Stori:Gladness Mallya-Global Publishers.
Unakumbuka zile habari za Wema Isaac Sepetu kununuliwa jumba la
kifahari na bilionea mmoja Kijitonyama, Dar? Sasa zimegeukia kwa staa wa
sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye naye kuna madai mazito ya
kuhongwa nyumba.
Ilikuwa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo gazeti hili lilipokea ujumbe mfupi wa simu ya mkononi ‘sms’ kutoka kwa chanzo chake.
HABARI ILIVYOANZA Chanzo: Hivi ninyi mna habari?
Risasi Jumamosi: Nyingi tu lakini kama una ya kwako itatufaa sana.
Chanzo: Kwa taarifa yenu Nisha kanunuliwa bonge la mjengo hapa
Kijitonyama karibu kabisa na Kituo cha Polisi cha Kijitonyama
‘Mabatini’.
Risasi Jumamosi: Nani kamnunulia?
Chanzo: Nasikia ni
bilionea mmoja mwenye fedha zake hapa Dar es Salaam, kainunua kisha
kamhonga Nisha kwa sababu ni mpenzi wake.
Risasi Jumamosi: Tunashukuru kwa taarifa, kaa mkao wa kula itaruka hewani mara moja baada ya upelelezi wetu.
RISASI LATUA KIJITONYAMA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilisaga soli hadi maeneo
hayo na kuanza kugonga geti moja baada ya lingine hadi lilipofanikiwa
kuinasa nyumba hiyo huku Nisha akiwa ndani kapumzika.
Msichana
aliyejitambulisha kuwa ni dada wa kazi au hausigeli kwa lugha laini
ndiye aliyetoboa siri kuwa ni kweli staa huyo yupo ndani na amehamia
mahali hapo muda si mrefu.
