EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Rose Ndauka. Show all posts
Showing posts with label Rose Ndauka. Show all posts

Saturday, March 21, 2015

WALEMAVU WAMDONDOSHA CHOZI ROSE NDAUKA


Stori: IMELDA MTEMA
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibu alijikuta akimwaga machozi baada ya kutembelea shule ya watoto wenye ulemavu ya Salvition Army, iliyopo Kurasini jijini Dar.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Staa huyo akiwa na timu yake ya Rozzie Magazine, walibeba misaada mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta, maharage na sukari ambapo mara baada ya kufika kwenye ukumbi maalum uliotaarishwa kwa ajili ya kuzungumza na watoto hao, alishikwa na moyo wa huruma na kudondosha machozi.
Rose akiwa amebeba bidaa kwa ajili ya walemavu.
“Kuna kitu nimejifunza hata kama hatuna tunahitaji kuja kuonana na watoto hawa kuzungumza nao na kuwafariji hivyo hata wasanii wenzangu wanapaswa kufanya hivi kwani ni muhimu katika maisha yetu,” alisema Rose.

Saturday, January 17, 2015

ROSE NDAUKA AFUNGUKA KUTOMMISI MZAZI MWENZAKE

Mwigizaji wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Na Laurent Samatta/Risasi
KAMA kawa kama dawa, tunakutana tena katika safu yetu ya Sindano 5, kutokana na maombi mliyonitumia wiki iliyopita tulipoianza safu hii, leo tunawaletea mwigizaji Rose Ndauka ambaye wengi mlimpendekeza awepo katika safu hii.
Mahojiano kati yake na paparazi wetu yalikuwa hivi:
    •Paparazi: Rose Ndauka mambo vipi? Siri ya urembo wako ni nini maana kuna tetesi kwamba mkorogo ndiyo unaokufanya uonekane mzuri?

Thursday, January 15, 2015

ROSE NDAUKA AKATAA KUMSAMEHE MZAZI MWENZAKE


Na Laurent Samatta/Amani
DIVA wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa ya rohoni kwamba hatokaa amsamehe mzazi mwenziye, Malick Bandawe.Akizungumza na Amani, Ndauka alisema alishawahi kufuatwa na mzazi mwenzake huyo kwa lengo la kumuomba msamaha ili waendelee na mapenzi yao lakini hakuwa tayari kumsamehe.
Diva wa filamu Bongo, Rose Ndauka akiwa na mzazi mwenziye, Malick Bandawe.
“Kuachana tumeshaachana, kama kurudi huwa inatokea lakini kwangu sipo tayari tena kumsamehe, anaweza kutokea mtu mwingine wa kunipenda ingawa kwa sasa nahitaji kupumzika kwanza,” alisema Rose.
Rose na mzazi mwenzake waliachana mwaka jana huku wakificha sababu za kuachana kwao.

Thursday, January 1, 2015

ROSE MHANDO ATUMBUIZA NA KITUMBO


Stori: Mwandishi Wetu, Singida
BAADA ya kudaiwa kulipwa fedha na kuingia mitini kwenye matamasha mbalimbali, mwanamuziki ‘grade one’ wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando (pichani) amenaswa akitumbuiza jukwaani akiwa na ujauzito mkubwa.
Mwanamuziki ‘grade one’ wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando akitumbuiza.
Tukio hilo lililowashangaza watu wengi lilitokea Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Ilongero jimbo la Singida Kaskazini kulipokuwa na mkutano wa hadhara aliokuwa akiuhutubia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Saturday, December 6, 2014

ROSE NDAUKA AWATEGA WATU KUCHUMBIWA

MTOTO mzuri Bongo Movies, Rose Ndauka amewatega mashabiki wake kwa kutupia picha ya kidole chake chenye pete ya uchumba kwenye mtandao wa Instagram kuashiria kuwa amechumbiwa.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Rose Ndauka.
Mara baada ya paparazi wetu kuiona picha hiyo iliyozua mjadala mkubwa mtandaoni, alimtafuta Rose na kumtaka afunguke kama amechumbiwa upya baada ya kumwagana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe hivi karibuni. Msikie alivyojibu:

Thursday, December 4, 2014

MZEE AIBUKA, ADAI ROSE NDAUKA NI MWANAYE

MADAI! Mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Severin Daniel Ndauka amejitokeza katika Ofisi za Global Publishers na kudai kwamba, staa wa sinema za Bongo, Rose Donatus Ndauka ni mtoto wa kaka yake ambaye alichukuliwa kutoka Tanga na kupelekwa jijini Dar.
Mzee Severin Daniel Ndauka anaedai kuwa Rose Ndauaka ni mwanaye.
Mzee huyo aliyekuwa akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, alisema mwaka 1979, shemeji yake, Nyazimbili au mama Godwin (anayedaiwa ni mama wa Rose) alijifungua mtoto wa kike katika Kijiji cha Sakura wilayani Pangani, Tanga ambapo kwa bahati mbaya mama huyo alifariki dunia hivyo mtoto kuchukuliwa na kanisa ambalo lipo Msimbazi Dar hakutaka kulitaja jina lililomlea mtoto huyo kwa kuwa familia haikuwa na uwezo.
“Baada ya hapo, hatupata taarifa tena lakini mimi niliamua kuja Dar kwa ajili ya kumtafuta Rose. Nilikwenda Msimbazi, nilipofika nikaambiwa Rose alichukuliwa na kituo cha kulea watoto kilichopo Kurasini. Ilibidi niende Kurasini, kufika nikaambiwa alichukuliwa na msamaria mwema kwa ajili ya kumlea kama mtoto wake.
Staa wa sinema za Bongo, Rose Donatus Ndauka.
“Tangu hapo hatukupata taarifa nyingine lakini baadaye dada yangu anaitwa Maria Ndauka akanipigia simu, akasema amemuona Rose kwenye televisheni akiigiza na marehemu Steven Kanumba ndiyo nimekuja hapa mnisaidie kumpata,” alisema mzee huyo.

Thursday, October 30, 2014

ROSE NDAUKA: SIFAGILII WANAUME TENA

Stori: Mayasa Mariwata
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema kuwa kwa sasa yupo bize na malezi ya mwanaye hivyo hana mpango wa kuwa na mwanaume yeyote hata awe pedeshee mwenye uwezo wa fedha kiasi gani kwani mwenyewe anajitosheleza.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kipindi hiki hafagilii kabisa mambo ya mabwana na wala hahitaji mapedeshee kwa kuwa yeye mwenyewe ana uwezo wa kujitosheleza kifedha. “Mimi sina bwana kwa sasa na wala sihitaji hao mapedeshee, watanisaidia nini wakati nafanya kazi zangu zinazoweza kuniingizia fedha, nina akili timamu, nina miguu na nina macho sasa kwa nini nitegemee pesa ya mtu?” alihoji Rose.
Kwa mara ya kwanza...

Monday, October 27, 2014

ROSE NDAUKA HAKAMATIKI

Stori: Musa Mateja
Acha kabisa!
Baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe kisha kurudi kwao, Kigogo jijini Dar, staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka anadaiwa hivi sasa hakamatiki hivyo hakauki viwanja.
Staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka akiinjoi uhuru wa kuwa 'Single' Viwanja.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ambalo limekuwa likimnyatia kwa ukaribu Rose unaonesha kwamba tangu ametengana na mwanaume huyo amekuwa huru kupita maelezo huku akionesha jeuri ya fedha kama ilivyokuwa kwa mastaa wenzake, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja.
Rose Ndauka akianza kukata mauno.
Pia uchunguzi huo ulibaini kwamba, mara tu baada ya kutoka ‘kifungoni’, Rose aliangusha bonge la sherehe ya ‘bethidei’ yake ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na ndiko alikoanza kuonesha jeuri ya fedha.
Rose Ndauka akimwagia midolari mtangazaji wa Times FM, 'Dida'.
Data zilionesha kwamba siku tishio ni ile ya Oktoba 18, mwaka huu ambapo Rose alikuwa kinara wa ushangiliaji wa timu yake ya Yanga, jambo ambalo siku za nyuma alikuwa hafanyi hivyo.
Siku hiyohiyo, baada ya kutoka uwanjani alikwenda kubadilisha mavazi yake ya njano na kijani kisha akatupia pamba za kuruka viwanja, akaibuka katika Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya Leader, Kinondoni jijini Dar.

Wednesday, October 15, 2014

ROSE NDAUKA HATAKI TENA MWANAUME


Stori:  Gladness Mallya/GPL
SIKU chache baada ya uchumba wake kuvunjika, msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka amefunguka na kusema kuwa kwa sasa haitaji tena mwanaume kwani anajikita zaidi katika kufanya kazi.
Msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Rose alisema katika maisha yake ya uchumba alijifunza mambo mengi na anamshukuru Mungu amempa zawadi ya mtoto hivyo anafanya kazi kwa bidii ili aweze kumlea mwanaye vizuri.
Alisema hajutii kwa yaliyomtokea kwa mchumba wake Malik Bandawe, kwani makosa yaliumbwa makusudi ili watu wapate kujifunza, hivyo akili yake kwa sasa anaiwekeza katika kazi zake za sanaa.

Thursday, October 2, 2014

WANAWAKE 2 WATAJWA KUVUNJA UCHUMBA WA ROSE NDAUKA

STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka ameanika ukweli kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mchumba wake Malick Bandawe baada ya kuwagundua wanawake wawili aliozaa nao mbali na yeye.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Rose aliamua kufungasha virago vyake na kurudi kwa mama yake mzazi maeneo ya Kigogo baada ya kugundua kwamba mchumba’ake huyo alizaa na wanawake wawili tofauti na yeye ambaye ni wa tatu.
“Alichokizungumza Malick kwamba alishamuweka chini Rose na kuzungumza naye si kweli, ila yeye Rose aliamua kurudi kwao baada ya kugundua jamaa ana wanawake wawili aliozaa nao kabla yake,” kilisema chanzo hicho.

Monday, September 29, 2014

ROSE NDAUKA MCHUMBA'KE WAACHANA!

Stori: Imelda Mtema Ooh…nooo! Wachumba wa muda mrefu, staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka na Malick Bandawe ambao maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakitawaliwa na msuguano wa chini kwa chini, hatimaye wameachana, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda mzima.
Staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini na cha uhakika kimemwaga data kwamba wachumba hao ambao walivalishana pete kwa mbwembwe miaka mitatu iliyopita huku wakipika na kupakua lakini wamekuwa katika mzozo wa muda mrefu wa kifamilia, ambapo mara kadhaa wameripotiwa kuchapana wameachana.

Wednesday, September 3, 2014

KICHENI PATI YA LUCY KOMBA MSHANGAO!

NI mshangao! Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya kiasili tofauti na matarajio ya wengi.
Staa wa filamu Bongo, Lucy Komba.
Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida, wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies walihudhuria.
Miongoni mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye magurudumu matatu (guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku miguuni.
Kwenye guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa nyasi juu, Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika nyungo ndogo kuashiria asili ya Mtanzania.

ROSE NDAUKA ASEMA UCHUMBA WAKE NGANGARI

Stori: Gladness Mallya/GPL MWIGIZAJI nyota wa filamu, Rose Ndauka ameibuka na kukanusha vikali uvumi uliozagaa kuwa uchumba wake na Malick Bandawe umevunjika na kusema siyo kweli kwani bado upo ngangari kuliko kawaida.
Mwigizaji nyota wa filamu Bongo, Rose Ndauka akipopzi.
Akistorisha na gazeti hili juzikati, mwigizaji huyo anayeishi na mchumba wake huyo, alisema uvumi huo hauna msingi kwa sababu asubuhi ya siku hiyo (Jumatatu) alikuwa amemnyooshea nguo alizovaa wakati akielekea kazini kwake.

Tuesday, August 19, 2014

ROSE MUHANDO AFIKISHWA POLISI

Stori: Mayasa Mariwata na  Makongoro Oging’
MWANAMUZIKI wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar baada ya mchungaji mmoja wa Kinigeria anayefanya shughuli zake nchini DR Congo,  Kabagambe Tchanda kumshitaki akidai kumlipa fedha ili akafanye onesho badala yake akaingia mitini.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando
Uchunguzi uliofanywa na Uwazi ndani ya jeshi hilo, umegundua kuwa kuna madai hayo na kwamba mchungaji huyo alitua jijini Dar na kufanya mazungumzo na Rose kwa ajili ya kwenda kutumbuiza nchini DR Congo, Julai mwaka huu katika mkutano uliohusisha wageni kutoka Ulaya na kukubaliana amlipe Dola za Marekani 5,000 (zaidi ya shilingi milioni 8).

Friday, July 11, 2014

ROSE NDAUKA AMKIMBIA MUMEWE, KISA MFUNGO


CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka hivi karibuni aliamua kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa Ramadhani ambapo sasa anaishi Kigogo na mama yake mzazi.
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka katika pozi.

Monday, March 31, 2014

ROSE NDAUKA: SIWEZI KUZEEKA

STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema licha ya kujifungua, kamwe hawezi kuzeeka kama wengi wanavyomtafsiri.
Rose alisema, kwa upande wake hata siku moja hawezi kumuunga mkono mtu anayesema kuzaa au kulea kunamfanya mtu azeeke kwani inategemea na jinsi mtu anavyojiweka.

Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
“Nawashangaa hata wasanii wasiotaka kuzaa wakiona kama watakuwa wamemaliza ujana wao, asikwambie mtu hamna kitu kizuri kama kuitwa mama, nimejitunza na nimezidi kuwa mrembo hata baada ya kuzaa,” alisema Rose.

Saturday, February 15, 2014

ROSE NDAUKA: NUSURA WATOTO WANIVUE NGUO

MWIGIZAJI mahiri Bongo, Rose Ndauka amefunguka kuwa amenusurika kuvuliwa nguo na watoto ambao walipandwa na midadi baada ya kumuona ‘live’.
 
Rose Ndauka.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika sherehe ya arobaini ya mwanaye iliyofanyika nyumbani kwao, Tandale-Tanesco, jijini Dar ambapo watoto hao walimvizia Rose alipotoka nje, walimvaa na kuanza kumng’ang’ania nguo.

“Hawakutegemea kuniona pale, wengi wamezoea kuniona kwenye TV. Daah nilipata wakati mgumu kidogo maana ilibaki kidogo wanivue nguo, lakini nashukuru Mungu niliwatuliza, wakanielewa nikarudi zangu ndani,” alisema Rose.

Sunday, February 9, 2014

MTOTO WA ROSE NDAUKA ASOMEWA KISOMO LEO,JIJINI DAR

Rose ndauka na Mchuma wake wakiwa na mtoto wao,Naveen Bandawe
 

PICHA: MTOTO WA ROSE NDAUKA ASOMEWA KISOMO LEO,JIJINI DAR

 Rose Ndauka na Irene Mwamfupe Ndauka katika picha ya pamoja.





 Rose Ndauka na mtoto wake wa kike Naveen Bandawe.
Msanii wa Filamu za kiongo Rose Ndauka amaye ni mwezi mmoja sasa na siku kadhaa tangu ajifungue mtoto wa kike Naveen Bandawe leo anasomewa kisomo 40 nyumani kwake kwa ajili ya kumuombea mwanae kwa Mwenyezi Mungu amkinge na kila lilio baya. IRENE JAMII blog tunamtakia maisha mema.




 
Mtoto wake wa kike Naveen Bandawe.

Monday, January 13, 2014

ROSE NDAUKA: KUZAA SIYO MCHEZO


WIKI tatu tangu ajifungue mtoto wa kike, staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amesema amejifunza tendo hilo siyo la mchezo na kugundua kuwa mama anapaswa kuheshimiwa.
Rose Ndauka.
Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Rose alisema kutokana na jinsi anavyohitajika kumhudumia mtoto, watu wote wanapaswa kumheshimu sana mama kwani kuzaa na kulea siyo mchezo.
“Mtu asikuambie kitu jamani, mama ni kitu kingine, nilivyozaa ndiyo nimeona mama ni kila kitu maana sasa hivi usiku silali kutokana na kumuangalia mwanangu,” alisema Rose aliyempa mwanaye jina la Naila.
CREDIT:GPL

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate