EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Peniel Mgilwa ‘Penny’. Show all posts
Showing posts with label Peniel Mgilwa ‘Penny’. Show all posts

Monday, August 17, 2015

Penny agoma kuulizwa kuhusu mtoto wa Diamond

PENNY1.jpg
Aliyewahi kuwa mwandani wa staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mwingilwa `DVJ Penny’.
Yamekuwa hayo? Aliyewahi kuwa mwandani wa staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mwingilwa `DVJ Penny’ amegoma kuulizwa chochote kuhusu kitendo cha zilipendwa wake huyo kupata mtoto wakati yeye alidaiwa kukataa kumzalia.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Penny alifunguka kwamba, haoni kama kuna sababu ya kumzungumzia Diamond na mtoto wake (Tiffah) kwani walishaachana zaidi ya miaka miwili sasa.
“Jamani, huyo mtu kwa sasa hanihusu na sioni kama kuna sababu ya kumuongelea mtoto wake, anayepaswa kuulizwa mambo ya Diamond ni Zari, kwa hilo mnisamehe (no comments), nikiulizwa niulizwe mambo yangu tu,” alisema Penny.

Thursday, March 19, 2015

DIAMOND, PENNY MZOZO UPYA

IMEVUJA! Ile mimba ya aliyekuwa Mtangazaji wa Efm Radio, Penieli Mungilwa ‘Penny’ ambayo ilijulikana alipachikwa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ imezua mzozo upya baada ya kuvuja kwa madai mengine.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Chanzo makini kimeliambia Amani kwamba, tofauti na madai ya Diamond kwamba Penny alitoa mimba yake, lakini kumbe Diamond hakumpa mimba ila ilikuwa ni magumashi ya Penny.
SIKIA HII
“Hali ilikuwa hivi! Kutokana na Diamond kutafuta mtoto kwa muda mrefu, hasa kwa mpenzi wake wa nyuma Wema Sepetu kushindikana, ikabidi Penny atumie mbinu yake ili kufaidika na pesa za Diamond.
“Penny aliahidiwa na Diamond kwamba, kama atakubali kuzaa naye atamnunulia gari zuri, kwa hiyo kazi ikawa kwa Penny sasa, afanyaje?
“Siku moja Penny alimwambia Diamond kwamba amenasa, Diamond akafurahi sana, lakini kumbe Penny alishaenda kwenye hospitali moja kubwa iliyopo Kinondoni (jina tunalo), akaongea na nesi mmoja kwamba kama atakwenda na Diamond kupima mimba akubali kwamba anayo, lengo lake ni kupata gari,” kilisema chanzo hicho.
Mtangazaji wa Efm Radio, Penieli Mungilwa ‘Penny’ akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Saturday, March 14, 2015

KISA BWANA, PENNY ADAIWA KUNYWA SUMU

MTANGAZAJI maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amedaiwa kunywa sumu kufuatia kunyang’anywa bwana na shosti yake aliyefahamika kwa jina la Diana.
Mtangazaji maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Kwa mujibu wa chanzo, Penny na Diana walikuwa marafiki lakini wakatofautiana baada ya Diana kumteka akili mwanaume wa rafiki yake huyo na kumkoleza mapenzi hadi kufikia hatua ya kumtangazia ndoa.
“Diana kampagawisha mwanaume wa watu, jamaa akatangaza ndoa na hivi ninavyokwambia siku siyo nyingi Diana anaolewa hicho ndicho kikasababisha Penny apandwe na presha hadi kufikia hatua ya kunywa sumu, alikimbizwa hospitali, akalazwa lakini sasa ametoka anaendelea vizuri,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Penny ili kujua anazungumziaje habari hizo za kunywa sumu hadi kulazwa hospitali ambapo alikanusha madai hayo.
“Sijanywa sumu, suala la mimi kulazwa huwa linatokea sababu nasumbuliwa na pumu mara kwa mara,” alisema Penny.

Friday, February 13, 2015

PENNY: MCHUMBA NINAYE ILA NDOA SIYO LEO

Na Hamida Hassan/Ijumaa
Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Diamond’,  Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kusema kuwa anashukuru amepata mchumba ila suala la ndoa siyo la leo wala kesho.
Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Diamond’,  Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akipiga stori na Ijumaa juzikati, Penny alisema wengi wamekuwa wakitaka kusikia suala la yeye kuolewa baada ya kubainika ana mchumba lakini mwenyewe anasema hajafikiria hilo la kuitwa mke kwa sasa.
“Kwenye hilo la kufunga ndoa naweza kusema bado niponipo sana, yapo mambo yangu ambayo lazima niyakamilishe kabla ya kuolewa, ndoa si mchezo, kujipanga ni muhimu,” alisema Penny.

Saturday, December 27, 2014

DIAMOND HANA UWEZO WA KUMPA MWANAMKE UJAUZOTO!

 
 
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Penny.
BAADA ya kudaiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa alichoropoa mimba zake mbili, mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kujibu mapigo kwamba mwanamuziki huyo hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
 
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu.
CHANZO CHA YOTE
Akizungumza na GlobalTV Online kwenye ofisi za gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar, hivi karibuni, Diamond alifunguka: “Nilimpa (Penny) mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hospitalini tukapime, akaambiwa anayo…nikafurahi nikampiga na ndinga (gari) mpya siku hiyohiyo, nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.

Friday, December 19, 2014

PENNY: NATAMANI MTOTO, SINA WA KUZAA NAYE

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.
Penniel Mwingilwa.
Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa jana (Alhamisi) na gazeti dada la hili, Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi.

Saturday, November 29, 2014

PENNY: SIWEZI KUVUNJA USHOSTI WA WEMA, AUNT!

MTANGAZAJI  Bongo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa kamwe hawezi kuwagombanisha marafiki wa damu, Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel, baada ya yeye kuingilia urafiki huo. 
Mtangazaji Bongo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akiwa na Wema Sepetu.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Penny alisema kuwa anaamini kabisa kuna baadhi ya watu  hawapendi kuwa na urafiki zaidi ya watu watatu kitu ambacho siyo sahihi, yeye anaamini baada ya  kupatana na Wema hivi karibuni, watakuwa marafiki watatu.

Wema Sepetu akiwa na Aunty Ezekiel.
“Nafurahi sana tunapokuwa na kampani kubwa nashangaa wengine mpaka wanafikia kupigana kisa akiona rafiki yake ana urafiki na mtu mwingine, mimi napenda tuwe wengi ili tuweze kushauriana mambo mbalimbali,” alisema Penny.

Tuesday, November 11, 2014

Wema Na Penny Nikama Best Friends,Waanza Kutembeleana

Baada ya kupatanishwa jumamosi ya November 8 2014, Wema na Penny sasa wameamua kuonyesha wazi kuwa hakuna beef kati yao na mambo yote yako wazi. Penny ameonekana akiwa karibu na Wema nyumbani kwake hivi karibuni.
Wanasema ni ngumu kuwa mabinti wawili waliowahi kuwa na mahusiano na mwanaume moja kubaki marafiki, Ni kweli Hii ?

Saturday, July 12, 2014

PENNY ACHUMBIWA, AONESHA PETE YA UCHUMBA INSTAGRAM


Mtangazaji wa kipindi cha Genge cha EFM Radio, Penniel Mwingilwa 'VJ Penny'.
Penniel Mwingilwa amepost kwenye Instagram picha inayoonesha mkono wake wa kushoto ukiwa juu ya usukani wa gari ambao una pete katika kidole cha chanda.
“Mdogo hicho nini kwenye kidolee?? Kabla sijaanza kurukaruka kwa furaha,”amehoji mmoja wa followers wake.
“Hv kumbe ni kweli @vjpenny04 ume engage? Kuna sehemu nilickia, basi sawa hongera zako mpe hi @halimakimwana1,” ameandika mwingine.
“Mungu awaondoshee hasad za waja wenye chuki za roho,ameenRabilaallamin @vjpenny94@halimakimwana1, na Kama ukweli uko engaged mwanangu mie furaha tele hapa nasubiri invitation card yangu ya mr&mrs na tutakuja all the way from Uk kwa jinsi nilivyo na hamu nayolove u all wanawake wenye msimamo, “amechangia mwingine.
Katika maelezo ya picha hiyo, Penny amesema; “Road trip…site here we come… Cc @halimakimwana1.”

Saturday, February 1, 2014

PENNY; CHAGUA BEGA, CHAPA ILALE!

LEO nabonga naye mwanadashosti anayeuza nyago kwenye kichupa cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Nianze kwa kukupa gwala kiroho safi. Juzikati umefunguka kuwa umepiga chini kiaina malovee na Diamond, mzuka mwingi. Umetisha sana.
Mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Unajua laifu la malavidavi ndivyo lilivyo siku hizi. Mizinguo inakuwa mingi na wengi huwa wanatambua kuna taimu inafika unalazimika kupiga chini ili michongo mingine iendelee.
Nikiwa katika mingo zangu za kusaka chambi, nilipata bahati ya kuchonga na masela f’lani hivi ambao walikuwa wakizimikia penzi lenu, walipenda kuliona linakimbiza kitaa deile lakini wakasema umechagua bega sahihi, kubwaga manyanga kwa pisi.

“Ni uamuzi mzuri sababu mchizi akiwa hasomeki huna haja kufosi kingi wakati unaona hivihivi chombo kishaenda mrama, halafu mbona mtoto mwenyewe full mauzo, shepu anayo na ameumbika kinoma?” alifunguka mwana mmko.

Saturday, January 25, 2014

PENNY AZUNGUMZA UKWELI WA MAMBO

Penniel Mwingila 'VJ Penny'.
Mtangazaji na meneja wa vipindi wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mwingila 'VJ Penny' amesema kuwa yeye na mpenzi wake, staa wa ‘My Number One’, Diamond Platnumz, wamepeana nafasi ili kila mmoja kutafakari anachotaka maishani.
Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.
CHANZO BONGO 5

Saturday, December 21, 2013

DIAMOND,PENNY WAMWAGANA!

NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wamemwagana, Risasi Jumamosi limemwagiwa upupu.
Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ wakiwa pamoja katika pozi.
KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’ wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao aliliambia gazeti hili kuwa chanzo cha Diamond na Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’ kilianza kama utani.
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.
                                Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu.
“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?” alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa Diamond.

RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya gazeti hili kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa Diamond na Penny imebaki stori!

 SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima Haroun ‘ Halima Kimwana’ ambayo aliiandaa Diamond.
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.
“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi,” alisikika mmoja wa waalikwa katika sherehe hiyo.
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na paparazi wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa. Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba zake.”
                                                                Penniel Mungilwa ‘Penny’.
PENNY KIZIMBANI TENA
Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, gazeti hili lilianza na Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa ‘mzito’ kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
“Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini.”
                                               Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’. DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji yenye maelezo yote, hakujibu.

Thursday, November 14, 2013

DIAMOND, PENNY NI NDUGU...MAAJABU!

Maajabu! Jambo zito limefichuka kuwa mastaa walio katika uhusiano wa kimapenzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Penniel Mwingilwa ‘Penny’ ni ndugu, AMANI limepekua na kupata mkanda kamili.
Diamond kwa sasa ndiye mwanamuziki aliye matawi ya juu zaidi kuliko yeyote kwenye Bongo Fleva, akisumbua vibaya na kibao chake cha Number One wakati Penny akiingiza mkwanja kupitia utangazaji katika kituo cha Runinga ya Dar es Salaam ‘DTV’.

ISHU YABUMBURUKA!
Sosi wa karibu, ndani ya familia ya Diamond alinyetisha kwamba, Diamond na Penny ni ndugu wa damu lakini jambo hilo limefahamika hivi karibuni na hivyo wanahaha namna ya kuzima aibu hiyo.

Saturday, August 31, 2013

PENNY: YATASEMWA MENGI DIAMOND SIMUACHI



Baada ya hivi karibuni kuandikwa habari iliyoeleza kwamba nchini Kenya kuna demu aliyemzimikia ile mbaya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akiahidi kumpa penzi zito, mpenzi wa msanii huyo Peniel Mwingilwa ‘Penny’ ameibuka na kudai hatishwi na maneno hayo.

Saturday, June 22, 2013

IMEVUJA, MIMBA YA PENNY YACHOROPOKA

TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
 
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
 
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Risasi Jumamosi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate