EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Staa Wetu. Show all posts
Showing posts with label Staa Wetu. Show all posts

Friday, December 11, 2015

Rayuu afungukia kujiuza nje



8977c613656d96073d7015b7676fe2b1
Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
MAYASA MARIWATA
MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefungukia ishu ya mastaa wengi kupenda kwenda kujiuza nchi za nje ikiwemo Sauzi akisema kuwa, wanaofanya hivyo hawajitambui na kinachowasumbua ni tamaa ya pesa.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Rayuu alisema alishasumbuliwa na wadada wengi wakimpa madili ya kwenda kujiuza China, Sauzi na kwingineko lakini akawatolea nje kutokana na msimamo alionao
“Unajua hakuna kinachowapeleka huko zaidi ya tamaa kwa kuwa kule wanalipwa kwa dola wakirudi huku wakizibadilisha wanapata pesa nyingi, halafu huku unakuta mtu ameshatembea na wanaume wengi ndiyo maana anakimbilia nje,” alisema Rayuu.

Wednesday, October 21, 2015

Monalisa: Mwaka huu lazima nipige kura

Cdrisa4-1
Msanii wa filamu Bongo , Ivon Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’.
Mayasa Mariwata
ZIKIWA zimebaki siku tatu kuelekea uchaguzi mkuu, msanii mkongwe wa filamu Bongo , Ivon Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ amesema safari hii lazima apige kura, hata kama kutakuwa na foleni ya aina gani.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Monalisa alisema bila kujali ustaa wake, siku ya uchaguzi atapanga foleni hata kama ni kubwa ili kutimiza azma yake ya kumpigia kura kiongozi anayefaa kuiongoza nchi.
“Japokuwa nina hofu, lakini lazima nikapige kura hivyo nawaomba Watanzania wawe watulivu na kudumisha amani, wakubaliane na matokeo ili kuepusha machafuko yasiyokuwa na maana ambayo yanaweza kuyagharimu maisha yetu,” alisema Monalisa.

Wednesday, October 14, 2015

ROSE NDAUKA: SITAKI KUWACHANGANYA MASHABIKI

MWANADADA staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema hataki kujihusisha na harakati za siasa kwa sasa kwa vile anaogopa kuwachanganya mashabiki wake.
Mwanadada staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akipiga stori na gazeti hili, Rose alisema kwa kuwa yeye ni kioo cha jamii anayeelimisha kupitia kazi yake, alisema kujiweka wazi upande ulipo ni kuwagawa watu wake kitu ambacho asingependa kitokee.
“Wasanii wanaozunguka kwenye kampeni hawafanyi vibaya, lakini mimi siwezi na sikutaka kufanya hivyo ila kura nitapiga na kuhusu ni nani nitakayemchagua kuwa rais ni siri yangu,” alisema nyota huyo ambaye anakiri kuwa soko lao limeyumba.

Kampeni zambadilisha akili Johari


johari (1)
Sta wa sinema za kibongo, Blandina Chagula maarufu kama Johari.
CHANZO: GPL
BLANDINA Chagula maarufu kama Johari, ambaye ni mmoja wa wasanii wanaozunguka nchi nzima kuipigia kampeni CCM katika uchaguzi mkuu, amesema baada ya kutembea na kufanya kazi, amejikuta akiihamishia akili yake katika siasa.
johari (3)

Jokate, Kiba picha sasa zinaiva

Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwandani wake Ally Salehe Kiba wakikumbatiana.
MAYASA MARIWATA NA BONIPHACE NGUMIJE
MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwandani wake Ally Salehe Kiba, wamethibitisha kuwa wana maelewano mazuri (picha zinaiva) baada ya mwishoni mwa wiki kuonekana pamoja katika bonanza maalum la wanafunzi, lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lililojulikana kama Kidoti Bonanza liliandaliwa maalum kwa ajili ya kuthamini vipaji vya wanafunzi na ambalo lilihudhuriwa na madenti wa shule mbalimbali ambao pia walipata burudani kutoka kwa wasanii na makundi tofauti.
Jokate alikuwa jukwaani pamoja na msanii anayetamba na kibao cha Ni Yule, Hellen George ‘Ruby’ ambaye alishika kipaza sauti na kuwauliza madenti hao kama wanafahamu mtu aliyeimbwa na Kidoti katika kibao chake cha Leoleo ambao wote kwa pamoja walijibu kuwa mtu huyo ni Ali Kiba.

RAYUU: WANAUME WANNE WAMEINGIA MITINI


Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
MAYASA MARIWATA
NYOTA wa filamu Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amesema anajihisi kama mwanamke mwenye mkosi baada ya wanaume wanne alioshiriki nao mapenzi kuonesha nia ya kumuoa, lakini ghafla waliingia mitini na kupeperusha ndoto yake ya kuwa mke wa mtu.
Akipiga stori na gazeti hili, muigizaji huyo alisema umri wake unamruhusu kuolewa na anafanya kila njia ikiwa ni pamoja na kutii maelekezo yote ya mwanaume ili kumvutia aingie naye katika ndoa, lakini kinachomshangaza hubadilika ghafla na kumpotezea kabisa.
“Siyo siri naumia sana, huenda nimerogwa nisiolewe, mwanaume anajitambulisha hadi kwa wazazi na kuanza mchakato wa ndoa lakini baadaye anaingia mitini,” alisema Rayu

FLORA MBASHA AKIRI: MWANANGU SI WA MBASHA!

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
OHOOO! Kimenuka tena. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amesema mwanaye mdogo (jina linahifadhiwa) hahusiani hata kidogo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha huku akidai kuwa anamtambua mwanaume huyo kama mzazi mwenzake kwa mtoto mmoja tu (Liz), Risasi Jumatano linakupa zaidi.
Mtoto anayedaiwa kuibuwa mazito.
Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki, Flora alisema amechoshwa na manenomaneno yanayosemwa juu yake na Emmanuel na kwamba kama mumewe huyo ameamua kumwaga ugali, yeye yupo tayari kumwaga mboga.
Mwimbaji huyo alisema kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa anampenda mumewe na kwamba yupo tayari kuishi naye haikutoka moyoni, isipokuwa alifanya hivyo kwa huruma tu, kwa sababu mwanaume huyo ni mtu katili, mwenye roho mbaya na asiyemuogopa Mungu.
“Mtu mwenyewe alimtelekeza mtoto (Liz) kwa zaidi ya mwaka mmoja, ni mtu mbaya sana, sina mapenzi na Mbasha hata kidogo, ni afadhali niolewe na chizi anayeokota makopo kuliko kurudiana na mtu katili na mnyama kama huyo, namheshimu kama mzazi mwenzangu kwa Liz,” alisema.

Saturday, October 3, 2015

Wolper kufunga ndoa ya siri

Imelda Mtema
BAADA ya kuvishwa pete na mwanaume aliyedaiwa kuwa na mume wa mtu, raia wa Kongo, mwigizaji Jacqueline Walper ‘Wolper’ amesema kamwe watu hawatajua siku atakayofunga ndoa kwani amegundua watu wengi wana husda.
Wolper alisema anaamini kuwa siyo kila mtu ana mapenzi ya dhati kwake hivyo atafunga ndoa ya kimyakimya ndipo baadaye atafanya sherehe.“Siku hizi wanga wengi watu watashtukia nimeshafunga ndoa sherehe baadaye kwa wale ndugu na marafiki maana najua siyo wote wanaopenda jambo hili litimie,” alisema Wolper.

