Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan Ni
pigo kubwa! Ile ndoa inayodaiwa kukaribia kufungwa kati ya nyota wa
filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Miss Tanga 2006 aliye pia msanii
wa filamu Bongo, Chuchu Hans imepingwa isifungwe mpaka mambo f’lani
yakae sawa.
Ray na Chuchu wakijiachia.
Kwa mujibu wa mtonyaji wetu, Ray na Chuchu wako mbioni kufunga ndoa
wakati wowote kuanzi Mei, mwaka huu, lakini mjadala mzito uliopo mbele
yao kwa sasa ni uhalali wake.
“Unajua wanachofahamu wao (Ray na Chuchu) wanaweza kufunga ndoa kwa ulaini kabisa, lakini ukweli ni kwamba kuna ugumu mkubwa.
UGUMU ULIPO “Kanisa analosali Ray, viongozi
wanasema wao si wa dunia hii mpaka wakubali kufunga ndoa ambayo mmoja wa
wahusika ana ndoa yake,” kilisema chanzo hicho.
Kikaendelea: “Kwa
hiyo kama wako tayari kufunga ndoa hiyo lazima Chuchu akubali kubadili
dini yeye ndipo ataruhusiwa kungia kanisani kufungishwa ndoa.”
Mtume na Nabii Onesmo Ndegi.
KANISA LA RAY Juzi Alhamisi,
Risasi Jumamosi
lilifunga safari hadi kwenye Kanisa la Living Water-Makuti Kawe, Dar
ambako mpaka mwaka uliopita magazeti pendwa yaliandika Ray anaabudu
huko.
Lengo la Risasi Jumamosi lilikuwa kuonana na
Mtume na Nabii Onesmo Ndegi lakini hakuwepo ofisini, ila msaidizi wake
mmoja alipopatikana alikiri kumfahamu Ray.
Msaidizi: Ray alishasali hapa, lakini sijamwona siku nyingi, sijui ana matatizo gani?
Risasi Jumamosi:
“Oke, tukiacha hilo la kutofika kwa siku nyingi. Lililopo sasa hivi ni
kwamba anataka kufunga ndoa na dada mmoja anaitwa Chuchu Hans ambaye ana
ndoa tayari, hajaachika na mumewe yu hai. Unasemaje kuhusu hilo?
Msaidizi: “Sisi hatuamini katika kuachana. Kama alishafunga ndoa na mume yupo hai, hao wametengana tu, lakini ndoa yao ipo.
“Huyo mwanamke alishajifunga, kifungo chake kitatenguliwa pale tu mumewe atakapoondoka duniani (kifo).
KANISA LA MTAKATIFU MAXIMILIAN KOLBE Baada ya
kuondoka kanisani hapo, mapaparazi wetu walikwenda Kanisa Katoliki
Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe, Mwenge, Dar es Salaam.
Risasi Jumamosi liliambiwa Baba Paroko hakuwepo kwa
wakati huo, lakini muumini mmoja aliyesema yeye ni mwalimu alipoulizwa
kuhusu nafasi ya Ray kufunga ndoa na Chuchu Hans alisema:
“Maandiko
yako wazi. Sasa kama huyo mwanamke ana mume wake tena mmesema yupo nje
ya nchi, siku akija si atamshika ugoni kwa mke wake?
“Huwezi kufunga ndoa kama bado una ndoa. Mungu hajaagiza hivyo. Ndiyo
maana sisi (Wakristo) huwa tunatoa siku ishirini na moja za kutangaza
ndoa ili kama kuna mwenye pingamizi ajitokeze na kulianika.
“Watu waongo siku hizi. Wapo wachumba wanakuja kuandikisha ndoa kumbe mmoja bado yupo kwenye ndoa halali.”
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
IMANI YA KIISLAM INASEMAJE? Mapaparazi wetu
hawakuchoka, walimtafuta Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi
Musa Salum ambaye kuhusu Ray na Chuchu kufunga ndoa alifunguka hivi:
“Kama Chuchu ni Muislam, itabidi Ray abadili dini awe Muislam, si vinginevyo.”
Risasi Jumamosi: Chuchu alifunga ndoa Bomani na mume Mkristo, ila yeye Muislam. Inakuwaje hapo?
S
heke Mkuu: “Itakubalika kama Ray atabadili dini tu, maana hiyo ndiyo ya Bomani, Kiislam siyo.”
Blandina Chagula ‘Johari’.
JOHARI, MAINDA WAPATANA ‘Johari’ ambaye ni
Blandina Chagula na ‘Mainda’ mwenye uhalisia wa jina la Ruth Suka
(zamani Mwanaid), wawili hao sasa ni mashosti wakubwa baada ya kuwa na
bifu la miaka 8 kisa kikitajwa kuwa ni ‘kaka mkubwa’ huyo (Ray)
kuwachanganya kimapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo, mastaa hao wanaotamba
kwenye filamu za Bongo kwa miaka mingi wameamua kumaliza tofauti zao
huku wengi wakitafsiri kuwa, wanashikamana kwa sababu ya kuumaliza
uhusiano wa Chuchu na Ray. Haikufafanuliwa.
Mainda.
MADAI MENGINE Pia ilidaiwa kuwa, Mainda aliamua kumaliza bifu na Johari kwa sababu mchungaji wake alimtaka kufanya hivyo.
“Niliwakuta kambini wakishuti filamu, Mainda akaniambia aliitwa
kushiriki filamu hiyo kama mpambaji, Johari yeye amecheza baadhi ya
vipande ndipo Mainda akamtaka mwenzake wamalize tofauti zao,” kisema
chanzo chetu.
Hivi karibuni, Risasi Jumamosi liliinasa picha
iliyotundikwa mtandaoni na Mainda akimwonesha yeye, Johari na Mtangazaji
wa StarTV, Sauda Mwilima.
Mainda aliisindikiza picha hiyo na maneno yaliyosema: “Nimejifunza kitu katika maisha, kusamehe.”
KAKA MKUBWA RAY Juzi, Risasi Jumamosi lilimpigia simu ya mkononi Ray lakini hakupokea. Akatumiwa meseji, hakujibu!
CHUCHU HANS Baada ya kusomewa mashitaka yote, alijibu kwa ufupi: “Sina cha kuongea.”
JOHARI
Johari naye hakupokea simu yake ya mkononi licha ya kuita kwa muda
mrefu na kukatika kisha kupigwa tena. Akatumiwa meseji, hakujibu!
MAINDA Na yeye simu yake iliita sana bila kupokelewa, akatumiwa meseji, hakujibu!
CHANZO NI GPL