Yapo magonjwa mengi yanayoweza kutibiwa kwa juisi ya kitunguu, lakini katika mfululizo wa makala haya ya leo, nawaletea machache yafuatayo:
TATIZO LA KUTOKA DAMU
Kuna ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa, tatizo ambalo huwapata watu wengi hasa wale ambao huwa na matatizo ya kukosa choo kwa muda mrefu kutokana na ulaji mbovu walionao. Lakini pia tatizo hili huweza kuwapata pia hata wale wanaokula vyakula sahihi lakini hukaa muda mwingi bila kufanya mazoezi.
Kwa kitaalamu ugonjwa huu hujulikana pia kama ‘Hemorrhoids’. Wako ambao husikia maumivu makali na wako ambao hawasikii maumivu ingawa hutokwa na damu.
Kwa utafiti na ushuhuda mbalimbali uliokwisha tolewa juu ya tatizo hili, mtu unaweza kupona kabisa tatizo hili iwapo utaliwahi, kwa kunywa juisi ya kitunguu kwa utaratibu maalum.
JINSI YA KUANDAA
Awali ya yote, hakikisha unapata kitunguu halisi kilichotokana na
kilimo cha kawaida kabisa (Organic Faming). Natoa tahadhari hii kwa
sababu siku hizi kuna vitunguu kutoka China, ambavyo ni vikubwa na
vyeupe kuliko kawaida. Hivi ni feki, havina virutubisho asilia.