Musa Mateja
Aah! Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alijikuta akipigwa butwaa kufuatia kitendo cha mcheza shoo wake, Moses Iyobo ëMozeí na mzazi mwenzake, Aunt Ezekiel kuoneshana ‘mahaba nipeleke kuzimu’ hadharani, Risasi Mchanganyiko lilikuwepo kushuhudia.
Tukio hilo la Diamond kupagawishwa na mahaba ya wawili hao lilijiri usiku wa kuamkia Agosti 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni jijini Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Iyobo. Lakini kabla ya kufika kwenye tukio hilo, twende hatua kwa hatua.
MWONEKANO WA DIAMOND UKUMBINI
Akiwa kwenye sherehe hiyo iliyojazwa pia na mastaa, muda mwingi Diamond alionekana mwenye furaha ya hali ya juu kufuatia mishemishe za bethidei hiyo iliyoandaliwa na Aunt kama moja ya kumshtukiza ‘sapraizi’ mpenzi wake huyo.
Habari zinasema mpaka Iyobo anaingia ukumbini hapo alikuwa hafahamu kama kuna sherehe ya kuzaliwa kwake.
Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kabeba keki.
MUDA WA MSHTUKO
Iyobo alizama ukumbini hapo saa 7 usiku kwa kuitwa na Aunt. Aunt pia ni staa wa sinema za Kibongo.
Baada ya Iyobo kuingia ukumbini alipata mshtuko kufuatia Diamond na nyota wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kumkaribisha kwa kummwagia maji na vinywaji mbalimbali ambapo waalikwa wengine nao waliungana kumuogesha huku wakimwimbia ‘hepi bethidei tu yu.’
DIAMOND AFUNGUA SHAMPENI
Baada ya zoezi la kumkaribisha Iyobo aliyekuwa amelala zake nyumbani kwa Aunt kumalizika, Diamond alipewa chupa ya kinywaji aina ya shampeni kwa ajili ya kufungulia sherehe hiyo ambayo ilianza hapo.
Moses Iyobo akiwa kamkumbatia mpenzi wake Aunt Ezekiel.
DIAMOND ACHEZA HUKU NA KULE
Katika hatua nyingine, waalikwa walitumbua macho kumwangalia Diamond ambaye muda mwingi alikuwa akicheza tena kwa vituko mbalimbali.
ABEBA KEKI
Pengine ni kwa sababu ilikuwa bethidei ya mcheza shoo wake, kwani ulipofika wakati wa kupeleka keki mezani, Diamond aliibeba yeye hadi eneo husika kwa ajili ya ‘kulishania’.
MAHABA NIPELEKE KUZIMU SASA!
Sasa wakati Aunt na Iyobo wakiwa katika tukio la kulishana keki kwa mtindo wa mahaba nipeleke kuzimu (mdomo kwa mdomo), Diamond alionekana kushtuka na kuwatumbulia macho (angalia picha ukurasa wa mbele).