Jana kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha Clouds FM chini ya bwana
Sudi Brown ama Gossip Cop kulikuwa na fununu kali iliyokuwa inamuhusu
mwanadada wa bongomovies na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Young D '
Young Dar es salaam' kama mwenyewe anavyojiita ya wawili hao kukutwa
kwenye gari wakifanya lile tendo linaloruhusiwa kufanywa mara baada ya
mdada na mkaka kufunga ndoa.
Young D
Kwa mujibu wa Sudi Brown 'Gossip cop' wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezi beach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada lulu na Polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.