Mastaa wawili Bongo waliokuwa watangazaji wa Shindano la Kuibua Vipaji vya Kuigiza, Tanzania Movie Talents (TMT), Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Lucas Mhuvile ‘Joti’ wamezua balaa na kuwaacha hoi mashabiki waliohudhuria fainali za shindano hilo kufuatia aina ya viwalo walivyokuwa wamepigilia.
Mpango mzima ulijiri kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, wikiendi
iliyopita ambapo katika kuonesha ubunifu, mchekeshaji Joti, alitupia
vazi la jinsi zote ambalo upande mmoja lilionekana ni sketi ya kike na
mwingine suruali ya kiume.