azidi Kupeta Mchujo wa Kugombea Kiti Cha Urais Marekani
Mgombea
urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda katika Jimbo la
Nevada nchini Marekani, na kuzidi kuimarisha uongozi wake katika mchujo
wa kuwania tiketi ya chama hicho.
Tajiri
huyo aliyewahi kutamka hadharani kuwa atawafunga jela Rais
Mugabe na Mseveni, sasa ameshinda mara tatu, kufuatia ushindi wake
katika Jimbo la New Hampshire na Carolina Kusini.
Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili.
Maofisa
wa chama hicho wamesema wanachunguza ripoti za watu kupiga kura mara
mbili huku eneo moja likidaiwa kuwa na vifaa vichache vya kupigia kura.
Baadhi
ya wapiga kura pia walidaiwa kuvaa nguo zenye picha za Trump, lakini
maofisa wamesema kuwa hatua hiyo siyo kinyume na sheria
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson Anusurika Kifo Baada Ya Kupata Ajali
NAIBU
Spika Dk. Tulia Mwansasu, amepata ajali mkoani Mbeya alikokwenda kwa
ajili ya mapumziko. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Zainab
Mbussi, Dk. Tulia alipata ajali hiyo jana wakati akitokea Mbeya mjini
akielekea Kyela.
Mkuu wa wilaya alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Shule ya Sekondari ya Kipoke iliyoko wilayani humo.
Alisema
maelezo ya askari wa usalama barabarani, yanaeleza kuwa chanzo cha
ajali hiyo ni gari dogo lililoelezwa kuwa liliibeba familia ya mtu
aliyetajwa kwa jina moja la Chacha, lililokuwa likitokea Kyela kwenda
Mbeya, lilipojaribu kulipita lori na kukutana na gari la Naibu Spika.
Zainab
alisema Dk. Tulia, mdogo wake pamoja na mlinzi wake waliokuwa kwenye
gari lake wako salama ingawa gari hilo limeharibika vibaya sehemu za
mbele.
Aidha,
alisema baadhi ya abiria waliokuwa kwenye gari la Chacha wakiwemo
wanawe wawili walipata majeraha na walipelekwa katika hospitali ya
Mission Igogo, Kiwira.
Awali
mapema jana, Dk. Tulia, alitoa msaada wa sh. milioni tano, ili
kulifanyia ukarabati bweni la Mapinduzi, ambalo alikuwa analala wakati
anasoma Shule ya Sekondari ya Wasichana Loleza, iliyopo jijini Mbeya.
Dk.
Tulia ambaye alisoma shuleni hapo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha
nne, mwaka 1991 hadi 1994, pia alitoa msaada wa magunia mawili ya mchele
kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi.
Akizungumza
na walimu na wanafunzi, Dk.Tulia alisema ametajiwa changamoto nyingi,
zinazoikabili shule hiyo na kuwa amzichukua na kuahidi kutafuta wadau
atakaoshirikiana nao ili waweze kusaidia kuzitatua.
Wednesday, December 16, 2015
Kajala ajiachia na dada’ke diamond!
Mwigizaji Kajala Masanja akiwa na Queen Darleen wakiponda raha.
Na Musa MatejaHUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala na Queen Darleen wamekuwa ‘beneti’ kila kona ambapo pia kuna fununu kuwa hata familia ya Diamond imebariki uhusiano wake na Mbongo Fleva huyo na wanampa ushirikiano wa kutosha Kajala.
“Fuatilieni tu, Kajala ameshakubalika kwa kina Diamond, ndiyo maana leo utaona Kajala na dada yake Diamond, Queen Darleen wanapiga misele pamoja, hata katika viwanja vingi vya starehe wanakwenda wote,” kilisema chanzo hicho.
…..Wakifurahia jambo.
Mwishoni mwa wiki hii, paparazi wetu aliwanasa laivu Kajala na Queen
Darleen katika fukwe za White Sands, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
walipokuwa wameenda kupunga upepo na kuwapeleka watoto wao kuogelea.Kuonekana kwa wawili hao kuliibua gumzo la aina yake ambapo wafuatiliaji wa ‘ubuyu’ walionekana kunong’onezana kuwa yale waliyokuwa wakiyasikia na kuyasoma kwenye mitandao kuwa Kajala ana uhusiano na Diamond, yana ukweli.
“Itakuwa ni kweli Diamond anamiliki Kajala, juzikati niliona kwenye mitandao, nikajua ni uzushi lakini si kwa ubeneti huu wa leo na Queen Darleen. Si bure, Queen atakuwa anautendea haki ‘uwifi’ wake kwa kumpa kampani Kajala,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Ili kukamilisha ubuyu huo, mwanahabari wetu alimuibukia Kajala aliyekuwa ameambatana na mwanaye Paula pamoja na baunsa wake, ili aweze kuzungumzia ukaribu wake huo na Queen ambao umeleta tafsiri kuwa ni mtu na wifi yake. Kajala akafunguka:
“Queen (Darleen) ni mtu pekee ninaye muamini, hana maneno ya kuhamisha hamisha, hivyo ametokea kuwa mtu wangu wa karibu na ndiyo maana utaona kwa sasa nipo naye kila sehemu hakuna uwifi hapa. Tumekuja kupunga upepo na kumleta mwanangu kuogelea,” alisema Kajala.
Kwa upande wake, Queen Darleen alisema mwenye macho haambiwi tazama!
CHANZO: GPL
Friday, December 11, 2015
Rayuu afungukia kujiuza nje
Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
MAYASA MARIWATAMSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefungukia ishu ya mastaa wengi kupenda kwenda kujiuza nchi za nje ikiwemo Sauzi akisema kuwa, wanaofanya hivyo hawajitambui na kinachowasumbua ni tamaa ya pesa.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Rayuu alisema alishasumbuliwa na wadada wengi wakimpa madili ya kwenda kujiuza China, Sauzi na kwingineko lakini akawatolea nje kutokana na msimamo alionao
“Unajua hakuna kinachowapeleka huko zaidi ya tamaa kwa kuwa kule wanalipwa kwa dola wakirudi huku wakizibadilisha wanapata pesa nyingi, halafu huku unakuta mtu ameshatembea na wanaume wengi ndiyo maana anakimbilia nje,” alisema Rayuu.
Bodi ya Mikopo watoa awamu ya pili wanafunzi waliopata mkopo 2015/16
AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda
kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa
imetoa Awamu ya Pili ya waombaji 28,554 waliofanikiwa kupata mikopo na
kufanya idadi ya waombaji wenye sifa wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa
kupata mikopo hadi sasa kufikia 40,836.Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo.
Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (Bofya Hapa www.heslb.go.tz ) Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa ya kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016 wanapata mikopo na hivyo kupata elimu ya juu.
Aidha, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu na kupuuza taarifa zinazosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
09 November 2015
Paul Makonda azindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kutoka Global
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda (katikati) akizindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba
inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd. Kulia ni Meneja Mkuu
wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho na kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo.
Paul Makonda akigawa vipeperushi vyenye nyumba na zawadi nyingine zinazoshindaniwa kwa wanahabari.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd,
Abdallah Mrisho akiwakaribisha wanahabari na Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda katika uzinduzi wa Bahati Nasibu ya Shinda
Nyumba uliofanyika katika ofisi za Global zilizopo Mwenge, Bamaga jijini
Dar.
Wednesday, October 21, 2015
Mwalimu mkuu, mzazi wanaswa
Mwandishi Wetu
DUNIANI kuna mambo! Katika hali ambayo haikutarajiwa, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyopo Upanga jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita alinaswa live ofisini kwake akiwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mzazi wa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, kisa kikitajwa ni maandalizi ya kuivunja amri ya sita ya Mungu, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Tukio hilo la kufedhehesha, lilishuhudiwa na makamanda wa Global Publishers Kitengo Maalum cha Operasheni Fichua Maovu (OFM) ambapo pia watu wengine kadhaa walijionea kioja hicho cha mwaka.
HIVI NDIVYO ILIVYOANZA
Awali, Kamanda wa OFM akiwa kazini, alipokea simu kutoka kwa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, akimfahamisha juu ya hali isiyo ya kawaida kwenye ofisi za mwalimu huyo zilizopo ndani ya geti la shule, kwani aliwaona askari polisi wakihaha kama wanaotaka kuzuia uhalifu.
“Jamani OFM, njooni hapa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa. Kama kuna ishu, naona askari wapo na pia ndani kwa mwalimu mkuu kama kuna ishu. Sijui ni nini!” kilisema chanzo hicho.Mara moja, kamanda huyo alifanya mawasiliano na wenzake waliokuwa ‘fildi’ na kuwafahamisha kuhusu ishu hiyo. Wakitumia pikipiki zao ‘zinazopaa’, makamanda hao walifika eneo la tukio dakika chache baadaye na kukuta mambo ndiyo kwanza yanaanza.
Shilole atoboa siri tattoo ya Nuh
STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametoboa siri ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh’ akisema alifanya hivyo ili kumpa imani mwanaume huyo kuwa anampenda sana.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Shilole alisema siku zote mpenzi wake hakuwa akiamini kama anampenda, licha ya ukweli kwamba naye alikuwa amechora tattoo yenye jina lake.
“Nuh alikuwa haamini kama kweli nina mapenzi ya dhati kwake, niliamua kuchora tattoo ya jina lake na sasa ameamini nampenda, mapenzi yetu yameimarika kuliko mwanzoni, amejiona ni mtu muhimu sana kwangu, kwani hata mwanaume yeyote akiona nimejichora jina hili, lazima ashtuke na aone kwamba nina mtu tunayependana,” alisema.
Subscribe to:
Posts (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe