EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Jokate Mwigelo ‘Kidot’.. Show all posts
Showing posts with label Jokate Mwigelo ‘Kidot’.. Show all posts

Monday, August 17, 2015

Jokate amtambulisha Ali Kiba apigwa chini kwao

jokate ali kiba
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiwa na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
Musa mateja Imevuja! Gumzo la ndoa ya staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ inadaiwa kupigwa zengwe kama ilivyowahi kutokea kwa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufuatia madai ya mwanadada huyo kumtambulisha jamaa huyo kwao kisha kukataliwa. MINONG’ONO Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wawili hao walihudhuria kwenye harusi ya dada wa Jokate hivyo kuibua minong’ono kwamba huenda harusi inayofuata itakuwa yao. Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, habari mbaya ni kuwa baada ya Jokate kumtambulisha Kiba kwa ndugu, jamaa na marafiki baadaye kumpeleka kwao, wazazi wa mwanadada huyo walikuja juu wakidai jambo hilo haliwezekani huku sababu nne zikianikwa. jokate
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
KIGEZO CHA DINI Madai yalishushwa kuwa, sababu ya kwanza ni kwamba, familia ya Jokate hasa wazazi wake ni watu walioshika sana Dini ya Kikristo (Kanisa Katoliki) huku Kiba akiwa ni Muislam kama ilivyokuwa kwa Diamond aliyeshindwa kumuoa Jokate kwa kigezo hichohicho. NDOA ZA MASTAA NI TATIZO? Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’. KIGEZO CHA KABILA Kigezo kingine kilichotajwa ni kabila ambapo wazazi hao wanataka Jokate aolewe na mtu wa kabila lake la Wangoni tofauti na Kiba ambaye ni Muha. 2alikiba-1
Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
KIGEZO CHA BONGO FLEVA Chanzo kilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, wazazi hao wanaamini kwamba baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva ni wahuni hivyo kuwawia vigumu kukubali binti yao kuolewa na Mbongo-Fleva.Pia habari za ndani zilidai kwamba, Jokate na Kiba walikuwa kwenye harakati za kuoana kabla ya mwaka huu kumalizika ila zengwe limekuwa kubwa upande wa familia hasa kwenye suala la dini ambapo kila mmoja amekuwa akitaka mwanaye abadili dini. KAMA DIAMOND “Unajua kilichompata Kiba ni kama kile kilichomfika Diamond kipindi kile alipotaka kumuoa Jokate. “Ilikuwa ni ishu hiyohiyo ya dini maana wazazi wa Jokate walikuwa wakimwambia kila siku kama kweli anampenda mtoto wao basi abadili dini lakini Diamond hakuweza kufanya hivyo na kujikuta wakishindwa kufikia lengo la kufunga ndoa,” kilitambaa chanzo hicho. KIBA KAMA KAWA Kama kawaida yake, Kiba alipoulizwa juu ya ishu hiyo alikanusha vikali akidai kwamba hajawahi kuwa na mipango hiyo na mrembo huyo.“Ulishawahi kunisikia nikizungumzia ishu hiyo? Siyo kweli bwana…hakuna kitu kama hicho,” alisema Kiba akionekana ‘kumaindi’ kwa kuulizwa juu ya jambo hilo.Kwa upande wake Jokate hakupatikana hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea. TUJIKUMBUSHE Kwa muda mrefu, Jokate na Kiba wamekuwa wakiripotiwa kuwa ni wapenzi lakini Kiba amekuwa mstari wa mbele kukanusha huku Jokate akikiri kuwa jamaa huyo ni mtu wake.

Thursday, June 4, 2015

Jokate Na Ali Kiba hawafichi mapenzi yao tena


Jokate 2

Ujumbe ulioamsha team kiba 04 June 2015 ni wa Jokate kwa anayeaminika kuwa mpenzi wake mpya Ali Kiba uliosema ‘All The Best Chèri’ ikiwa ni ishara ya kumtakia siku njema kwenye siku yake anayofanya video nchini Afrika Kusini.
Ujumbe huu uliambatana na hii picha.
Jokate

Friday, March 27, 2015

WANAKWAYA: JOKATE ANATUTIA AIBU

Hamida hassan
Ile skendo ya kupiga picha za nusu utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii huku midume ikijirushia na kujifaidia kwa macho, ukijumlisha aibu mpya ya kukata mauno mbele ya wanaume, staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amewakera wanakwaya wenzake ambao wamedai kuwa anawatia aibu, Ijumaa lina mchapo kamili.Staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
TUJIUNGE KANISA LA SAINT PETER, OYSTERBAY, DAR
Ishu ya Jokate kutupia picha za nusu utupu mitandaoni si mpya, mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kwa tabia yake hiyo kiasi cha kuwakera wanakwaya hao wa kanisa analosali la Saint Peter lililopo Oysterbay jijini Dar.
Mbali na picha hizo, safari hii anaandamwa na skendo mpya ya kudaiwa kukata mauno mbele ya midume anapokuwa kwenye shoo zake baada ya kutumbukia kwenye muziki wa Bongo Fleva.
AJADILIWA KANISANI
Kwa mujibu wa baadhi ya wanakwaya hao, wamekuwa wakimjadili mara kwa mara hasa wanapokuwa mazoezini kanisani hapo mara baada ya mmoja wao kurushiwa picha za mwanadada huyo kwenye mitandao ya kijamii.
NI AIBU KWA KANISA?
Baadhi ya wanakwaya hao walikwenda mbele zaidi na kudai kwamba mbali na kuwa ni kioo cha jamii lakini bado ni alama ya kanisa hivyo ni aibu kwa kanisa pia kwa sababu binti aliyelelewa kidini kama Jokate hawezi kuwa na tabia za aina hiyo.
Jokate akiwa kwenye pozi.
AU BIASHARA MATANGAZO?
Kuna baadhi walidai labda mwanadada huyo anafanya hivyo ikiwa ni njia ya kujitangaza yeye na biashara yake bila kujali kama anaweza akajiondolea ute wake na heshima aliyoijenga kwa miaka mingi.

Thursday, January 22, 2015

JOKATE ACHEKELEA KUMBWAGA LULU

MWANAMITINDO na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo amekuwa tishio kwa msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa urembo na muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini.
Mwanamitindo na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo.
Mtandao mmoja wa hapa nchini umeendesha zoezi la kuweka picha zao kali zinazowaonesha wote wawili wakiwa na muonekano na picha kali huku wakiuliza nani zaidi ya mwenzake.Jokate ameibuka mshindi kwa kupigiwa kura tano huku watu wakimsifia kuwa ni wa kimataifa zaidi ambapo Lulu alionekana kupigiwa kura na mtu mmoja.
Msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Amani liliongea na Jokate ambaye aliwashukuru Watanzania kwa kumpenda na kumpa nafasi lakini aliwasihi kwa kuwaambia kuwa yeye aonavyo wote ni warembo.“Mimi naona sisi wote ni warembo, nawashukuru Watanzania walionichagua na kuniona nafaa,” alisema Jokate
Lulu alipotafutwa, hakupatikana.

Monday, January 19, 2015

WEMA ACHEKELEA KANDAMBILI ZA JOKATE

Stori: Imelda Mtema/Ijumaa Wikienda MBUNIFU wa mavazi na mtangazaji Bongo, Jokate Mwegelo amesababisha shosti yake, Wema Sepetu ‘Madam’ afurahi baada ya kumpelekea zawadi ya kandambili zake za Kidoti pamoja na vipodozi mbalimbali.
Jokate alisema Wema ni miongoni mwa watu ambao anawakubali kutokana na mchango mkubwa katika tasnia ya filamu Bongo, hivyo ameamua kumpelekea zawadi  ya bidhaa zake za Kidoti kuonesha heshima yake.

Monday, January 12, 2015

JOKATE:SIJAWAHI ‘BANJUKA’ NA MILLARD AYO!

Stori: Hamida Hassan
MTOTO mzuri mwenye taito kubwa katika anga la mitindo Bongo, Jokate Mwegelo ameucho molea vilivyo uvumi uliozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM.
Mtoto mzuri mwenye taito kubwa katika anga la mitindo Bongo, Jokate Mwegelo akipozi kimahaba na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM.
Uvumi huo ulianzia mitandaoni ambapo mwanahabari wetu alipomtafuta Jokate juzikati, aliweka plain ukaribu wake na Millard ambaye ni mtangazaji mwenye mvuto mkubwa kwa jamii.
“Millard ni mshkaji, namkubali kutokana na uchapakazi wake, anajua kujituma na ni mpambanaji lakini nje ya hapo hakuna cha zaidi,” alisema Jokate.

Friday, January 2, 2015

JOKATE: DIAMOND HANA AKILI TIMAMU

Stori: Imelda mtema
Staa wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ au ‘Jojo’ amemrushia maneno makali aliyewahi kuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa hana akili timamu kufuatia maneno aliyotoa kuwa enzi za uhusiano wao, eti mwanadada huyo alikuwa akichenga kumzalia mtoto.

Staa wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ au ‘Jojo’.
MAHOJIANO
Katika mahojiano maalum ya hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Runinga ya GlobalTV Online chenye makao yake makuu ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge, Dar, Diamond alitoa madai kuwa, amekuwa akihaha kupata mtoto.

Alisema kwamba, katika harakati zake hizo, warembo ambao alishatoka nao kimapenzi akiwemo Jokate walikuwa wakimchezea mchezo mchafu ili wasimzalie kwa kuwa alikuwa akiwaambia anahitaji mtoto kwa udi na uvumba.

Saturday, December 27, 2014

DIAMOND HANA UWEZO WA KUMPA MWANAMKE UJAUZOTO!

 
 
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Penny.
BAADA ya kudaiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa alichoropoa mimba zake mbili, mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kujibu mapigo kwamba mwanamuziki huyo hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
 
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu.
CHANZO CHA YOTE
Akizungumza na GlobalTV Online kwenye ofisi za gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar, hivi karibuni, Diamond alifunguka: “Nilimpa (Penny) mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hospitalini tukapime, akaambiwa anayo…nikafurahi nikampiga na ndinga (gari) mpya siku hiyohiyo, nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.

Friday, December 12, 2014

JOKATE AANIKA MAPENZI YAKE KWA JANUARI, ZITTO NA MILLARD

Leo kwenye safu hii tunaye mwanadada ambaye anaendesha maisha yake kwa kazi mbalimbali zikiwemo uigizaji, muziki, uanamitindo, ujasiriamali na utangazaji.
Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo akipozi.
Huyu ni Jokate Mwegelo ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006. Wiki hii yuko hapa kujibu maswali 10 ambayo mwandishi wetu Hamida Hassan alimuuliza na akatoa ushirikiano katika kuyajibu.
Ijumaa: Kuna madai kwamba sasa hivi unatoka kimapenzi na mtangazaji wa Clouds, Millard Ayo, hili unalizungumziaje?

Friday, December 5, 2014

JOKATE: NASIKIA RAHA KUKAA UTUPU NIKIWA CHUMBANI


Stori: Hamida Hassan
Modo ambaye pia anafanya muziki na ujasiriamali, Jokate Mwegelo amefunguka  kuwa, awapo chumbani na mpenzi wake huwa anasikia raha kutovaa chochote.
Modo ambaye pia anafanya muziki na ujasiriamali, Jokate Mwegelo.
Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Jokate alisema haoni aibu kusema akiwa faragha na mpenzi wake hapendelei kuvaa kitu kwani ni eneo la kujiachia.“Kwa kweli nikiwa chumbani na mpenzi wangu sipendi kuvaa kitu kabisa,” alisema Jokate kwa kifupi.

Saturday, November 22, 2014

JOKATE ATAJA SABABU ZA KUWA KARIBU NA WANAUME WENGI

MWANAMITINDO na mtangazaji kiwango Bongo, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa sababu kubwa inayomfanya awe karibu zaidi na wanaume ni marafiki zake wa kike kuwa nje ya nchi.
Mwanamitindo na mtangazaji kiwango Bongo, Jokate Mwegelo.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Jokate alisema amekuwa akipata malalamiko kutoka kwa watu wengi kuwa kampani yake kubwa ni wanaume hadi wengine kumuona ni malaya wakati si kweli.

Monday, October 13, 2014

MNIGERIA AOZA PENZI LA JOKATE

Kutoka moyoni! ‘Ubuyu’ mpya mjini ni madai ya staa wa muziki wa Nigeria, Panshak Zamani ‘Ice Prince’ kuoza akilitamani penzi la staa wa Kibongo, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
Staa wa muziki wa Nigeria, Panshak Zamani ‘Ice Prince’ kuoza akiwa na staa wa Kibongo, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
MNIGERIA ABEMBELEZA
Habari kutoka kwa vyanzo makini zilidai kwamba, Mnigeria huyo amekuwa akiwasiliana na kumbembeleza Jokate usiku na mchana akiomba wawe pamoja kwa jinsi moyo unavyomtuma.
Ilidaiwa kwamba hivi karibuni, Ice Prince anayekimbiza na ngoma yake ya I Swear amekuwa akitumbukiza vipande vya video kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram akimsifia Jokate ambaye anapendelea zaidi kumwita Kidoti.

Thursday, August 21, 2014

INASEMEKANA OMMY DIMPOZ ATEMANA NA DEMU WAKE WA ULAYA NA KUHAMISHIA MAJESHI KWA JOKATE, SOMA HAPA

Kupitia Gazeti la Makorokocho leo mezani tumepata story ya muda mrefu ya Penzi la siri kati ya Ommy Dimpoz na Jokate aka Kidoti.
stori hii ilivuja baada ya beef la chini kwa chini kati ya Jokate na mwimbaji mmoja wa kike ambae hawana maelewano mazuri na chanzo kikidaiwa kuwa ni mwanamuziki huyu wa kike (jina lake linaanzia na herufi V)
 
Mapenzi hayo yalianzia huko mikocheni A ambapo Ommy Dimpoz alikwa akiishi nyumba ya kushare na kila bibie kidoti alipokuwa akienda hapo watu walimuona na kuna kipindi dada yetu kidoti alikuwa akiminya ndani ya gari bila kushuka mahaba yakiwa tele kwenye gari hilo.
sasa wataalamu wa mambo wanasema dada yetu huyu anaonekana sana maeneo ya kinondoni katika mjengo wa kupanga wa star huyu wa ndagushima chande na mapenzi yao bado inasemekana yanaendelea chini kwa chini lakini nje nje.
ommy dimpoz ameingizwa kwenye list ya wanaume walio na mapenzi ya siri na dada yetu kidoti.
patamu hapoooo.
kama namiona vile
kukuta meseji za Mapenzi kati ya Mpenzi wake huyo na dada yetu kidoti.
Chanzo kinasema kidoti na Ommy Dimpoz walianza mapenzi ya siri kwa siri baada ya dada huyo kuachana na diamond.
 
Mapenzi hayo yalianzia huko mikocheni A ambapo Ommy Dimpoz alikwa akiishi nyumba ya kushare na kila bibie kidoti alipokuwa akienda hapo watu walimuona na kuna kipindi dada yetu kidoti alikuwa akiminya ndani ya gari bila kushuka mahaba yakiwa tele kwenye gari hilo.
sasa wataalamu wa mambo wanasema dada yetu huyu anaonekana sana maeneo ya kinondoni katika mjengo wa kupanga wa star huyu wa ndagushima chande na mapenzi yao bado inasemekana yanaendelea chini kwa chini lakini nje nje.
ommy dimpoz ameingizwa kwenye list ya wanaume walio na mapenzi ya siri na dada yetu kidoti.
patamu hapoooo.
kama namiona vile
CREDIT : SOUDY BROWN 

Friday, August 1, 2014

DIAMOND: SITAOA KAMWE, WEMA ANA CHAKE

CHANZO NI GLOBAL PUBLISHERS
Kutoka moyoni? Wakati bimkubwa Wema Isaac Sepetu akijiaminisha na kuhisi kuwa amepata mume ambaye ni baba bora, mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kuwa kamwe hafikirii kuoa, Ijumaa lina cha kukuhabarisha.
Wema Isaac Sepetu akiwa kwenye pozi la kimahaba na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Kauli hiyo ya Diamond inakuja wiki kadhaa baada ya Wema kuonekana na pete ya ndoa kidoleni kisha kukiri kuvishwa na ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva ambaye amerejea kutoka Marekani alikotwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki zilizokwenda kwa jina la African Muzik Magazine (AFRIMMA) 2014.

Thursday, May 15, 2014

JOKATE AHOFIA HOMA YA DENGU


MWANAMITINDO maarufu Bongo ambaye pia ni Mtangazaji wa Kituo cha Runinga cha Channel O cha Sauzi, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameweka wazi hofu aliyonayo juu ya gonjwa hatari la Homa ya Dengu ambalo limeshika kasi katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na paparazi wetu juzi jijini Dar, Jokate alisema anapata wakati mgumu sana  anapohisi anaumwa kwani huamini kuwa tayari amenasa homa hiyo.
“Ninauogopa sana huu ugonjwa wa Dengu maana nasikia ni hatari sana, basi mimi nikiumwa kidogo tu nahisi ndio tayari nimeukwaa na sijui hata unatibiwa vipi, naogopa sana kufa,” alisema Jokate.
CHANZO NI GPL

Wednesday, February 5, 2014

BIFU LAO KWA DIAMOND... JOKATE AMWANGUKIA WEMA


WERAWERAA! Staa wa Bongo anayesumbua kwenye mitindo na sinema, Jokate Mwegelo amekubali kushindwa baada ya kumwangukia Wema Sepetu waliyekuwa kwenye bifu la kimyakimya wakigombea penzi la Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Jokate akiwa sambamba na Wema.
Tukio hilo la kufungulia mwaka lilijiri wikiendi iliyopita jijini Arusha, katika kiwanja cha kulia bata, Triple A Club ambapo Wema alikuwa akimtambulisha mwanamuziki Miraji Hussein ‘Mirror’ kutoka Lebo ya Endless Fame Production.
Wema aikumbatiana na Jokate.

Wednesday, December 4, 2013

Friday, November 22, 2013

WEMA, JOKATE WAMPONZA DIAMOND


Gumzo kubwa kwenye harusi ya staa wa dunia katika Kundi la P-Square wanaotarajiwa kuangusha shoo Bongo kesho, Peter Okoye mwishoni mwa wiki iliyopita, ni mwaliko wa msanii pekee wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye alipondwa kwa kuvaa suruali ‘njiwa’ (ya ajabuajabu).
Wema Isaac Sepetu.
Ishu hiyo ilijiri huko Lagos, Nigeria ilikofanyikia sherehe hiyo ambapo Peter alifunga ndoa ya kimila na mrembo wa haja, Lola Omotayo huku Diamond akipata fursa ya kukutana na baadhi ya mastaa wakubwa duniani, kasoro pekee ikawa kwenye mavazi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Diamond alichemka kwa kuvaa kivazi hicho kifupi miguuni kikiwa na mistari myeupe na myeusi hivyo kusababisha kutukanwa mitandaoni.

WEMA, JOKATE KIVIPI?
Huku wakitumia picha za waliowahi kuwa wapenzi wa Diamond, Wema Isaac Sepetu na Jokate Mwegelo wakiwa wamevaa ‘taiti’ kama ‘kisuruali’ cha mwanamuziki huyo, walieleza kuwa inawezekana wao ndiyo walimdizainia hivyo kumsababishia matusi ya nguoni katika mitandao ya kijamii.
Jokate Mwegelo.
“Mafashenista wengi wanamtukana Diamond lakini inawezekana na zile nguo kadizainiwa na Wema au Jokate kwa sababu ni staili zao. Nao wana nguo kama hizo, hebu cheki kwenye picha,” alisema mmoja wa wachangiaji wa mada hiyo katika mitandao ya Naija huku akitundika picha za Wema na Jokate wakiwa wamevaa kama Diamond.

Monday, November 4, 2013

MSIBA WAWAKUTANISHA WEMA, JOKATE

LICHA ya kuwa waliwahi kupokonyana bwana (Nasibu Abdul ‘Diamond’), mwigizaji Wema Sepetu na  mtangazaji Jokate Mwegelo wamekutana katika msibani na kupiga stori.
Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa meneja wa Wema, Martin Kadinda, Jokate aliibuka Jumanne iliyopita usiku kwenye msiba wa baba Wema uliochukua nafasi nyumbani kwao Sinza-Mori jijini Dar na kumfariji hadi usiku mnene.
 
Jokate Mwegelo.
“Fani ya urembo na ubunifu ni fani za watu makini sana ambao chuki kwao ni mwiko, nimefurahishwa na kitendo cha Jokate kuja msibani kwani anaonyesha dhahiri kuwa ni mtu mwenye huruma na imani,” alisema Kadinda.
HABARI NA GPL

Friday, September 13, 2013

JOKATE AELEZA SIRI YA WANAUME KUMGANDA

MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
 
“Kujiamini ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.
 
“Kujitegemea ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
 
Jokate alisema sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.
 
Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.
 
Gazeti hili liliwasiliana na Jokate kuhusiana na maandiko hayo ambaye alijibu; “Hahaha….sina comment hapo aisee…”
Jokate pia ni mwanamitindo, msimamizi wa shughuli mbalimbali katika kampuni yake ya Kidoti iliyozinduliwa mwaka jana.
Credit: GLP

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate