MWIGIZAJI na mwanamuziki mwenye mbwembwe nchini Hemed PHD
ametoa onyo kwa wanawake ‘wanaomsarandia’ wakitaka penzi lake wamwache
atafute maisha kwani huu ndio wakati wake.
Hemed PHD.
Amesema kitendo cha baadhi ya wanawake kuacha
shughuli zao na kuanza kumfuatilia wakitaka awe mpenzi wao kimekuwa
kikimkera sana hasa ikizingatiwa kuwa hakiendi sawa na utamaduni kwani
mwanamume ndiye anayetakiwa kumfuata mwanamke.“Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kwangu kukaa na namba moja ya simu kwani nikishaona nasumbuliwa sana huwa nalazimika kubadilisha ili kuepusha usumbufu,” anasema.
Anaongeza kuwa huwa anawatosa wanawake wanaomfuatilia kwa kuwa anaamini hawamtakii mema : “Ninahisi wengine wanataka kuniharibia tu, huwezi jua labda ni mbinu tu za kutaka kunipoteza kwenye ramani.”
Hemed anasema kipaumbele chake sasa ni kazi na ndiyo maana muda mwingi amekuwa haonekani au kusikika.




