Moja kati ya madhumuni mawili makubwa ya tamasha hilo ni kukumbushana
umuhimu wa uzalendo wa dhati wa kudumisha amani, kurejesha matumaini
kwa Watanzania waliopoteza matumaini, kuipenda na kujivunia Tanzania.
Tunaamini kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete kuhutubia Watanzania, ameweza kutimiza malengo hayo kwa
kiasi kikubwa.
Tunapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mhe. Rais kwa kukubali kuacha
shughuli zingine na kujumuika nasi katika tamasha hilo na pia kukubali
kuzungumza na wananchi na hatimaye kuandika historia mpya ya kuwa rais
wa kwanza kuingia uwanjani kuanzisha mechi ya mpira wa miguu, kati ya
Yanga na Simba za wabunge kwa kupuliza filimbi!