JB: Bora uigizaji kuliko ubunge

JB (2)Erick Evarist
MKURUGENZI wa Jerusalem Film Company, Jacob Stephen ‘JB’ ameweka wazi kuwa kamwe hafikirii kuwa mwanasiasa kwani sanaa inamlipa zaidi.
Akizungumza na mwanahabari wetu katika mahojiano mafupi, JB alisema kipindi cha nyuma ziliibuka tetesi kuwa huenda anaweza kuwa mwanasiasa lakini ukweli kutoka moyoni, sanaa inamlipa.
“Sanaa inanilipa, sifikirii kama ubunge au siasa kwa ujumla inaweza kunilipa kama sanaa ambayo naipenda kutoka moyoni. Labda nikupe mfano, kupitia kampuni yangu, nikizalisha filamu moja inatoa ajira kwa wafanyakazi wasiopungua 30, itatoa ajira katika maduka, machinga na sehemu mbalimbali zinazouzwa filamu.
“Sanaa imetoa ajira kwa wasanii Mil 10. Unafikiri hao watu wangefanya nini kama si sanaa?,” alisema JB.
JB aliongeza kuwa, kwa sasa anamuunga mkono mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli kwani mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete ameweka misingi mizuri katika sanaa.
“Kikwete ametusaidia kwa kiasi kikubwa kuitangaza sanaa yetu, amekuwa akishiriki katika shughuli zetu kitu ambacho kwetu sisi kina maana kubwa sana katika suala zima la kututangaza na ndiyo maana tunaunga mkono CCM na ukizingatia Ilani ya CCM ya uchaguzi huu, imetugusa moja kwa moja,” alimalizia JB.

Wednesday, September 30, 2015

Bela atafuta kiki kwa picha za utupu

ISABELA-(1)
Miss Ruvuma 2006, Isabela Mpanda.
KATIKA kile kinachoaminika kama ni kutafuta kiki, Miss Ruvuma 2006, Isabela Mpanda amepiga picha za utupu na kuzitupia katika mitandao ya kijamii akiwa katika pozi mbalimbali.
Rafiki yake mmoja (jina linahifadhiwa) aliyelinyetishia gazeti hili kuhusu uwepo wa picha hizo, alisema kwa jinsi picha hizo zilivyo ni wazi kuwa endapo sheria ya mtandao itafanya kazi yake, basi mrembo huyo atakuwa matatani.
Gazeti hili lilipowasiliana na Isabela baada ya kuziona picha hizo na kutaka kujua jinsi atakavyoshughulika na sheria ya makosa ya mtandao alisema; “Picha siyo kitu cha kunifanya nishtakiwe kwa sababu simtukani mtu, wala mavazi yangu siyo sababu ya kuchukuliwa hatua labda wanaopitia sheria hii wawe hawana kazi ya kufanya.”

Zari atumika kumdhalilisha Wema! Kisa kuzaa na Diamond

zarinah
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, akiwa na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’
Mwandishi wetu
WATU wabaya! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia watu wanaoasadikiwa kuwa ni wafuasi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, kutumia jina na picha ya mwandani wa sasa wa staa huyo, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumdhalilisha mpenzi wa zamani wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache tangu Zari, ambaye ni mjasiriamali maarufu aliyemzalia Diamond, amfanyie mwanaye Latiffah ‘Tiffah’ sherehe ya kumtoa nje kwa mara ya kwanza (Arobaini).
ZARI (1)
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
KIINI CHA UDHALILISHAJI
‘Kirusi’ wa kwanza kuanzisha udhalilishaji huo alijitambulisha katika mtandao wa Instagram kwa jina la Who is Boss ambapo aliweka picha inayomuonyesha Zari akiwa amembeba mtoto wake na Wema akiwa amembeba mbwa kisha kusindikiza ujumbe uliosomeka:
“Ukibeba mimba utalea mtoto na ukitoa mimba utalea mbwa.”
TIMU DIAMOND ZAMSHAMBULIA WEMA
Mara baada ya Who is Boss kuweka picha na ujumbe huo, wafuasi wa Diamond (Team Diamond) walianza kumshambilia Wema kwa kumkejeli na kumtukana matusi mazito yasiyoandikika gazetini.
Wafuasi hao walimtuhumu Wema kuwa alichezea ujana kwa kutoa mimba matokeo yake kwa sasa analea mbwa wakati mwenzake Zari ametumia ujana wake vizuri na ndiyo maana amemzalia Diamond.
wema (3)
Wema Sepetu ‘Madam’.

Jayjay nimeumizwa na mapenzi!

janethMAUMIVU niache! Msanii wa filamu ya Who Is My Child, Janeth Jackson ‘Jayjay’ amekiri kuumizwa na kulizwa na mapenzi mara kwa mara licha ya kuwa na muonekano wenye mvuto machoni kwa wanaume jambo linalomnyima amani ya maisha.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Jayjay alisema si rahisi kwa watu kuamini ukweli huo kutokana na uzuri wake wa umbo na sura, lakini ukweli ni kwamba hana furaha juu ya mapenzi kufuatia wanaume wengi kumtumia kisha kumkimbia bila kutimiza ahadi zao.
“Sina furaha na mapenzi, nimeumizwa sana na wanaume kila anayekufuata anakuahidi mambo mengi lakini akishatimiza haja zake anakimbia, kwa sasa sitaki tena mapenzi,” alisema Jayjay na kuongeza kuwa sasa anataka kujikita zaidi katika kazi.

Ndoa ya wastara, bond baada ya uchaguzi

WASTARA2GSASA imethibitika kuwa ndoa kati ya muigizaji nyota wa filamu Wastara Juma na Mtangazaji Bond Suleiman itafanyika mara baada ya uchaguzi mkuu ujao.
WASTARA-43Bond ambaye pia ni muigizaji, aliliambia gazeti hili kuwa wawili hao wameshafikia muafaka wa kuoana lakini Wastara yupo bize na kampeni, kwani baada ya kuanguka katika ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM, sasa anazunguka mikoani na Samia Suluhu ambaye ni mgombea mwenza wa John Magufuli jambo ambalo limesababisha washindwe kufanya maandalizi.
“Unajua Wastara amejiingiza kwenye siasa na mimi nataka akomae kwani itakuja kutusaidia baadaye ndiyo maana tumekubaliana kuahirisha ndoa mpaka uchaguzi uishe ndipo tutapanga tena,” alisema.

Thursday, September 3, 2015

RIYAMA LAIVU!

KANASWA! Staa wa filamu Bongo, Riyama Ally kwa mara ya kwanza amenaswa laivu na kijana aliyemtambulisha kama mwandani wake, akimtaja kwa jina la Idd Mwalimu Mzee, anayemzidi umri kwa miaka saba, Amani linaandika.
Staa wa filamu Bongo, Riyama Ally akiwa na anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.
‘Sapraizi’ hiyo ilitokea saa sita mchana Jumatatu wiki hii nyumbani kwa muigizaji huyo, Mabibo jijini Dar, akiweka wazi kuwa muda wowote kuanzia sasa watafunga ndoa, kwani anampenda kwa dhati mpenziwe huyo, aliyesema ni msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, akifanya Hip Hop.

ESTA KIAMA KUBADILI DINI!

Msanii wa filamu Bongo, Esta Kiama.
MSANII wa filamu Bongo, Esta Kiama amesema kuwa yupo mbioni kubadili dini yake ya Kikristo na kwenda kwenye Uislam kwa kile anachodai kuwa amejisikia tu.
Akichezesha taya na Amani, Esta alisema kuwa ameamua kubadilisha dini kwa matakwa yake mwenyewe na siyo kwa kulazimishwa na mtu yeyote.
“Muda wowote kuanzia sasa nitabadilisha dini kwa kuwa nimeamua na wala si kwa ajili ya kumfuata mtu yeyote maana najua wazi kabisa kuna watu wengine wanajua kutabiri vitu kuliko mimi mwenyewe nitakachokieleza,” alisema Esta.

Saturday, August 29, 2015

Mkopo noma! Mfanyabiashara atupiwa vitu nje, Nyumba yauzwa!

