STAA wa sinema za Kibongo, Irene Paul amejikuta akitofautiana
kauli na msanii mwenzake, Neema Ndepanya hivyo kutaka kuzichapa kavukavu
‘live’.
Shuhuda
wetu ambaye alilinusa sakata hilo a to z, alisema wawili hao walianza
kama utani kubishanabishana kabla ya kufikia hatua ya kutaka kuzichapa
ukweliukweli walipokuwa lokesheni.
“Walikuwa wakirekodi filamu ya
Kichupa maeneo ya Mbezi jijini Dar sasa ile utaniutani mara ghafla
wakashikana kiukweli ndipo mama Kawele alipoingilia na kuwaamua,”
alisema shuhuda huyo.
Credit: GLP
