Ashley Toto, Mrembo ambaye kwa sasa anaishi Ujerumani, ni muigizaji mpya wa filamu anayechipukia akiwa ughaibuni. Ashley tayari ameigiza kwenye filamu ndogo inayoitwa “MOYO WANGU;” mojawapo ya filamu za Kiswahili zinazotengenezwa nchini Denmark ili kuunganisha nguvu za kutangaza filamu na tamaduni za kiafrika nje ya bara la Afrika.
Hivi karibuni Ashley, ambaye ni mzaliwa wa Kenya, alikua nchini Denmark akitokea Ujerumani kwa ajili ya kuigiza kwenye filamu hiyo.