Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Stori: Musa Mateja Imevuja!
Kumbe kile ‘kibendi’ cha staa wa sinema za Kibongo, Jennifer Kyaka
‘Odama’ ni cha kigogo mmoja serikalini na ndiyo sababu kubwa ya
mwigizaji huyo kufanya siri nzito juu ya ujauzito huo.
Kama mbu
aenezavyo ugonjwa wa malaria, ndivyo rafiki wa karibu na msanii huyo
alivyotunyetishia juu ya usiri huo huku akisisitiza hifadhi ya jina.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu mwanzoni mwa wiki hii,
rafiki huyo alisema kwa sauti tulivu kuwa mimba ya Odama ni ya bosi
mkubwa wa moja ya wizara nyeti hapa nchini (jina na wizara vinavunda
kwenye droo zetu) na kwamba moja kati ya masharti magumu aliyompa ni
kuhakikisha jambo hilo linabaki kuwa siri hadi Yesu atakaporudi.
Ilisemekana kuwa usiri huo unatokana na madai kwamba kigogo huyo ni mume wa mtu.
Akiendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi, ‘kikulacho’ huyo alisema
licha ya Odama kupata huduma zote bora anazostahili mjamzito lakini hana
raha kwani furaha ya mjamzito ni pamoja na kumnadi mhusika wa ‘mzigo’
jambo ambalo limekuwa likimnyima raha.