Kinyanganyiro
cha kumtafuta mnyange wa Kanda ya Ziwa kwa mwaka 2013, kimeteguliwa
usiku huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest baada ya Mrembo Lucy
Charles msomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo
wengine 17 waliojitokeza.
| Top 10. |
Mrembo huyo aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika
ukumbi wa Hotel ya Gold Crest baada ya kujibu swali kwa ustadi
lililouliza Ni changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Eshe Rashid na mshindi wa tatu ni Salsha Isdore
Vinara
watatu .katikati ni Lucy Charles mshindi wa Redd's miss Lake zone 2013,
kulia ni Eshe Rashid kutoka Mara na kushoto ni Salsha Isdore kutoka
Geita na wote watatu wanaenda ngazi ya taifa.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Eshe Rashid na mshindi wa tatu ni Salsha Isdore