KUDAMKA KUPIGA DEKI KWENYE KORIDO WAKATI KUNA
WAGENI WAMELALA
NI jambo la ajabu sana, utakuta mwanamke amepata
wageni, ndugu wa mumewe wametokea kijijini. Kwa sababu sehemu ya kulala ni
finyu, mume anamwambia mkewe watandikiwe kwenye korido ndani walale maana
watakaa siku mbili au tatu tu.
Cha ajabu sasa, mke huyo anayeonekana ana busara
zake, anadamka saa kumi na moja alfajiri na kuanza kupiga deki hivyo kuwafanya
wageni waamke na kwenda kukaa nje kwa sababu ya maji, tena ya baridi maana ni
asubuhi. INAKERA SANA.
HII NAYO INAKERA
MKE KUULIZWA CHUMBANI, KWENDA KUJIBA SEBULENI
UTAKUTA mke wa mtu yuko na mumewe chmumbani,
anamuuliza ‘dear ni kwanini leo chakula kinanuka sana moshi?’ mke badala ya
kujibu kulekule chumbani, anatoka kama vile hajamsikia mumewe, akifika sebuleni
ndiyo anaanza:
“Si ungepika wewe kama unajua kupika. Moshi moshi,
wenzako Somalia wanatafuta chakula hata kinachonuka kinyesi hawakipati, acha
hizo.”
Inakera sana, ukizingatia sebuleni anakokwenda
kujibia kumepakana na dirisha la nyumba nyingine ya pili!