YELEUWIII! Katika hali ya kushangaza, sauti ya mpenzi wa staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ inayosikika akimtongoza Wema Sepetu imemfikia Shilole na kusababisha azimie, Ijumaa Wikienda linakupa ‘ubuyu’ kamili.
BETHIDEI YA SHAMSA
Tukio hilo lililozua mtafaruku lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kulipokuwa na pati ya bethidei ya mwigizaji Shamsa Ford.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kilishuhudia tukio hilo mwanzo-mwisho, saa chache baada ya kumalizika kwa shughuli ya kulishana keki, waalikwa walishangaa kumuona Shilole akiishiwa nguvu na kudondoka baada ya kusikiliza ujumbe wa sauti aliotumiwa kwenye simu.“We acha tu. Ilikuwa balaa. Watu tulikuwa katika shamrashamra ya kulishana keki, ghafla tukashangaa mwenzetu anaishiwa nguvu na kuanguka,” kilieleza chanzo.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, akiwa na mpenzi wake wa sasa Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
UJUMBE ULISEMAJE?
Chanzo hicho kilitiririka kuwa, ujumbe huo wa sauti ulisikika Nuh akimuimbisha Wema kwa maneno ya kimahaba.
“Nuh kajipambanua ileile. Kaimbisha mistari yote ya kimahaba, utafikiri alikaririshwa. Alijitahidi kushusha vesi tamu ili kumuingiza Wema kwenye himaya yake. Huwezi amini jamaa alizidisha mbwembwe kiasi cha kumwambia amkubalie kwani hamtaki Shilole tena.
WEMA AMTOSA
“Wema amesikika akikataa, akamwambia hawezi kuwa naye kwani ni shemeji yake na anamheshimu Shishi,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu.
SHILOLE AMFUATA NUH
Chanzo hicho kilieleza kuwa, baada ya kuusikiliza ujumbe huo, Shilole alimfuata Nuh kwa ajili ya kumsikilizisha lakini Nuh alijibu ‘mbovu’ ndipo Shilole alipomuomba ufunguo wa gari waliyokwenda nayo, akarudi alipokuwa amekaa awali.
APOTEZA ‘NETIWEKI’
“Aliporudi alipokuwa amekaa, Shilole alijikuta akiishiwa nguvu na kuzimia ambapo Aunt Ezekiel na kina JB (Jacob Stephen) walipofanya kazi ya ziada kumpepea, huku wengine wakihangaika kummwagia maji kunusuru afya yake.
“Walifanikiwa kumpandisha kwenye gari lake. Joto lilikuwa kubwa kufuatia hali hiyo maana kila mtu alishindwa kuelewa kilichotokea, hivyo Shilole, baada ya kuzinduka aliulizwa kilichomfanya azime ambapo aliwasikilizisha sauti hiyo kila mmoja akabaki ameduwaa,” kilieleza chanzo.
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa na mashabiki wake.
Waandishi Wetu
Kufuatia kupigwa mwereka kwenye Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekiri kwamba kilichomponza katika kinyang’anyiro hicho ni skendo za ngono hivyo kwa sasa atakuwa makini ili asichafuke.
A photo posted by 👄wemasepetu👄 (@wemasepetu) on
Akizungumza na gazeti hili baada ya kupokelewa kishujaa na kuacha historia jijini Dar aliporejea kutoka Singida wikiendi iliyopita, Wema alisema mashabiki wake hawatamsikia tena na skendo hizo huku akiahidi kuibuka na bonge la ‘surprise’.
UMAKINI
“Shukurani zangu zipo palepale kwa mashabiki wote wanaonisapoti.
“Ninachowaahidi kwa sasa ni kuwa makini na skendo lakini pia kuna kitu cha kushtua nitafanya hivi karibuni ambacho kitaibua surprise (mshtuko) nzito kwa mashabiki wangu,” alisema Wema.
Mashabiki wakiwa na Wema wakati wa mapokezi.
TEAM WEMA
Katika mapokezi hayo ambayo gazeti hili lilikuwa mstari wa mbele, makundi ya mashabiki wake na yale ya Team Wema yalipeana taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kipenzi chao, Wema angefika Dar, Jumapili iliyopita ambapo taarifa zilisema kuwa walikutana kimyakimya na kuandaa mapokezi ya Madam.
Mishale ya saa 7:00 mchana ndipo Team Wema na mashabiki wake wengine walianza kumiminika maeneo ya Kimara-Baruti jijini Dar wakiwa na mabasi ya kukodisha, pikipiki na magari binafsi ambapo shamrashamra za kila aina zilifanyika.
KIBAO-KATA
Pia kulikuwa na ngoma ya Kibao-Kata, michezo ya pikipiki huku nyimbo za kumsifu Wema zikiimbwa.
Kama hiyo haitoshi, amshaamsha hiyo ilikuwa ikifanywa kila sehemu ambapo mastaa walikuwa wakitokea maeneo hayo kwa ajili ya kumsapoti Wema.
SHANGWE
Umati uliojitokeza walianza kulipuka kwa shangwe baada ya kumuona Meneja wa Wema, Martin Kadinda aliyeingia katika eneo hilo akifuatiwa na Petit Man ambaye alifuatana na wasanii wa Bongo Fleva, Mirror na Suma Mnazareti.
MJAMZITO
Mashabiki hao wa kila kada huku watoto wakifurika kumuona Wema walionekana kuwa na mapenzi ya hali ya juu huku mama mmoja mwenye ujauzito mkubwa akionekana akijichanganya kila kona bila kujali hali yake.
WEMA ENEO LA TUKIO
Wema aliingia katika maeneo hayo (Kimara-Baruti) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser ambapo alishuka na kuingia ndani ya BMW lililoletwa kumpokea ambapo alitokea kwenye paa na kuanza kusalimia mashabiki wake waliolipuka kwa furaha na wengine wakiangua kilio cha furaha.
MABUSU
Kuna wengine walishindwa kujizuia wakajikuta wakimfuata Wema wakimbusu na kumshika nywele zake kama vile siyo binadamu.
CHENI NA PETE
Wema alilazimika kugawa cheni na pete zake za dhahabu kwa mashabiki wake ili kuwatuliza huku akiwashukuru kwa kumpokea na kuwaaga kuwa anakwenda nyumbani kwake Kijitonyama ambapo msafara wake ulisababisha foleni ya zaidi ya robo saa njia nzima ambapo alikuwa akisindikizwa na pikipiki.
“Yaani Madam amepokelewa na watu kama rais vile, duh! Sijawahi kuona, amekosa ubunge lakini shamrashamra yake kama vile ameshinda!” Alisema mmoja wa mashabiki wa Wema aliyevalia fulana zenye nembo iliyoandikwa ‘Wema’.
KINACHOONEKANA
Habari zilieleza kwamba, kinachoonekana Wema anajipanga upya ili kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya baadaye hivyo atajitahidi kuwa mbali na skendo hasa za wanaume.
TUJIKUMBUSHE
Huko nyuma Wema aliwahi kuripotiwa kubadili wanaume mbalimbali wakiwemo; Jumbe Yusuf Jumbe, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na CK.
Deogratius Mongela, Chande Abdallah na Musa Mateja
Wema Sepetu alipokuwaakikabidhiwa fomu za kuwania ubunge viti maalum mkoa wa Singida leo mwishoni mwa wiki iliyopita.
DU! Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.
Aliyekuwa Mbunge wa Monduli na mmoja wa watia nia ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM walioenguliwa, Edward Ngoyai Lowassa.
Mafahari wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’.
Imelda Mtema MAFAHARI wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu
‘Madam’ wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo
kwenye mgahawa unaojulikana kama Snow Cream na kuchuniana kama vile
hawajuani.
Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kiliusoma ‘mchezo’ mwanzo mwisho,
Wema ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye mgahawa huo na wapambe
wake kisha baada ya muda kidogo kupita, Aunt pamoja na watu wengine nao
walifika na kukaa meza nyingine.
Aunt Ezekiel.
Habari zinazidi kudai kuwa baada ya Aunt kukaa, walitupiana macho na
Wema bila kupeana salamu ingawa Wema hakuwahi kumuona mtoto wa Aunt
tangu ajifungue.
HAKUNA mwanzo usiyokuwa na mwisho! Huu ni usemi pekee ambao umejidhihirisha kwa Mkurugenzi wa Endless Fame Production na mbunge mtarajiwa wa Viti Maalum mkoani Singida kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu baada ya kumwangukia aliyekuwa shostito wake, Kajala Masanja ‘Kay’.
MWISHO WA MATUSI?
Wema na Kajala wamekuwa na bifu zito lililokuwa likichukua sura mpya kila kukicha kufuatia wawili hao kutokusameheana, kutukanana na kukashifiana ambapo Wema alifikia hatua ya kumwita mwenzake ‘bogasi’ na yeye (Kajala) akamwita chizi.
Tukio la Wema kujishusha na kutoa kauli ya kusema yuko tayari kumsamehe Kajala aliitoa mbele ya mwandishi wetu, Julai 15, mwaka huu ndani ya Ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Miss
Tanzania 2006 na Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akipokea maelekezo
kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Bw. Alluu Ismaili Segamba
kwenye Mkutano uliofanyika Mkoani Singida wiki iliyopita.
Gladness Mallya BARAKA! Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri
kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea
ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka
mrembo huyo kwa uamuzi wake huo.
…Wema akipokelewa na Makada wa Chama cha Mapinduzi, CCM mkoani Singida.
Akistorisha na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule
ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti
maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.
“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza
ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM
mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu
barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza
kugombea,” alisema Nape.
Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama
hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki
kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka
2010.
Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha
ya Wema ni Ndumbagwe Misayo ëTheaà (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara
Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini).
Oscar ndauka LICHA ya kupatana,
habari ya mjini kwa sasa ni ugomvi mkali, wenye visa vya kushangaza
kati ya mastaa wawili wa sinema za Bongo, Wema Sepetu na Aunt
Ezekiel.Hii ‘kapo’ siku za karibuni, ilikuwa nzuri kwa maana ya urafiki
wao mkubwa.Urafiki wa Wema na Aunt ulianza pale Wema alipoutengua
urafiki wake na staa mwingine wa fani hiyo, Kajala Masanja.
Wema Sepetu akiwa na Aunt Ezekiel.
Kuna visa lukuki kuhusu chanzo cha ugomvi wa Wema na Kajala, lakini ‘kuchukuliana’ bwana ndiyo kulitajwa sana! Ikumbukwe kuwa, Kajala naye alirithi kijiti cha urafiki kwa Wema kutoka kwa msanii wa filamu na Mbongo Fleva, Snura Mushi.
TUREJEE KWA AUNT Katika urafiki ambao ulionekana ungedumu zaidi
ni kati ya Wema na Aunt kwa vile, Aunt alionekana kama mkomavu wa mambo
ya ukaribu kuliko wengine, Snura na Kajala.Sasa siku za hivi karibuni,
Magazeti Pendwa ya Global Publishers (ambayo huwa ya kwanza kufichua
mambo ya siri ya mastaa), yaliandika kuhusu uhasama ulioibuka kati ya
wawili hao chanzo kikiwa ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS ‘Nikifa usije kunizika, ukifa sitakuzika’! Ni maneno makali
sana kuyatamka kiasi kwamba, enzi za wahenga ilipotokea ndugu, marafiki
au majirani wakaapishana kwa maneno hayo, walitafutwa wazee wenye hekima
ili kuondoa laana hiyo.
Msanii wa sinema Bongo movie Aunt Ezekiel Grayson.
Sasa, hivi karibuni, baada ya kuvunjika kwa urafiki wa ‘kupika na
kupakua’ kati ya mashostito wawili walio katika tasnia ya Bongo Movies,
Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu maneno hayo yametumika pasipo
sababu, Ijumaa Wikienda lina kila kitu!
Wema Sepetu na Aunt Ezekiel.
AUNT BILA KUUMA MANENO Juzi, Aunt ameibuka na kutoa kauli kali bila kuuma maneno kwamba,
Wema akitangulia kuaga dunia, yeye hatakwenda kumzika kwa maana ya
kuuaga mwili wake sanjari na kuomboleza.
MAJANGA!
Wasanii wawili mahasimu katika tasnia ya filamu, Kajala Masanja na Wema
Sepetu ‘Madam’ wametengeneza tena vichwa vya habari baada ya kukutana
ndani ya klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzua minong’ono miongoni mwa wadau wengi
wa burudani, Risasi Mchanganyiko linakupa hatua kwa hatua.
Msanii wa filamu Bongo,Kajala Masanja akifurahia jambo.
Matukio hayo tofauti kwa wasanii hayo yalitokea ndani na nje ya
ukumbi huo katika shoo maalum ya kumchangia mke wa msanii Mabeste
Venus, Lisa Karl Fickenscher iliyowakutanisha mastaa wengi wa
‘category’ mbalimbali. SHUNGULI YAANZA VIZURI Shughuli nzima ilionekana kwenda vizuri,
isipokuwa mara chache ambako kulitokea vituo vya hapa na pale, ingawa
vingi kati ya hivyo vilisababishwa na baadhi ya wahudhuriaji kuzidiwa na
kilevi. WATENGANISHWA Wakati flani ‘usiku mnene’, Kajala alijongea kwenye
jukwaa maalum la waalikwa (V.I.P) kutoka kujichanganya kwa wadau,
ambako pia alikuwa amekaa Madam aliyeonekana kuzidiwa na ‘kiburudisho’. Akitambua wazi kuwa lolote lingeweza kutokea, Petit Man, mtu wa
karibu wa Wema, alimshika mkono na kumtoa eneo hilo, lakini muigizaji
huyo alipohoji sababu za kuondolewa ‘V.I.P’, aliambiwa kuwa hapakuwa
sehemu salama kwa wakati huo. KAJALA NDANI YA NYUMBA Kajala alionekana akijiachia kwa mapozi na
‘mihangaiko’ ya hapa na pale ikiwemo kucheza na kubadili vinywaji akiwa
sanjari na marafiki zake.Wakati wote, msanii huyo alionekana mwenye
furaha iliyoambatana na tabasamu na vicheko vya mara kwa mara jambo
lililotafsiriwa kama tayari alikuwa amepata kiburudisho cha kutosha. AKUTWA NA MKASA Mapambazuko yalipoanza kulivamia anga, Kajala na
‘kampani’ yake walitawanyika lakini wakati wakiwa nje ghafla jamaa mmoja
ambaye hakufahamika ‘aliwa-join’ na kuwachangamkia kusiko kwa kawaida
huku wao wakionekana kutompa ushirikiano aliouhitaji.
Wema Sepetu akiwa kwenye gari.
AMSHIKA MAKALIO Hata hivyo, jamaa huyo ‘alifika mbele’ zaidi kwa
kumshika makalio Kajala ambaye alimnasa kibao. Katika kujibu mapigo,
jamaa huyo alimpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha jeraha
usoni. Baada ya tukio hilo, marafiki wa pande zote mbili
walijitahidi kutuliza hali ya hewa iliyochafuka na kila mmoja akaendelea
na hamsini zake.
Pole sana mama! Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu
‘Madam’ amefunguka kuwa mama yake mzazi, Miriam Sepetu anasumbuliwa na
macho ambapo madaktari wamegundua kwamba amepoteza uwezo wa kuona kwa
asilimia sabini na tano (75%). Kwa
mujibu wa Wema, aliamua kumpeleka mzazi wake huyo hospitalini
(hakuitaja) ndipo alipohakikishiwa tatizo hilo ambalo limekuwa
likimsumbua kwa muda mrefu.
“Kumnusuru mama yangu asipate upofu wa moja kwa moja inabidi afanyiwe
operesheni ya macho,” alisema Wema kwa huzuni kwa kuwa hakuna kama
mama.
MASIKITIKO! Baada ya mrembo Wema Sepetu kutupia ujumbe kupitia
mtandao wa Instagram kuwa si kwamba hapendi kuzaa bali hana uwezo wa
kufanya hivyo mashabiki wake wengi wameonekana kuumizwa na taarifa hiyo.
Wengi wa mashabiki wameonekana kumpa ple Wema na kumtia moyo kuwa ipo siku naye atapata mtoto na kuitwa mama.
Wema aliamua kuandika ujumbe huo baada ya kushambuliwa na baadhi ya
mashabiki wasiomtakia mema alipompongeza mwanamitindo Hamisa Mobeto
aliyejifungua hivi karibuni.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
WAPENZI? Kwa mara nyingine Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu
amesababisha kichwa cha habari kufuatia kunaswa ‘live’ usiku mnene akiwa
na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan
wakioneshana vitendo vya ‘nakupenda tu’ mbele ya kadamnasi, Risasi
Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
NI ESCAPE ONE MIKOCHENI Wawili hao walinaswa wakioneshana mahaba
niue hayo usiku wa kuamkia Machi 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Escape
One, Mikocheni jijini Dar walipokuwa wamekwenda kushuhudia shoo kali ya
mpambano kati ya Bendi za The African Stars ‘Twanga Pepeta’ na FM
Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
PICHA LILIVYOANZA Awali, paparazi wetu aliyeamua kulivalia njuga
tukio hilo alimshuhudia Wema akiingia ukumbini humo akiwa sanjari na
kampani yake, akiwemo shosti wake mkubwa kwa sasa, Aunt Ezekiel na
mshauri wake kikazi, Petit Man.
Walikwenda kukaa kwenye viti vilivyokaribiana na kuanza kufuatilia
mpambano wa bendi hizo mbili kubwa nchini uliokuwa ukiendelea jukwaani
kwa kishindo kikuu.
Idrisakimweleza jamboWema Sepetu.
PETIT AKAA NA MADAM Kutokana na mpangilio wa watatu hao, Petit
Man alikaa katikati ya Wema (kushoto kwake) na Aunt, lakini muda mwingi
alikuwa akinong’onezana na Madam huyo huku wakionekana kuzungumza mawili
matatu yahusuyo mpambano huo unavyoendelea.
IDRIS NDANI YA NYUMBA Ndani ya dakika kama ishirini tangu Wema na
msafara wake waingie ukumbini humo, Idris naye aliwasili akiwa
ameongozana na mdogo wa hiari wa Wema aitwaye Bite pamoja na mtu
mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja. Nao
walikwenda walipokuwa wamekaa akina Wema.
ONA HII SASA Kuonesha kwamba itifaki inazingatiwa, Idris
alipofika mahali hapo, Petit alisogeza nyuma kiti chake na kuwafanya
Wema na Idris waweze kukaribiana na kuzungumza kwa ujirani zaidi.
Wakipozi kimahaba.
WAANZA KUNONG’ONEZANA Kitendo cha wawili hao kukaa karibu tu,
fasta walianza kuongea kwa staili ya kunong’onezana kwa muda mrefu,
wakati mwingine wakishikana mikono.Kuna wakati walikwenda mbali zaidi
hadi kufikia hatua ya kupapasana mapajani huku wakiendelea kuzungumza
maneno ambayo hayakuweza kusikika kwa sababu ya sauti ya muziki ukumbini
hapo kuwa juu.
POLE sana! Tatizo la kutoshika mimba (infertility) au kushindwa
kupata mimba (conceive) limekuwa likimtesa staa wa Bongo Movies,
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na limehusishwa na ugumba.
Akizungumza na Amani juu ya ishu hiyo hivi karibuni jijini Dar es
Salaam, Wema alisema suala la kutopata mtoto limekuwa likimkosesha amani
katika maisha yake ya ukubwani.
Staa wa Bongo Movies, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu.
ASHINDA AKILIA Alisema kwamba, amekuwa akishinda akilia kila
anapokutana na shosti wake wa sasa, Aunt Ezekiel ambaye ni mjamzito.Wema
alitiririka kwamba, kila wakati amekuwa akimwambia Aunt kuwa na yeye
anatamani kupata mimba lakini Mungu hajamjalia. Kwa kusema hivyo, huwa
wanajikuta wakikumbatiana na kuangua vilio wote kwa pamoja.
TATIZO UMRI UMEENDA Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mkali huyo wa
sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, mwanadada huyo
anaona umri umeenda sana kwani tayari ana miaka 26 sasa.
“Unajua Wema alishajaribu kupata mtoto mara kadhaa ikashindikana na umri
nao unakwenda hivyo lazima akose amani. Hebu fikiria aliwahi kuwa na
Kanumba (marehemu Steven), Jumbe (Yusuf), Chaz Baba (Charles Mbwana) na
Diamond (Nasibu Abdul) lakini kote huko alitoka kapa.
Lady jaydee.
YAMKUTA YA JIDE “Mbaya zaidi ni maneno yanayosemwa na watu
yanamuumiza sana, wanasema ni mgumba kama ilivyokuwa kwa Jide
(mwanamuziki Judith Wambura ‘Jaydee’).“Kwa kweli hali hiyo inamtesa sana
ila watu hawajui bora wakafunga vinywa vyao na kuacha kuandika kwenye
mitandao ya kijamii,” alifunguka mtu huyo wa karibu.
KATIKA
kile kinachoonekana kuwa ugomvi wao bado ni mbichi kabisa, nyota wa
filamu Bongo, Wema Sepetu Jumanne wiki hii akiwa ni mshehereshaji katika
sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtoto wa mtangazaji maarufu,
Zamaradi Mketema, aligoma kumtaja Kajala Masanja kama mmoja wa watu
waliotakiwa kula keki, Ijumaa lina mkanda kamili.
Staa anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Gladness Mallya STAA anayefanya
vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa
anatamani aone mastaa wawili ambao wana bifu kali, Wema Sepetu na Kajala
Masanja wanamaliza tofauti zao kwani maisha ni mafupi.
Wema na Kajala enzi wakiwa bado mashosti.
Akizungumza na gazeti hili, Aunt alisema kati ya mabifu ambayo
angependa yaishe ni la Wema na Kajala kwani wapo wasanii wamefariki
dunia wakiwa na bifu huku wale waliobaki ambao walikuwa na mabifu nao
wakitamani waamke walau mara moja wamalize tofauti zao lakini
haikuwezekana.
BAADA ya taarifa za mwigizaji Kajala Masanja kudaiwa kumuibia bwana
aliyekuwa shosti yake, Wema Sepetu kudumu kwa muda mrefu na kukosa
ushahidi wa moja kwa moja, hatimaye ushahidi wa SMS za mapenzi za Kajala
na bwana huyo wa Wema ambaye ni kigogo zimenaswa, Amani linakumegea
mchongo kamili.
Staa wa Bongo Movie, Kajala Masanja.
Chanzo makini kilichokuwa karibu na Kajala na kigogo huyo,
kilipenyeza habari kuwa kimefanikiwa kuzinasa meseji za Kajala kupitia
kwenye simu ya kigogo huyo ambaye alidumu katika penzi na Wema kisha
kumwagana baada ya Kajala kuingilia kati.
Musa Mateja/mchanganyikoMSANII
nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
amepatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuwepo madai ya kudaiwa kiasi cha
zaidi ya shilingi milioni 800 na serikali kupitia Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.
Msaniinyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
ILIKUWAJE? Mwishoni mwa wiki iliyopita, barua
inayodaiwa kuandikwa na mamlaka hiyo halali ya serikali, ilisambazwa
mitandaoni, ikielezwa kuwa ilikuwa imetumwa kwa meneja wa msanii huyo
ambaye kwa sasa ndiye yupo juu, ikimtaka kupeleka nakala za mikataba
yote ya muziki aliyoingia kwa ajili ya kufanya shoo, kuanzia mwaka 2010
hadi sasa. GUMZO MITANDAONI Baada ya kuwekwa kwa barua hiyo
mitandaoni, watu mbalimbali walitoa maoni yao walionyesha hisia
tofauti, baadhi wakipinga kwa madai kuwa wanamuonea huku wengine
wakisema siyo Diamond tu, bali wasanii wote wanastahili kulipa kodi
kutokana na mapato wanayopata kupitia kazi zao. KODI ZIPOJE KIBONGOBONGO? Mtaalam mmoja wa mambo
ya kodi aliyezungumza na Risasi Mchanganyiko, alisema kwa mujibu wa
taratibu zao, msanii huyo anastahili kulipa kodi kiasi cha asilimia kumi
ya fedha anazopata katika kila mkataba anaoingia. “Kuna walipa kodi wengine kama wafanyabiashara, hawa wanalipa kile
ambacho kitaalamu kinajulikana kama Capital Gain, yaani kulipa kadiri
unavyopata. Mtu anakwenda TRA mwenyewe na kueleza mapato yake na mamlaka
itampangia kiasi cha kulipa. Ila watu kama wasanii na wengine
wanaolipwa, wanatakiwa kutoa asilimia kumi ya malipo,” alisema mtaalam
huyo aliyekataa kutajwa jina gazetini. DIAMOND ANADAIWA SH. NGAPI?
Kama suala hilo litafanyika kwa mujibu wa mtaalam huyo, Diamond ambaye
malipo yake kwa shoo moja yanatajwa kuwa ni shilingi milioni 20 kwa
sasa, atatakiwa kulipa kiasi kinachozidi milioni 800 kutokana na hesabu
zilizofanywa na watu wanaofuatilia muziki wake.
Mwandishi Wetu/ijumaawikienda
Haya ni madai mazito! Mama mzaa chema wa staa wa sinema za Kibongo,
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu anadaiwa kumzaba vibao askari
wa kampuni binafsi.
Mama mzaa chema wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu.
UJIUNGE NA SHUHUDA Kwa mujibu wa shuhuda huyo,
tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi lilijiri kwenye Bandari ya Dar
es Salaam, majira ya mchana Ijumaa iliyopita.Kabla ya kushusha stori
kamili, Ijumaa Wikienda lilimhoji shuhuda huyo kama anamjua vizuri mama
Wema ambapo alithibitisha kuwa ni yeye huku akisapotiwa na wenzake
waliokuwa wakisikika kwenye simu.
HABARI ya mjini ni kwamba, lile penzi linalonadiwa
la Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mwigizaji Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ limejaa magumashi, ikidaiwa kuwa jamaa huyo kawekwa
kama boya tu, nyuma yake kuna kigogo mzito serikalini ndiye anayekula
vinono, Risasi Jumamosi limetonywa.
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akiwa na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Dimpoz ameagizwa na kigogo huyo
awe mpenzi kivuli wa Wema ili kuzuga watu wasishtukie mchezo kama yeye
ndiye anayesukuma gududumu la malovee kwa Madam.
STORI: Musa Mateja/Amani HABARI ya mjini ni kwamba, Beautiful Onyinye, Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumuumbua shosti wake wa zamani, Kajala
Masanja kwa kumwaga ‘ubuyu’ kwamba amefilisika baada ya kigogo maarufu
kama CK anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake, kuyumba kiuchumi, Amani
linakupa mchapo kamili.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kigogo huyo aliyewahi kuwa na uhusiano na Wema kisha kumwagana naye,
imedaiwa kuwa ile jeuri ya kununua magari ya kifahari, kumiliki biashara
mbalimbali mjini, kwa sasa ameangukia pua kwani hawezi tena
kujitutumua.