Kwa mujibu wa chanzo chetu, Husna ndiye aliyeanza kuwa na uhusiano na Mkongo huyo mwaka jana na kila anapofika nchini hutanua naye kwenye ‘viwanja’ mbalimbali.
“Husna ndiye mwenye mwanaume, akija Bongo wako wote, lakini hivi karibuni ghafla tu, jamaa kaja na kuwa na Wolper, Husna kapigwa chini, sijui Wolper alimpatia wapi?” kilisema chanzo hicho.
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimtafuta Husna na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alifunguka kwa kusema:
“Ni kweli kabisa, Wolper amenichukulia mwanaume wangu. Mi nimemshangaa sana. Halafu eti ananitumia meseji za ajabu ajabu mimi, eti anasema hajanichukulia bali ni bwana ‘ake siku nyingi (huku akionesha meseji hizo).
Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011, 'mlimbwende' Husna Maulid.
Baadhi ya meseji hizo zinaonesha Husna akijibu mapigo upande wa pili
huku akishambulia kwa maneno makali kufuatia madai kwamba anatembea na
Mkongo wake.