LILE sakata la Miss
Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu kudaiwa kudanganya limeingia
ukurasa mwingine kufuatia ufukunyuku wa gazeti hili kubaini kuwa, miaka
25 ndiyo sahihi kwake.
Kufuatia ushindi alioupata siku ya shindano
la kumsaka Miss Tanzania 2014 lililofanyika Oktoba 11, mwaka huu ndani
ya Ukumbi wa Mlimani City, kuliibuka madai kwamba mrembo huyo
alidanganya umri.