DSC_0594
Mfanyabiashara maarufu, Mohamed Majid Seif akitaharuki.
Boniphace ngumije
Mkopo noma! Mfanyabiashara maarufu, Mohamed Majid Seif, mkazi wa Mikocheni A, Kinondoni jijini Dar, ametolewa vitu ndani ya nyumba yake namba A35/210 baada ya kushindwa kulipa mkopo wa Sh. Milioni 210 aliouchukua kwenye Benki ya Boa (Bank Of Africa) mwaka 2011.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, katika tukio hilo lililojiri nyumbani hapo, Seif alikopa kiasi hicho cha fedha akiwa na wenzake, lakini baada ya kushindwa kulipa kwa muda wa miaka miwili kama makubaliano yalivyoonesha, wenzake waliingia mitini na kumuachia msala.
DSC_0486
Vyombo vikipakizwa kwenye gari.
Ilidaiwa kwamba, baada ya Seif kuachiwa msala huo, aliiomba Boa kumuongezea muda ili aweze ‘kuklia’ deni hilo lakini benki haikuwa tayari kutokana na makubaliano waliyoweka Aprili 18, 2011 kuwa zikizidi siku sitini (60) kwenye muda wa makubaliano ya mkopo, bila kulipwa kwa fedha hizo pamoja na riba nyumba iuzwe.
“Baada ya makubaliano kushindikana, benki hiyo ilitangaza kuipiga mnada nyumba hiyo kupitia magazeti ya kila siku ambapo siku ya mnada, ilinunuliwa na Mwanaiba Mohamed Mzee, mkazi wa hapohapo Mikocheni kwa Sh. Milioni 56,” kilisema chanzo hicho.
DSC_0499‘Ubuyu’ uliendelea kudondoshwa kuwa, Seif hakuridhishwa na uamuzi huo uliochukuliwa na benki hiyo, jambo lililomfanya kukimbilia kwenye Mahakama ya Ardhi na Makazi, Kinondoni kuomba kutenguliwa kwa mnada huo.

Thursday, August 27, 2015

Lulu amhenyesha Mboto ukumbini

IMG_1826
Haji Salum ‘Mboto akisaidia kulibeba gauni la Lulu.
DIVA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni amemhenyesha staa mwenzake wa filamu, Haji Salum ‘Mboto’ baada ya kumpa kibarua cha kulishika gauni lake lisiguse chini.
Tukio hilo lilitokea kwenye fainali ya shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT 2015) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo Lulu na Mboto walikuwa washehereshaji.
IMG_1779Katika hali iliyoonesha Lulu alikuwa ‘siriaz’ stejini alimsisitizia Mboto kila mara ahakikishe amelishika gauni lake vizuri na asiliachie.
“Mboto hapa kazi yako ni kulishika gauni langu kwa nyuma kila nitakapokuwa nawe na ole wako uliachie,” alisikika Lulu ambapo Mboto alitekeleza ombi la Lulu.

Friday, August 21, 2015

Ester, mke wa Dude wapatanishwa

ester-kiama
Bifu kwishnei! Wasanii wa filamu Bongo, Eva Dude na Ester Kihama, mapema wiki hii walikutana uso kwa uso katika Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki jijini Dar ambapo mmoja wa watu wao wa karibu aliwakutanisha ili kuwapatanisha.
Chanzo chetu cha kuaminika kilieleza kuwa, kukutana huko kumekuja kufuatia mke wa Dude, Eva kurudi kwao baada ya kupewa umbeya kuwa, ndoa yake inaingiliwa na Ester.
“Kama unakumbuka mke wa Dude alirudi kwao baada ya kuhisi mumewe (Kulwa Kikumba ‘Dude’) anatoka na Ester, ukatokea msuguano mkubwa lakini juzi usiku walikutanishwa na kumaliza tofauti zao,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Ester ambaye alisema: “Ni kweli nilikutanishwa na Eva, tulipatanishwa na kimsingi tumemaliza tofauti zetu, sasa roho imetulia maana si unajua tena maneno haya huwa yanatibua mambo!”

Thursday, August 20, 2015

Rose Ndauka: Nipo tayari kuolewa na yeyote!

rose_ndauka_2012.jpg
ROSE Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ amesema kama mwanamke aliyekamilika na mwenye kuhitaji heshima katika jamii, yupo tayari kuolewa na kuishi kama mama na mwanaume yeyote.

Akichonga na Amani, Rose alisema japo mume bora anatoka kwa Mungu na kwamba anangojea aliye chaguo lake, lakini amechoshwa na hali ya kuishi bila ndoa.
“Mimi kama mwanamke ninayetoka kwenye familia yenye maadili, inafika wakati natamani kuishi katika ndoa, natamani kuwa na familia yangu na mume wangu na kwa sasa akitokea yeyote, nikajihakikisha kuwa anavyo vigezo ninavyovihitaji, hakika niko tayari kuanzisha naye safari ya maisha,” alisema Rose.
Awali Rose alikuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ‘King Chiwaman’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na mwishoni mwa mwaka jana waliachana.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate