Na Erick Evarist
Mshtuko!
Siku chache baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas
Zuberi Mtemvu ameibua mshangao wa aina yake kutokana na utata wa umri
wake, Ijumaa limesheheni data.
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akionesha cheti mara baada ya kuhitimu masomo.
Utata huo uliibuka saa chache mara baada ya shindano hilo kufanyika
Oktoba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo
wadau mbalimbali walianza kuhoji.
UTATA WENYEWE HUU HAPA
Mara baada ya mrembo
kutangazwa mshindi, habari za chini kwa chini zilidai kwamba Sitti
alijinasibu kuwa ana umri wa miaka 18 na elimu ya (digrii mbili)
(masters), mambo ambayo yaliwashtua wengi na kuanza kuhoji uhalali wa
umri huo ukilinganisha na kiwango chake cha elimu.
“Mh! Haiwezekani,
kama ana miaka kumi na nane atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na
miaka miwili?” Alihoji mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe
gazetini.
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akipozi.
ELIMU YA BONGO IKOJE?
Kwa mfumo wa elimu nchini
ulivyo, mtoto huanza darasa la kwanza akiwa na kati ya miaka mitano hadi
saba, jambo ambalo haliingii akilini kwa Sitti kwani hesabu zinakataa
hata kwa mtu asiyesomea mahesabu.
Ukiachilia mbali shule ya awali (nursery) ambayo huchukua kati ya
miaka miwili hadi mitatu, ukihesabu miaka saba ya elimu ya msingi
(primary), miaka minne ya sekondari (ordinary level), miaka miwili ya
kidato cha tano na sita (advanced level) na miaka mitatu ya shahada
kwanza (bachelor degree), jumla ni miaka 16.
Mlimbwende, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
Pia kuna madai kwamba ametumia mwaka mmoja kusomea shahada ya pili
(masters) huku kukiwa na muda ambao kwa kawaida huwa unapotea baada ya
kumaliza kidato cha nne kwenda cha tano na baada ya kumaliza kidato cha
sita kwenda chuo kikuu.
INA MAANA ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MIAKA MIWILI?
Kwa mantiki hiyo, kama kweli Sitti ana umri wa miaka 18, basi atakuwa
alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo ni msamiati
mpya kwa jamii ya Kibongo.
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akifurahia jambo na marafiki zake wa mamtoni.