Stori: Imelda Mtema/Amani
SIKU chache baada ya Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuweka picha zinazomuonesha mpenzi wake wa sasa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo.
Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo hicho, alimtaka Zari aendelee kumpenda Diamond, amgande kila idara ili isije kutokea akarudi kwa binti yake ambaye walimwagana mwishoni mwa mwaka jana.
“Yaani kama inawezekana naomba sana huyo Zari azidi kumganda Diamond, asimpe muda wa kugeuka nyuma kabisa ili mambo mengine yaendelee kwa sababu uhusiano wa Diamond na mwanangu haukuwa na baraka zangu,” alisema mama Wema.
Mama Sepetu aliongeza kuwa, hana maana ya kumchagulia mchumba mwanaye bali anahitaji mwanaume yeyote mwenye heshima na anayejiheshimu kwa sababu mwanaume asiyejitambua hawezi kuwa baba bora wa familia.
SIKU chache baada ya Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuweka picha zinazomuonesha mpenzi wake wa sasa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo.
Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Mzazi huyo ambaye ni fundi wa kuzungumza, alisema tukio hilo
limemfurahisha kwani anaamini ndoto za Diamond kurudiana na binti yake
zitakuwa zimeyeyuka rasmi kama alivyokuwa akimuomba Mungu siku zote.Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo hicho, alimtaka Zari aendelee kumpenda Diamond, amgande kila idara ili isije kutokea akarudi kwa binti yake ambaye walimwagana mwishoni mwa mwaka jana.