EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Shilole. Show all posts
Showing posts with label Shilole. Show all posts

Monday, August 3, 2015

Nuh Mziwanda amuomba penzi Wema!

Musa Mateja
YELEUWIII! Katika hali ya kushangaza, sauti ya mpenzi wa staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ inayosikika akimtongoza Wema Sepetu imemfikia Shilole na kusababisha azimie, Ijumaa Wikienda linakupa ‘ubuyu’ kamili.
BETHIDEI YA SHAMSA Tukio hilo lililozua mtafaruku lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kulipokuwa na pati ya bethidei ya mwigizaji Shamsa Ford.
TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kilishuhudia tukio hilo mwanzo-mwisho, saa chache baada ya kumalizika kwa shughuli ya kulishana keki, waalikwa walishangaa kumuona Shilole akiishiwa nguvu na kudondoka baada ya kusikiliza ujumbe wa sauti aliotumiwa kwenye simu.“We acha tu. Ilikuwa balaa. Watu tulikuwa katika shamrashamra ya kulishana keki, ghafla tukashangaa mwenzetu anaishiwa nguvu na kuanguka,” kilieleza chanzo.
nuhumziwanda.pngStaa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,  akiwa na mpenzi wake wa sasa Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
UJUMBE ULISEMAJE? Chanzo hicho kilitiririka kuwa, ujumbe huo wa sauti ulisikika Nuh akimuimbisha Wema kwa maneno ya kimahaba. “Nuh kajipambanua ileile. Kaimbisha mistari yote ya kimahaba, utafikiri alikaririshwa. Alijitahidi kushusha vesi tamu ili  kumuingiza Wema kwenye himaya yake. Huwezi amini jamaa alizidisha mbwembwe kiasi cha kumwambia amkubalie kwani hamtaki Shilole tena. WEMA AMTOSA “Wema amesikika akikataa, akamwambia hawezi kuwa naye kwani ni shemeji yake na anamheshimu Shishi,” kilisema chanzo hicho.
wema 2Wema Sepetu.
SHILOLE AMFUATA NUH Chanzo hicho kilieleza kuwa, baada ya kuusikiliza ujumbe huo, Shilole alimfuata Nuh kwa ajili ya kumsikilizisha lakini Nuh alijibu ‘mbovu’ ndipo Shilole alipomuomba ufunguo wa gari waliyokwenda nayo, akarudi alipokuwa amekaa awali.
APOTEZA ‘NETIWEKI’ “Aliporudi alipokuwa amekaa, Shilole alijikuta akiishiwa nguvu na kuzimia ambapo Aunt Ezekiel na kina JB (Jacob Stephen) walipofanya kazi ya ziada kumpepea, huku wengine wakihangaika kummwagia maji kunusuru afya yake. “Walifanikiwa kumpandisha kwenye gari lake. Joto lilikuwa kubwa kufuatia hali hiyo maana kila mtu alishindwa kuelewa kilichotokea, hivyo Shilole, baada ya kuzinduka aliulizwa kilichomfanya azime ambapo aliwasikilizisha sauti hiyo kila mmoja akabaki ameduwaa,” kilieleza chanzo.

Monday, July 20, 2015

Penzi la Shilole na Nuh layeyuka

shilolee-3
Bongo Fleva na mwigizaji, Zuwena Mohammed a.k.a Shilole a.k.a Shishi Beiby na msanii mwenzake Nuh Mziwanda.
Na Saphyna Mlawa LILE penzi lililotikisa Bongo kati ya mwanadada mrembo ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na mwigizaji, Zuwena Mohammed a.k.a Shilole a.k.a Shishi Beiby na msanii mwenzake Nuh Mziwanda, limevunjika ghafla wikiendi iliyopita. Awali, Shishi Beiby alikuwa amekolea kimahaba kwa ‘serengeti boy’ huyo na kulikuwa na kila dalili kwamba watafunga ndoa lakini mrembo huyo ndiye aliyekuwa kwa kwanza kutangaza juzi kwamba amempiga chini Nuh.
SHILOLE390
...Wakifanya yao.
Wikiendi iliyopita, wapenzi hao waliokuwa wameshibana na kugandana kama kupe, walionyesha kwamba wameachana vibaya, baada ya kutumia mitandao ya kijamii kutukanana, kitu ambacho wengi walikiponda na kudai wanatafuta kiki kwa lazima. Championi lilipata taarifa hizo na kuamua kuwafungia kazi wote wawili na kuanza kumvutia waya Shishi Beiby ambaye alitoa ufafanuzi wa kile kinachoendelea kwenye uhusiano wao. nuhu Championi: Mambo vipi Shishi? Shishi: Mambo poa tu mzima wewe? Championi: Mi mzima aisee sijui kwa upande wako? Shishi: Niko poa pia. Championi: Vipi Ramadhani imeendaje? Shishi: Kwanza kabisa ninamshukuru Mungu kwani tumemaliza salama funga yetu, lakini pia kupitia Mfungo wa Ramadhani kuna mambo mengi ambayo nimejifunza ikiwemo, kuswali, kupenda amani, kusamehe pamoja na kuwa na hofu ya Mungu. MZIWANDA2340 Championi: Vipi imekuwaje tena mbona nasikia umeachana na kaka yetu? Shishi: Aisee ni kweli unajua Nuh ni mzinguaji, yaani licha ya kumsaidia lakini ananiletea ujinga daah! Acha afanye yake as longer as ni mwanaume na mimi ni mwanamke kila mtu atapata riziki yake mbele. Championi: Kwani tatizo ni nini, maana mlikuwa kimya wenyewe imekuwaje? Shilole: Kwa kweli mi siwezi kuzungumzia sana sababu ni mambo ya ndani kuachana naye ila we jua tu Nuh anazingua. Championi : Ok! Basi poa, nikutakie siku njema. Shilole: Asante na kwako pia. UJUMBE ALIOUTUMA SHILOLE KWENYE INSTAGRAM Shilolekiuno: Mwanaume hata umfanyie nini haridhiki lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakini mh! Nimejitahidi, nimehangaika ila sasa kama gari limewaka, akaaa babu weeh! Kanikuta na maisha yangu, wacha niendelee na maisha yangu, mimi na yeye baaaaaaasi #Gandalandizi. Alipotafutwa Nuhu alisema kwa kifupi: “Kuachana siyo jambo la kushangaza, kwa sababu wengi wanaachana na Mungu kapenda tuachane, kwa sasa nadili na kazi zangu tu.” MUDA MFUPI BAADAYE NUHU NAYE AKATUPA JIWE M ziwandanation: “Mwanaume wa kweli hukaa kimya, sibishani na upumbavu, mwanamke asiyeridhirika na kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa na kuvumilia mambo yote aliyonifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu, familia, wasanii wenzangu na wadau anaanza kunitukana mitandaoni for whaaat!!! mxeeeew mimi bado kijana na nina time ya kupata maisha yangu na mtu atakayethamini moyo wangu, nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari #Ashangedere. ALICHOSEMA SHILOLE ALIPOZUNGUMZA NA CHAMPIONI WIKI MOJA ILIYOPITA KUHUSIANA NA PENZI LAKE KWA NUH Jamani Nuh siyo mdogo ila ni mwili wake tu, lakini pia kama wanaona ni mdogo basi ni kwa upande wao na mtazamo wao, kama angekuwa mdogo mbona mimi ananiridhisha sana kwenye mambo yetu? Hakuna mfano, ndiyo maana tumetulizana.

Friday, June 26, 2015

NDOA YANGU NA NUHU ZIMEBAKI SIKU CHACHE TU – SHILOLE

3d99b__hhhklMwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuh Mziwanda.
Mpenzi msomaji tunakutana tena katika safu hii ambapo mastaa mbalimbali hujibu maswali kumi kikamilifu, leo tunaye mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye amefunguka mambo mengi alipokuwa akizungumza na Mwandishi Wetu IMELDA MTEMA. Ili kujua aliyoyasema endelea kusoma.
Ijumaa: Vipi kuhusu sakata lako la nguo kukuvuka ukiwa jukwaani limekuathiri kivipi?
Shilole: Halijaniathiri chochote hiyo ni kama mtu anapata ajali akiwa kazini.
Ijumaa: Wakati zile picha zilipokuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii, mpenzi wako Nuhu alilizungumziaje hilo?
shiloleNUH 
Shilole: Hakuzungumza chochote kwani tulikuwa pamoja siku ya tukio hivyo anajua nini kilitokea.
Ijumaa: Najua una wakwe, je, walipoziona hizo picha hawakumsumbua Nuhu na kuona kama unawadhalilisha?

Wednesday, March 18, 2015

DOKTA: SHILOLE MGONJWA!

Shani Ramadhani  na Chande Abdallah
DAKTARI mmoja bingwa wa saikolojia, Erick Mutchumbh, amesema tabia zinazofanywa na nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ zinaashiria kuwa ni mgonjwa aliyeathirika kisaikolojia na matatizo ya unyanyaswaji wakati wa utoto wake.
Nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Mutchumbh alitoa maelezo hayo baada ya kuombwa kuzungumzia tabia za Shilole za kugombana mara kwa mara na mpenzi wake, Nuh Mziwanda, kama zinaweza kuwa ni tatizo la kisaikolojia linalomsumbua mmoja wao au ni ugomvi wa kawaida wa kimapenzi.
“Mtu yeyote aliyepitia matatizo hasa unyanyasaji akiwa mtoto ‘child abuse’ iwe kunyanyaswa kwa kubakwa, kupigwa, kunyimwa chakula au mateso ya aina hiyo, akikua bila kupata tiba ya kisaikolojia huwa na tatizo kubwa kwa miaka mingi akiwa mtu mzima.
“Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na kupenda kujitenga, hasira za karibu, tabia za ajabu na kubwa zaidi ni kumfanyia mtu mwingine hasa mtoto ukatili aliofanyiwa yeye kitaalamu wanaita ‘Propensity Victimization,’” alisema daktari huyo.
Nuhu Mziwanda.
Alisema katika nchi zilizoendelea, tatizo hilo hupewa kipaumbele katika matibabu kuliko ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika kwani madhara yake huwa ni pamoja na mwathirika kuamua kujinyonga au kuua.
Kwa maelezo hayo, mengi yanaonekana kufanana na matukio yaliyowahi kumkuta Shilole, kwani akiwa na umri wa miaka 14, aliwahi kubakwa, pia anatajwa kujihusisha kimapenzi na watu wenye umri mkubwa, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ngumu katika umri mdogo.

Thursday, January 1, 2015

SANDRA: SHILOLE USIDANGANYIKE NA PETE YA UCHUMBA

Staa wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’.
NA Mayasa Maliwata
STAA wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’ amemshauri msanii mwenzake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kupigania kuolewa na mwandani wake, Nuhu Mziwanda ambaye alimvisha pete ya uchumba siku chache zilizopita kwa kuwa kitendo hicho kwa sasa kimeshazoeleka.
Staa wa muziki wa mduara Zuwena Mohammed ‘Shilole’akivikwa pete na mwandani wake, Nuhu Mziwanda.

Wednesday, December 24, 2014

PETE YA SHILOLE YAIBUA MAZITO!


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ akiwa na bebi wake Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
Stori: Waandishi Wetu
JAMBO limezua jambo, saa chache baada ya mwanadada mtafutaji kunako tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kuvalishwa pete ya uchumba na mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ tayari watu wameanza kuisengenya.

Wednesday, December 17, 2014

SHILOLE: KUNA WATU WANATAMANI KUNIUA


Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye pia anafahamika kama Shishi Baby, amesema baadhi ya watu wana chuki naye kiasi kwamba wanatamani kumtoa roho kwa kutopenda mafanikio yake.

Monday, November 24, 2014

SHILOLE ATUA UBELGIJI KWA KISHINDO



  Furaha ilishika nafasi pale mwanadada shilole alipowasili uwanja wa kimataifa wa ndege wa Zaventem jijini Brussel.
 Msanii Shilole akiwa na furaha baada ya kupokelewa na wenyeji wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem jijini Brussel.
The Big Boss Mohammed akiwa na msanii Shilole muda mfupi tu baada ya kuwasili uwanjani Brussel.
 Msanii Shishi Baby Shilole akipata picha na mmoja wa sapota wake bidada Latifa.
 Chantel akiwa na msanii Shilole baby.

Thursday, September 25, 2014

SHILOLE: SIWEZI KUACHANA NA NUH

Na Shani Ramadhani KUFUATIA varangati lililotokea Tabora katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,  baada mpenzi wa mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,  Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kukataliwa na mashabiki, Shilole ameamua kufunguka kuwa Nuh atabaki kuwa mpenzi wake katika hali yoyote.
Mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na paparazi wetu, Shilole alisema lengo lake lilikuwa ni kumtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki wake japo walimkataa kuwa shemeji yao.

Thursday, September 4, 2014

SHILOLE: MPENZI WANGU NDIYE ANAYENITIBU VIZURI

Na Imelda Mtema
STAA wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefungua kinywa chake na kusema mpenzi wake wa sasa, Nuh Mziwanda ndiye anayemtibu vizuri kunako ‘sita kwa sita’ japokuwa watu wengi wamekuwa wakiudharau mwili wake.
Staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na gazeti hili bila kung’ata maneno, Shilole alisema wengi wanashindwa kujua kwamba mtu anaweza kuwa na mwanaume mwenye umbo kubwa lakini akawa hayajui mapenzi lakini mwenye umbo dogo kama Nuh, akawa ni bingwa wa mapenzi.
Akiendelea kumwaga data mbele ya kinasa sauti cha Amani, msanii huyo anayetamba na wimbo wa Nakomaa na Jiji alisema kuwa katika mapenzi, umri wala ukubwa wa umbo hauna maana yoyote.

Thursday, August 7, 2014

Nuh Mziwanda Na Shilole Waonyesha Penzi Leo Litadumu Zaidi Ya Miezi Kadha Waliyotabiriwa

Star Couple inayofuatiliwa kwa sasa ya Nuh Mziwanda na Shilole iliripotiwa kuvunjika hivi karibu imerudi kwa nguvu zaidi na kusambaza picha wakiwa pamoja kama ishara ya mapenzi yao kuongezeka zaidi. Nuh na Shilole wote waliweka picha instagram kuonyesha wamepatana na mapenzi yatadumu zaidi ya miezi kadha iliyotabiriwa.
Siku chache nyuma Nuh aligombana na Shilole mpaka kupelekea kupigana sababu ikiwa ujumbe mfupi wa maneno na missed call kwenye simu ya Shilole zilizokutwa na Nuh Mziwanda.
 Nuh Mziwanda Na Shilole 2 Nuh Mziwanda Na Shilole 3 Nuh Mziwanda Na Shilole 5

Wednesday, August 6, 2014

SHILOLE: YEMI ATAFIA UGENINI


IKIWA imesalia siku moja kuelekea Tamasha la Usiku wa Matumaini, Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa, diva kunako muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametupa kijembe kwa staa wa Nigeria aliyekuja kukinukisha Bongo, Yemi Alade kuwa amekuja kufia ugenini.Diva kunako muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

Saturday, August 2, 2014

SHILOLE LIVE CHUMBANI

KABANG! Picha za staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’ zinazomuonesha live akiwa chumbani tena kitandani kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda zimevuja, Risasi Jumammosi linazo kwenye makabrasha yake.
Staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Shilole, picha hizo walijipiga wenyewe wakiwa kitandani nyumbani kwa mwanadada huyo, Kinondoni jijini Dar.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha hizo walijipiga baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kabla ya hapo wasingefanya hivyo.
Katika picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa katika mahaba niue, Shilole anaonekana akiwa amemlalia Mziwanda ambaye naye amejiachia vya kutosha.
‘Shilole’ akipozi kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda.
Habari za ndani zinadai kwamba mmoja wa watu wa karibu alishika simu ya Shilole kisha akajifowadia picha hizo ndiyo chanzo cha kumfikia sosi wetu huyo.

Monday, December 23, 2013

SHILOLE ALIZWA SIMU

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ hivi karibuni alimwaga machozi hadharani baada ya kuibiwa simu yake ya mkononi, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
 
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyemshuhudia mwanadada huyo akilia, tukio hilo lilitokea Jumapili baada ya Shilole kushuka kwenye gari lake na kumwachia fundi kwa ajili ya marekebisho ambapo alipanda teksi na kuelekea saluni, alipofika akajikuta hana simu.

“Shilole alilia kama mtoto mdogo kwani alikuwa anatakiwa kusafiri siku hiyohiyo usiku kwenda Uingereza, ikabidi aanze kufanya jitihada za kupata simu nyingine lakini kwa kuwa ilikuwa ni wikiendi, kazi ilikuwa ngumu kwake,” kilisema chanzo hicho.

Mwandishi wetu alipojaribu kumtafuta Shilole ili aeleze simu ilikuwa ya gharama kiasi gani, hakuwa akipatikana hewani mpaka gazeti hili linaenda mtamboni.
CHANZO NI GPL

Wednesday, July 24, 2013

SHILOLE MATATANI WIZI SIMU ZA DIAMOND.



STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.

Mfano wa aina ya simu anazo daiwa kuiba Shilole
Msanii huyo alikumbwa na kasheshe hilo Julai 19, 2013 nyumbani kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mori, Dar.
Siku hiyo Diamond alikuwa akifuturisha na aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa lakini nusura futuru iingie doa kufuatia zogo hilo.

ISHU ILIKUWAJE?
Ndugu wa Diamond aitwaye Majaliwa Majuto ‘
Q Boy’ alidai ndiye mwenye simu hizo. Alisema miezi kadhaa iliyopita, Shilole alikwenda nchini humo kufanya shoo ya muziki. Wakati wa kuondoka alimpa simu tatu, Ipad, Samsung Galaxy na Blackberry ili akifika Bongo ampe Diamond lakini msanii huyo hakufanya hivyo.

Monday, July 22, 2013

Shilole ndani ya beef la "kifo" na Sintah, kisa?.

Mwigizaji wa bongo movies na mwanamuziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamedi ama shilole ameingia katika beef la hatari na mwigizaji, blogger na mtangazaji wa kituo cha DTV Christine Sintah “Sintah”

CHANZO NINI?

Habari zinasema kuwa tatizo limeanza baada ya Sintah kuandika kwenye blog yake kuwa mwanadada Shilole kuwa hana Kipaji cha kuimba kama tunavyonukuu maneno yake hapa chini…
“…sasa J wake Lo na Shilole jamani hebu tuweni wakweli aiiiii nimesema kidogo kwa Lina anyway tusubiri collabo nahisi nitaenda kuingiza vocal maana my dada hatokosa kuniita nijionee mchiriku mix…”

SHILOLE AMJIBU…

“Nashangaa, sijawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah, anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani, ameshangaa watu wa Bongo kuwa na tabia ya kudharau muziki wa nyumbani na kubabaikia muziki wa Marekani wakati wenyewe hawana muda muziki wa hapa Bongo, anamchukia Sintah kwa kuongea kitu asichojua na kumponda yeye na Snura…”

“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu alikubali kufanya kazi na mimi, ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” anasema Shilole….

Saturday, December 22, 2012

PICHA NNE ZA SHILOLE AKITONGOZWA NA MMOJA WA WAIMBAJI WA KOFFI OLOMIDE.

MSANII wa sinema na muziki wa Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Desemba 16, mwaka huu alinaswa gizani akiwa amejiweka kimahaba kwa mmoja wa waimbaji wa mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Antoine Christophe Agbepa Mumba ‘Koffi Olomide’,

Tukio hilo lilitokea ndani ya Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar, ambapo Shilole alienda kwa ajili ya kushuhudia shoo ya mwanamuziki huyo.
Haikuweza kufahamika mara moja kama Shilole alimkubalia mshikaji huyo lakini wadakuzi wanadai baada ya shoo kumalizika, mwanamuziki huyo alimfuta tena Shilole na kuongozana naye hadi kwenye gari alilokwenda nalo pale ukumbini. 

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate